Nawapa pongezi sana lakini wasiwasi wangu ni umri wa hiyo ndege na matengenezo yake yako vipi? Nawaomba maofisa wa TCAA waifanyie uchunguzi ndege hiyo kabla haijatua bongo. Ni ndege kubwa kwa safari za medium range kama south na Dubai. Keep it up precision.
Nami nawapongeza sana hawa. Ni kampuni pekee ya Kitanzania tunayoweza kujivunia ambayo imeweza kutoa ushindani katika sehemu hii ya dunia!
Let us support our lovely wing of Kilimanjaro (air Tanzania with a leased Airbus 320-214). Hii mapato yake tunauhakika yanarudi serikalini kwa maendeleo ya Taifa.
Hapana .......
Njia ya kuhakikisha kwamba fedha hizi zinarudi serikalini kwa ajili ya maendeleo ya taifa ni kwa kulipa kodi, na kwa kutoa ajira kubwa zaidi n.k. Anayechangia hivyo zaidi anachangia maendeleo zaidi, huo ndiyo ukweli ulio wazi. Kwa hiyo kampuni inayokua na kuendelea ina nafasi nzuri ya kufanya vyote hapo juu.
Sasa hawa wa ATCL, badala ya kuchangia serikalini, Serikali ndiyo inawapa ruzuku, kwa maana nyingine wananchi tunawachangia. Hata kodi hawataki kulipa, hivi karibuni TRA waliwapeleka mahakamani kwa kutotaka kulipa kodi ya TZS bilioni mbili!
Wasafiri tuwe na moyo wa utaifa.
Ndiyo, hili naunga mkono mia kwa mia, lakini kwa kampuni zetu zinazoweza kuchangia maendeleo. Tuombe Mungu ATCL iweze kufanya hivyo. Mimi binafsi siamini ATCL ina uwezo huo. Tusubiri matokeo miaka 2!
Kuhusu hisa za Precision kwa Wakenya ... sidhani kama ni jambo baya, as long as bado huyo mtanzania (siyo mchagga - how lowly!) anazo controlling shares. Huo ndo uwekezaji tunaotaka, wenye maendeleo kwa Taifa.
Asanteni