Chakochangu
JF-Expert Member
- Mar 21, 2011
- 2,668
- 2,164
Mugabe angejenga heshima kama angestaafu siku nyingi. Hali ilivyo hana tofauti na Nkurinziza na Dr Shein.
Mimi kwa mawazo yangu naona Mzee Robert Mugabe hataki kuachia madaraka sababu ni kwamba
katika kuchunguza kwake ndani ya chama chake au hata upinzani hajaona mtu wa kufuata sera zake za kupinga Ukoloni mkongwe na Ukoloni mambo leo.
Hivyo ameona ni bora afie pale kwenye kiti, hao watakao shika usukani baada yake hata wakilamba miguu ya Wakoloni yeye hatakuwepo hivyo haitamuuma sana.
Nafikiri kwa wale wazee au wengi si mnakumbuka Mwalimu J K Nyerere alivyokuwa anasononeka kuhusu Marais waliomfuatia yaani Mzee Mwinyi na Mkapa walivyoongoza hii Nchi na kuikabidhi kwa Mabeberu ya Magharibi?
Sasa mambo kama hayo Bob Mugabe hataki yamkute yu hai. Hao waje wakute Kaburi lake tu.