Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,498
- 7,048
Prince Rahim Al-Hussaini, anayejulikana pia kama Prince Rahim Aga Khan, ametangazwa rasmi kuwa Imam wa 50 wa Waismailia wa Kishia baada ya kufunguliwa kwa wosia wa baba yake, Prince Karim Aga Khan IV, Jumatano. Tangazo hilo limetolewa na Aga Khan Development Network (AKDN).
Uteuzi wake unafuatia kifo cha Prince Karim Aga Khan IV, aliyefariki Jumanne jijini Lisbon, Ureno, akiwa na umri wa miaka 88. Lisbon ni makao makuu ya Imamat ya Waismailia.
Prince Rahim Aga Khan alizaliwa Oktoba 12, 1971, na ni mtoto wa kwanza wa marehemu Aga Khan IV na Princess Salimah, aliyewahi kuwa mwanamitindo wa Uingereza. Amejihusisha kwa muda mrefu na shughuli za maendeleo kupitia AKDN, hasa katika masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi.
Soma: Aga Khan Afariki dunia akiwa na Miaka 88
Jamii ya Waismailia ina zaidi ya wafuasi milioni 15 duniani, wanaoishi katika Asia ya Kati, Mashariki ya Kati, Kusini mwa Asia, Afrika, Ulaya, na Amerika Kaskazini.
Marehemu Aga Khan IV alikuwa Imam wa 49 wa Waismailia, akijulikana kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya jamii na utajiri wake. Mbali na uongozi wa kiroho, alikuwa mpenzi wa mbio za farasi na mfadhili wa miradi mingi ya maendeleo duniani. Alizaliwa Desemba 13, 1936, jijini Geneva, Uswisi, lakini sehemu ya utoto wake aliitumia Nairobi, Kenya, kabla ya kurejea Uswisi kusoma na hatimaye kujiunga na Harvard University kusomea historia ya Uislamu.