Prof. Kabudi awataka Mabalozi kujipanga na kutafuta fursa za masoko ya bidhaa za Tanzania

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,203
5,611

Mabalozi wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nje ya Nchi wameelekezwa kujipanga, kushiriki na kutafuta fursa zitakazowezesha bidhaa mbalimbali za Tanzania kupata masoko ya uhakika katika nchi walizopo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wakati akizungumza na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na kuongeza kuwa , Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatamka bayana juu ya diplomasia ya uchumi sambamba na kuimarisha sauti ya Tanzania na taswira yake katika medani ya uhusiano wa kikanda na kimataifa.

Prof. Kabudi ameongeza kuwa ili kufanikisha hilo Balozi zinapaswa kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika jumuiya nyingine za kimataifa zikiwemo, Indian Ocean Rim Association, Indian Ocean Tuna Commission, South South Commission, South West Indian Ocean Fisheries Commission.

Aidha amewataka Mabalozi hao kuzingatia maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyoyatoa wakati akizundua Baraza la Wawakilishi ya kutaka Uchumi wa Bluu kupitia uvuvi wa Bahari Kuu unakuwa na manufaa kwa Wananchi hususani katika kuongeza mapato, ajira na kukuza uchumi kwa kuzingatia kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni ya Muungano.

Pia Prof. Kabudi amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) katika maendeleo ya Taifa na kuzielekeza Balozi zianze na ziboreshe kanzi data ya Diapora ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kuanzisha Jumuiya zao.

“Natambua kazi hiyo inaendelea na kwa sasa tuna data za diaspora takriban 98,658 na kuna jumuiya 77 za diaspora. Nichukue fursa kusisitiza umuhimu wa Balozi zetu kuboresha na kuharakisha zoezi hili kwa kubuni njia mbalimbali za kuwaandikisha”.Amesema Prof. Kabudi

Mkutano huo wa Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi umehudhuriwa pia na Naibu Waziri, Mhe William Tate Ole Nasha,Katibu Mkuu Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 
Hakuna kiongozi namuona hamnazo na haifai kuwepo kwenye serikali ya mh rais mama yetu Samia kama huyu kabudi .yani ni mchumia tumbo sjui alisomeaga nn huyo propesa wa jalalani.
 
Huyu kwanza CCM kaujulia wapi ?

Maushari wa Diaspora waliyakalia now wanajifanya wanatambua michango yao... mpuuzi sana huyu... Watu wamewanyang'anya mali zao kwa kupoteza uraia wao wameomba duo citizenship wamekataa afu nani aingie mkenge? Mama Samia bora aondoshe Nawaziri fuata upepo haswa hawa wenye Elimu bila akili
 
Hakuna kiongozi namuona hamnazo na haifai kuwepo kwenye serikali ya mh rais mama yetu Samia kama huyu kabudi .yani ni mchumia tumbo sjui alisomeaga nn huyo propesa wa jalalani.
Wengi mnao kashifu mawaziri na viongozi wengine wa awamu ya tano, tukifatilia elimu zenu wengi wenu ni form2/form4 basi, Watanzania walio soma mpaka vyuo vikuu hawawezi kupoteza muda wao wanakashifu, beza beza binadamu wenzao wanatumia lugha ya mipasho ya taarabu kama ya Khadija Kopa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…