Prof. Baregu: Prof. Kabudi na Humphrey Polepole mkitusaliti kuhusu rasimu ya Warioba tutawashangaa

Hapo ndo siasa zinanichosha kwa unafiki wa wanasiasa.
Hajaona usaliti uliofanywa na chama chake kwa kuwapokea mafisadi walioikataa katiba mpya walipokua ccm sasa mishipa imemshupaa kwa wenzie waliopata kibarua.
Mjinga gani atakusikiliza wewe Baregu aache kumsikiliza mwajili wake serikali?
Nyambafu kabisa...
Yaani ukiona jitu zima na ma_degree yake linaongozwa na mtu aliyepata zero utaona hata elimu haina maana.
My god! But why all these insults? Hivi haya matusi yanajibu hoja kwamba wajumbe wa Tume ya Warioba waliopata kazi ccm na serikalini wanatarajiwa na wananchi waendelee kutetea maoni ya Watanzania kuhusu katiba mpya? Sitegemei hata kidogo Polepole na Prof. Kabudi wanaweza kuwa na mtazamo duni na dhalili kama ya Uamifukazi. Mara kadhaa Polepole ameshaweka wazi msimamo wake kuhusu rasimu ya Warioba. Kama alivyodokeza Lissu, rasimu ya Warioba inayo mchango mkubwa wa Prof. Kabudi na sidhani kama rais kamteua kwa lengo la kumnyamazisha.
 
Prof Baregu amewataka waliokuwa wajumbe wa tume ya katiba Prof Kabudi na Polepole kutosahau msimamo wao ndani ya tume.

Amesema baada ya tume kuvunjwa, yeye pamoja na Warioba, Kabudi, Butiku na Polepole waliendelea kufanya mikutano ya kuhamasisha rasimu ya Warioba chini ya mfuko wa Mwalimu Nyerere.

Amesema yeye aliamini ktk serikali moja na Warioba aliamini ktk serikali mbili lakini UKWELI waliokutana nao uliwafanya wabadilike.

Hivyo amewatahadharisha endapo wataisaliti rasimu ya Warioba, wananchi watawashangaa.Wewe unalisemeaje hili?Karibu

Chanzo: ZITV
mkuu, mtu yeyote akipewa shavu na lile genge la kijani/njano, akili yake inakuwa possessed kama mtu aliyeingiwa na pepo.
Polepole na Kabudi ndiyo tushawapoteza hivyo kwenye suala la katiba mpya.
 
Mbona Baregu alibadili msimamo wake dhidi ya FISADI MKUU na akaanza kumtetea tena mbele ya BUTIKU??

Kwa nini vijana wa siku hizi mmekuwa wepesi wa kutoa majibu rahisi kwenye maswali magumu?
Naamini Prof Kabudi mwenyewe anatumia muda mwingi kuwaza ushauri huu hasa anapoangalia mustakabali wa Taifa.

Ifikie mahali hata ktk siasa tuwe kwenye baadhi ya mambo tutangulize maslahi ya Taifa mbele hata kama kunaweza kuwa na tofauti ya itikadi. Katiba ni zaidi ya chama, ni zaidi ya nafasi ya uongozi aliyonayo mtu,na ni zaidi ya utani na kebehi za kitoto tunazoziendeleza.
 
Ccm waliidhinisha mabilioni kuandaa katiba halafu wakachomekea ya kwao waliyoiandaa lumumba hivyo huku wakijisifu kuwahadaa wananchi. Watanzania tuwaulize ccm ipo wapi katiba ya Warioba?
 
Back
Top Bottom