Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 129
Jamani hao wazeee walijua wanachokifanya lakini???maana ile ni kisiwa kilichomo ndani ya jamhuri halali kabisa ambayo yatambuliwa hata Un ....sasa walichokitaka wao mi nakiona kama ni kosa ingawa sio uhaini.....moja kwa moja
Kijana unachekesha sana na unanifanya nikuone ndio walewale!
Kumbuka madai ya hawa wazee ni ya msingi wao wanabaguliwa hawashirikishwi katika serikali ya mapinduzi zanzibar wala kwenye serikali ya muungano! Wao ni sehemu ya Muungano na sehemu ya zanzibar. Tangu Mapinduzi ya Zanzibar hakuna Rais alyetoka Pemba sasa wewe hizo SKILLS zako unashindwa kujua kuwa hawa wazee wanamadai ya msingi? Kudai haki ni kosa? Kumbuka mkate tu hutafutwa kwahiyo haki haiji yenyewe inatafutwa ikiwezekana hata kwa ncha ya upanga!
SKILLS wewe na Prof Issa Shivji nani ni mtaalamu wa mambo ya sheria? Sasa mbona Prof Shivji amenukuliwa kwenye gazeti la mwananchi jana kuwa wale wazee wa watu hawana hatia yoyote na madai yao ni ya msingi?
SKILLS wewe unasema wamekosa! Prof Shivji anasema hawana kosa! Jaribu jingine usitulishe pumba mzee SKILLZ