Premier Betting Tanzania acheni Utapeli na Usumbufu

mtoromkuu

Senior Member
Mar 7, 2015
147
39
Mimi ni mmoja wa wadao wanaofanya michezo ya betting kupitia makampuni ya betting hapa Tanzania, cha kusikitisha kuna kampuni moja kubwa ya betting hapa nchini inajulikana kwa jina la PREMIERE BETTING.

Kampuni hii kadri ya siku zinavyokwenda huduma zake zinazidikua kero, za kitapeli na dharau kwa wateja, ni as if kampuni hii haina viongozi au ni kama vile wateja wake uwa wanapewa msaada tu kupata huduma bila kulipia malipo yeyote!

Mfano mzuri ni katika uendeshaji wake wa kutoa malipo pale mteja anaposhinda ticket yake, ulipwaji wake umekua ni wa hovyo kabisa, unaweza ukafuatilia malipo kwa kituo kama cha Kawe kila ukienda wanakuambia hawana hela.

Unaweza ukafuatilia ulipwe wiki mbili nzima kila siku utaambiwa hawana hela, ila ukweli ni kuwa kwa wale wa Kawe uwa wana wateja wao maalum ambao wanawapigia simu kuwa wazuie hela kwa kuwa watakuja chukua na kuwapatia mgao kidogo, so kwa wewe usietaka kutoa rushwa hautohudumiwa hata kama ni zaidi ya mwezi labda uende makao makuu Kariakoo.

La pili kituo hiki hiki cha Kawe kuna mvulana ambae uwa anatoa huduma kuanzia mchana, uwa hajui kabisa customer care, ana majibu mabovu kwa wateja, ana lugha za matusi kwa wateja na huyu ndie kinara wa kusema hatuna hela ili hali jamaha zake wakija anawapatia malipo na wanampa chochote.

Nataka uongozi wa premier betting ufuatilie mapungufu haya kwa kila tawi lake husika hasa kuanzia Kawe na wamuangalie sana huyu kijana aliyekosa si elimu tu bali hata uelewa na nidhamu ya kazi pia, anawaharibia sana.

Pili hata office yao ya Kariakoo imejaa rushwa tupu, ni kama vile uongozi unazuia hela kupelekwa kwenye matawi mengine ili wateja warundikane Kariakoo na iwe rahisi kwa wafanyakazi wao wapate mianya ya kupata rushwa kwa wateja wasiotaka usumbufu!

Kifupi ninaomba baraza la bahati nasibu la taifa na taasisi ya kuzuia rushwa walimulike na kufuatilia kampuni hii ya Premier Betting inayoendesha shughuli zake kisanii sanii.
 
Mkuu bora umeliona ili suala,hawa jamaha ni wababaishaji kupita kiasi!ukweli wanakera,Merridian wako vizuri kuliko hawa wababaishaji!tena yule jamaha wa Kawe ndio m.p.u.u.z.I kuliko wote,anajisikia na kujibu hovyo wateja sijui kwa kipi alicho nacho!kweli kukosa elimu na kua lofa ni kitu kbaya sana
 
Mkuu bora umeliona ili suala,hawa jamaha ni wababaishaji kupita kiasi!ukweli wanakera,Merridian wako vizuri kuliko hawa wababaishaji!tena yule jamaha wa Kawe ndio m.p.u.u.z.I kuliko wote,anajisikia na kujibu hovyo wateja sijui kwa kipi alicho nacho!kweli kukosa elimu na kua lofa ni kitu kbaya sana

Mkuu ni bora Meridian wangejipanua na kua na matawi mengi tu,wale jamaha wako so modern na hawana longolongo kabisa,ila natafuta means ya kuwasiliana na ngazi za juu kuanzia Premier betting wenyewe na shirika bahati nasibu la taifa kuwapa fact juu ya madudu haya
 
Kawe chamtoto. kuna malaya mmoja. kimaramwisho. ukishinda 83000.-82000=yaani anatoa. zenye 70-80-50 alt..hizo 3000-2000 anadai zinachangia ofisiyao mpuuzikwelii
 
Ilausikazoeesana hasa kipindihiki chelsea na yangaq washachukua ubingwa.. mimba
 
Last edited by a moderator:
jiungeni meridian betting online lazima uwe na email,kisha fungua meridian.co.tz hata humu wamo kwenye jukwaa la kubet kisha unajiunga nao kwa web site yao kisha watakutumia email na utafungua account yako thru maelezo ya email waliokutumia na utaanza kubet
 
Naomba kuuliza kati ya kununua na kuuza hisa na kucheza iyo betting ipi inamanufaa zaidi...kwako, familia yako na vizazi vijavyo?....
 
Back
Top Bottom