Prof Janabi awekwa mtu kati

Prof.Janabi akiambiwa uongo wake na Mkali wa Bio-Chemistry View attachment 3309840
Watanzania tujifunze namna ya kuchakata taarifa siyo kila tunachokiona mitandaoni tunakibeba tu.
Sasa huyu mzungu ameonyesha uongo gani wa alichosema Janabi? mbona kwenye video ameenda tu expand na kutolea maelezo zaidi yale aliyoyasema Prof.

Tuzingatie kwamba Janabi alikua naongea kwenye hadhira ya watu ambayo angeanza kubreak down hizo molecules wasingemuelewa, ametumia glocose kwenye maelezo kwa sababu ni aina ya sukari inayojulikana zaidi na watanzania kuliko hizo nyingine.

Kwenye Muktadha wa nutrition, kula mchanganyiko wa matunda (fruit salad) kunasababisha kuconsume kiasi kikubwa cha sukari kwa sababu matunda yanatofautiana viwango vya aina za sukari zilivyonavyo. Kijiko kimoja kidogo cha sukari ni gramu 5, sasa fikiria ukijaza bakuli la mchanganyiko wa matunda umeweka ndizi, zabibu, embe, nanasi na machungwa, unakula gramu ngapi za sukari kwa mlo mmoja (matunda yana virutubisho na faida nyingi kwenye lishe hasa kwenye kutengeneza mlo kamili, ila ni muhimu yaliwe kwa kiasi).

Huyu mzungu anawapotosha na watu mnashupaza vichwa tu kijinga jinga, "za kuambiwa changanya na zako, sivyo utapoteana mjini hapa".

"Jedwali la kiwango cha sukari kwa kila gramu 100 ya matunda"
Sugar levels in fruits.png
 
Au tunashadadia kwa vile amesema mzungu? Ina maana Tanzania hatuna wasomi waliokuwa wanafahamu hizo hoja anazokuja nazo mzungu? Ni vipi kama Janabi alikuwa anazungumzia hakuna ulazima wa kuchanganya matunda kama kote unaweza kupata fructose, maltose na sucrose? Hatuoni kama ukiyachanganya unaweza kuzidisha kiwango kinachojitajika na mwili? Wacha nisubiri wanafunzi wa Prof. Janabi wanavyoweza kumnasua mwalimu wao katika hili!
Hata mimi nimeshangaa sana, sasa prof angeanza kuelezea haya 👇 kwenye hiyo hadhira watu wangemuelewa.

Screenshot 2025-04-20 at 10.29.53.png

ila nimelijibia kwa urefu hapo juu Prof Janabi awekwa mtu kati japo mimi sikua mwanafunzi wa Prof. 😅
 
Prof.Janabi akiambiwa uongo wake na Mkali wa Bio-Chemistry View attachment 3309840
Ushauri wangu,kula matunda,aka vitu vya asili zaidi kuliko vyakula vya viwandani aka processed food,fanya mazoezi,pumzika angalau masaa 7, kwafupi kila unachokula kula/kunywa Kiasi itakusaidia sn kulinda mwili wako.
Hizo food composition waachie wenyewe wajidanganye,hapo kemia lazima iwe nzuri bila hivyo utaishia kua umekariri vimstari 3 ukajiona mwamba
 
Back
Top Bottom