Precision Air na matatizo yao: Wanaelekea wapi?

ATCL....... huu ni wakati wa kurudia enzi za kuwa ndege bora angani....!
 
Kinachotakiwa sasa ATCL wachukue fulsa hii ya kusuasua kwa Precisson Air ili kujiweka sawa Kibiashara.
 
mkuu nyau
--------------------------------------------------------------------------------

Sio majungu. Ni kweli, ndege huahirishwa pale kunapokuwa na tatizo - kwa ajili ya usalama wa abiria.

Lakini unaelezaje pale unaporipoti kwa ajili ya safari na kuambiwa ndege imeshaondoka? Binafsi hii imenitokea mara mbili kwa Precision Air. Reporting time ni saa 12 na nusu asubuhi, departure saa mbili. Nikafika airport saa 12 na dakika 45 asubuhi nikaambiwa ndege imeshaondoka! That day 15 passengers tulikuwa stranded. The next time that happened to me, 9 passengers were stranded.

Hili nalo ni jungu? It happened to real people - frequently.

Ingelikuwa ni mara moja moja watu tusingililalamika, kwa kuwa inaanza kuwa ni the rule rather than the exception - flight cancellation - ndio maana watu wana voice frustrations zao na hii hali. Myself included!

Nyau

Hilo tatizo lipo sana kwa hawa waheshimiwa wa precission;labda nikuelekeze kinachofanyika wamewahahidi travel agent hela nzuri iwapo kama watakuwa wkaiijaza ndege yao na pia kila abiria anaetaka kwenda na atcl aambiwe ndege iko kancelled.......................................
sasa wanachofanya wanauza hata kama wanona kwenye sysytem imejaa ilimradi ndege ijae ndipo sasa basi.....wanaweza kuwaona kwenye system ndege imejaa lakini wakiwa wanajua wana flt nyingine baadae ya mwanza kuliko kuwaacha wanawasakazia different time ili wakibaki wanadumbukia ya mchana ;;sasa nafikiri kunatakiwa kuwepo na sheria ya kuwabana washenzi kama hawa travel agent wanaodanganya muda abiria.....kama wanajua ndege inaondoka saa 2 wanatakiwa kuwahi masaa mawili kabla iweje wanaaandika muda tofauti
 
mwaka juzi nilikata tiketi na kupanda precision air ATR 42, niliripoti airport saa moja ili niondoke saa 2 from dsm to kia. however, tuliombwa msamaha kuwa kuna technical problem, hivyo tukaondoka saa tatu, na rubani akatutangazia kuwa kila kitu kiko ok. tukiwa hewani just kama 10 minutes ngede ikaanza kutoa moshi mweupe nyuma, yaani ndani ya ndege, moshi ukawa mwingi na ikalzamu rubani airudishe ndege back to mwalimu nyerere airport. kile kihoro kikanifanya niachane na ile safari ingwa walikuwa wako tayari kutufaulisha kwenye ndege nyingine. sababu ya kutoa moshi eti walisahau grease juu ya air conditions wakati wanafanya service, hivyo ndege ilipowashwa na kuruka ile grease ikaana kuuungua na kutoa moshi.

sijawahi kuipanda tena hiyo precision na tiketi nikawaachia

Ndugu yangu mimi pia yalinipata mwaka 2007 october 15. Nilikuwa natoka KIA to Nairobi halafu nairobi to Lusaka lakini pale kia Precision air ATR 42, ilikuw tuondoke saa 12.30 asubuhi lakini kabla hata hatuja panda tukaambiwa tusubiri, wakaiwasha ikawaka, tukaambiwa ndege sasa iko tayari tukapanda kabla hata hawajafunga milango, tukaambiwa teremkeni ndege ina matatizo. baada ya kama dkk 20 tukaambiwa imekuwa tayari, basi mpaka nafika Nairobi, mwili haukua wangu.

Kingine ni kwamba Precision air wasipo angalia Kenya Airways itachosha ndege zao na wakisha kosa ndege, soko lao watalichukua.
 
tuwape moyo precision ..kwani kampani hii ya wazawa ikifa basi ..tanzania tutabaki hatuna ndege kabisa....precision wako imara ......ndio mkombozi wetu ....scenerio moja isiwe ndio ..general
 
Precision Air ni kampuni binafsi ambayo haipati msaada wowote kutoka serikali, Air Tanzania inatanua kwa pesa zetu walipa kodi na tena wanafuja sana pesa. Mi nasema kheri entreprenuers kama Precision kuliko Air Tanzania mara 20! Katika entreprenuership kuna kukosa na kupata lakini naheshimu juhudi za mtu kuanzisha kitu chake na kukipalilia.

Kitu wanachohitaji Precision ni kupata operations manager mzuri. Inaonekana hawajui jinsi ya kupanga route vizuri ili safari zao ziwe zinalipa. Pia suala hili la kuacha wasafiri check in counter nimelikuta hata mimi na ni kitu ambacho inabidi walichunguze kwa makini sana. Huwezi kumzuia msafiri eti kwa kisingizio chochote. The person is at the counter, bdege haijaondoka, take the passenger!

ATC ni afadhali ife kifo natural lakini tukishindwa tuipatie euthanasia! Imenyonya pesa zetu nyingi sana kwa mafanikio madogo au nil. Katika world economy ya leo, serikali chache sana zinaweza kuendesha their own airline. In fact ni serikali zenye mafuta za middle east ndo zimeonyesha uwezo huu, hata serikali za nchi za Ulaya kama Ujerumani, Uswisi zimeshindwa kumudu gharama.
 
Tatizo sio precision au ATCL, tatizo ni kitu chochote kinachoongozwa na mbongo per se... lazima kiwe na matatizo.

Sijui tumerongwa, tumelaaniwa, au tumejiloga au tumejilaani... I'm lost

I rest my case.
 
Nimesoma leo kwenye Guardian precision wamekuwa quoted wakisema kuwa hawana matatizo yoyote. wanasema ndege zao ndogo nyingi zipo kwenmye matengenezo na kufutwa kwa safafri kunatokana na kupungua kwa abiria katika kipindi hiki ambacho si cha msimu (wa utalii?). wamewaahidi wateja wao kuwa mambo yatarejea kuwa ya kawaida msimu utakapoanza
 
Kumbe target market yao ni watalii sasa nyie wabongo mnafuata nini ?
 
Huko nyuma imewahi kuripotiwa kuhusu ubovu wa ndege za PRECISION, nilichangia na nikatoa ushahidi kuwa I WAS ONE OF VICTIM. leo yamenikuta tena, safari yetu ya MWANZA - DAR imegeuka upepo, wakati tukiwa tumeisha check in na mizigo kupakiwa kwenye ndege mara tunaambiwa safiri haipo, tatizo? Engine moja haionyeshi kwenye DASH BOARD. hilui ni tatizo la kawaida lakini najiuliza WHY PRECISION? tena kwa mfululizo? wamwzidiwa? Airline business ahina faida siku hizi mpaka hatuna many players in the domestic market? KUNA NINI JAMANI? Mungu tunusuru. TUOMBAEANE JAMANI KESHO NAENDA KUPANDA TENA.
 
Precision air might've broken its promise to fly you to Dar or even broken your heart but this surely isn't breaking news now is it?
 
Precision air might've broken its promise to fly you to Dar or even broken your heart but this surely isn't breaking news now is it?
This has just happened some minutes before the posting, being a breaking news or not will depend on your perception pole kama nimeigusa kampuni yako.
 
Huko nyuma imewahi kuripotiwa kuhusu ubovu wa ndege za PRECISION, nilichangia na nikatoa ushahidi kuwa I WAS ONE OF VICTIM. leo yamenikuta tena, safari yetu ya MWANZA - DAR imegeuka upepo, wakati tukiwa tumeisha check in na mizigo kupakiwa kwenye ndege mara tunaambiwa safiri haipo, tatizo? Engine moja haionyeshi kwenye DASH BOARD. hilui ni tatizo la kawaida lakini najiuliza WHY PRECISION? tena kwa mfululizo? wamwzidiwa? Airline business ahina faida siku hizi mpaka hatuna many players in the domestic market? KUNA NINI JAMANI? Mungu tunusuru. TUOMBAEANE JAMANI KESHO NAENDA KUPANDA TENA.

...Tanzania ni nchi ya miujiza. kila jambo linawezekana hapa
pole sana
 
Tatizo sio precision au ATCL, tatizo ni kitu chochote kinachoongozwa na mbongo per se... lazima kiwe na matatizo.

Sijui tumerongwa, tumelaaniwa, au tumejiloga au tumejilaani... I'm lost

I rest my case.

"Miafrica ndivyo tulivyo"
 
Hayo ni mambo ya kawaida tu,yanatokea kila sehemu.

"Kila sehemu" ni wapi huko????

tusilee uzembe! remember we pay for its service, thus we need the value for our money. Time is also a valuable resource by cancellation means a resource has been wasted.
 
"Kila sehemu" ni wapi huko????

tusilee uzembe! remember we pay for its service, thus we need the value for our money. Time is also a valuable resource by cancellation means a resource has been wasted.
Marekani, Uingereza, SA etc. Ndege ni mashine na inaweza ikaleta tabu mara moja moja.
 
Back
Top Bottom