Pongezi za nini ilhali ni haki ya kikatiba?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
93,475
119,287
Inavyoonekana yale maandamano ya CHADEMA yaliyopangwa kufanyika keshokutwa, yatafanyika.

Sasa nimeanza kuona eti pongezi anapewa Rais Samia!

‘Whims’ za Samia ndo zimekuwa haki za kikatiba au?

Hakuna haja yoyote ya kumpongeza mtu kuhusu kitu kilichopo kwenye katiba ya Tanzania.

Haki zilizomo kwenye katiba ni haki za Watanzania wote.

Baadhi ya Watanzania wakitaka kuzitumia haki hizo, madhali ni kwa amani, hapaswi kuletewa figisu.

Hivi kweli unaweza kumpongeza jambazi kwa kutokukupora mali yako?

CCM wanakiuka katiba kila mara. Ikitokea kwenye jambo hawajakiuka katiba, mnawapa pongezi za nini?

Kuacha watu wafaidike na haki za kikatiba is the bare minimum.

Hivi ni kweli kuna Watanzania wanaona ni sawa kupongeza hata yale matakwa ya chini kabisa ya kikatiba yanapoacha kuporwa na CCM?

Tatizo ni ujinga au ukondoo? Au ni vyote kwa pamoja?

SMFH!

=================
For English Audience

CHADEMA demonstrations scheduled for tomorrow will occur, and there is a growing trend of praise directed towards President Samia. The questions rose is the constitutional rights of all Tanzanians, and questions why people should be praised for their constitutional rights, especially when they are violated by the Central Bank of Tanzania (CCM).
 
Mkuu Nyani, kwani hujui Rais wa Tanzania yupo juu ya sheria?

Kwani miaka ya 2018 hadi 2021 wakati yanapigwa marufuku hayo maandamano hakukuwa na huo Uhuru wa Kikatiba?

Rais wa Tanzania ni Kama Mungu, maana huwezi kum_challenge kwa lolote, maana Katiba yenyewe sio lolote wala Chochote kwake
 
Mkuu Nyani, kwani hujui Rais wa Tanzania yupo juu ya sheria?

Kwani miaka ya
Hapana.

Kiukweli Rais wa Tanzania hayupo juu ya sheria.

Na licha ya katiba kuwa mbovu, bado madaraka ya Rais yana mipaka.

Tatizo ni ujinga na ukondoo tulionao tu.

Ujinga na ukondoo tulionao ndo unaweza kumfanya Rais atoe amri ya wewe kuuwawa na firing squad na hakuna mtu atakayegoma kuitekeleza hiyo amri.
 
Hastahili pongezi yoyote watu wanaexercise haki yao kikatiba.

Mbona kuna lile kundi linaitwa chawa wa mama walifanya maandamano kumpongeza huyo ajuza wa kizimkazi na hawakuzuiwa?
 
Inavyoonekana yale maandamano ya CHADEMA yaliyopangwa kufanyika keshokutwa, yatafanyika.

Sasa nimeanza kuona eti pongezi anapewa Rais Samia...
Picha yenye hijab iliotulia inaonekana kila afisi ya umma, hii inawakera baadhi ya watu- alisikika mmoja wa member maarufu Jf
 
Inavyoonekana yale maandamano ya CHADEMA yaliyopangwa kufanyika keshokutwa, yatafanyika.

Sasa nimeanza kuona eti pongezi anapewa Rais Samia!

‘Whims’ za Samia ndo zimekuwa haki za kikatiba au?

Hakuna haja yoyote ya kumpongeza mtu kuhusu kitu kilichopo kwenye katiba ya Tanzania.

Haki zilizomo kwenye katiba ni haki za Watanzania wote.

Baadhi ya Watanzania wakitaka kuzitumia haki hizo, madhali ni kwa amani, hapaswi kuletewa figisu.

Hivi kweli unaweza kumpongeza jambazi kwa kutokukupora mali yako?

CCM wanakiuka katiba kila mara. Ikitokea kwenye jambo hawajakiuka katiba, mnawapa pongezi za nini?

Kuacha watu wafaidike na haki za kikatiba is the bare minimum.

Hivi ni kweli kuna Watanzania wanaona ni sawa kupongeza hata yale matakwa ya chini kabisa ya kikatiba yanapoacha kuporwa na CCM?

Tatizo ni ujinga au ukondoo? Au ni vyote kwa pamoja?

SMFH!
Screenshots_2024-01-23-06-28-59.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna kitu niliona kule X(twitter) niangalie hotuba za kina Kennedy na Nixon walivyokuwa wanahutubia wananchi miaka ya 1960's wakiwa wanasaka urais, alafu angalia kina Trump na Biden. Angalia Nyerere alivyokuwa akiongea na halaiki alafu angalia kina Nape et al.. hao wa zamani walikuwa wanaongea na raia wenye akili, hawa wa sasa wanajua wanaongea na vilaza.

Point yangu: kwamba hizi siasa za sasa tunazozi-experience ni zao la kizazi ambacho hakijielewi.. kwa hiyo kauli kama hizi hazijakulenga ww au mimi, kuna recipients wake watazisikia sana na wataunga mkono.
 
Hivi ni kweli kuna Watanzania wanaona ni sawa kupongeza hata yale matakwa ya chini kabisa ya kikatiba yanapoacha kuporwa na CCM?

Tatizo ni ujinga au ukondoo? Au ni vyote kwa pamoja?
Mbona enzi za Magufuli uliunga mkono ukiukwaji wa katiba na ukamwaga pongezi hata haki hizo ziliposiginwa?.

Hypocrisy....
 
Kuna watu wanaimba mapambio kumsifu rais kwa kuruhusu mikutano ya kisiasa, utamsifuje mtu kutekeleza kile kilichomo kwenye katiba halafu knamwomba awape katiba mpya. Huu ni uzuzu uliopitiliza.
 
Toka lini mpumbavu akawa na ufaham wa kung'amua haki zake,mtu mpumbavu ni mpumbavu tu.Na kwa bahati mbaya kundi la wapumbavu ndo wengi kama kipindi cha Shujaa waliitwa Wanyonge na wakakubali watashindwa vipi kuona haki zao ni kama hisani.
 
Inabidi tu apongezwe kwani miaka ile ya mwendazake hakukuwa na ruhusa hiyo.
 
Inavyoonekana yale maandamano ya CHADEMA yaliyopangwa kufanyika keshokutwa, yatafanyika.

Sasa nimeanza kuona eti pongezi anapewa Rais Samia!

‘Whims’ za Samia ndo zimekuwa haki za kikatiba au?

Hakuna haja yoyote ya kumpongeza mtu kuhusu kitu kilichopo kwenye katiba ya Tanzania.

Haki zilizomo kwenye katiba ni haki za Watanzania wote.

Baadhi ya Watanzania wakitaka kuzitumia haki hizo, madhali ni kwa amani, hapaswi kuletewa figisu.

Hivi kweli unaweza kumpongeza jambazi kwa kutokukupora mali yako?

CCM wanakiuka katiba kila mara. Ikitokea kwenye jambo hawajakiuka katiba, mnawapa pongezi za nini?

Kuacha watu wafaidike na haki za kikatiba is the bare minimum.

Hivi ni kweli kuna Watanzania wanaona ni sawa kupongeza hata yale matakwa ya chini kabisa ya kikatiba yanapoacha kuporwa na CCM?

Tatizo ni ujinga au ukondoo? Au ni vyote kwa pamoja?

SMFH!
Looooo tangu Jiwe afariki naona mliokuwa wafuasi wake mmeamua kukihama ccm.

Hongereni sana maana hata huo ni ukombozi wa kifikra.
 
Kiukweli Rais wa Tanzania hayupo juu ya sheria.

Na licha ya katiba kuwa mbovu, bado madaraka ya Rais yana mipaka.

Tatizo ni ujinga na ukondoo tulionao tu.
Umetaja vitu muhimu 2 vinavyofanya Rais wetu waendelee kusigina Katiba na kutuswaga kama Kondoo

Tatizo kubwa ni Ubovu wa Katiba yetu iliyompa mamlaka makubwa Rais

Ndiyo maana Leo hii hata ungekuwa wewe ndiyo Rais wa Nchi ungefanya kama wao...

Imagine Jaji Mkuu unamteua wewe Rais

IGP unamteua wewe Rais

CDF, DG wa TISS hadi Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi...

Niambie hapo nani ataweza Kumfunga Paka kengele ili sisi Panya tusiliwe na huyo Paka...

Umetaja pia Ukondoo,

Naam, Ukondoo wetu wa Tanzania pia unatu-gharimu.

Sasahivi Kila fedha itakayoletwa Wilayani kwaajili ya shughuli za maendeleo wanasema fedha za Rais...

Ni as if ametoka mfukoni mwake, kumbe ni Kodi zetu
 
Back
Top Bottom