GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
- Thread starter
- #21
Mtoa mada usiyumbishwe... Simamia msimamo wako... Hizi tabia zina kera kweli... Mimi siku hizi nikitumiwa picha kabla aijafunguka naichungulia kabisa ili nifute kabla... Kuna vitu vya kutisha mijitu ina rusha tu.
Kuna siku reporter wa redio flan ya huko DSM alimkuta dereva bajaji kagongwa na daladala... Yeye badala ya kuangalia namna ya kumsaidia yule mtu eti akapiga simu redioni... Huko nako wanaanza kumuhoji ajali ilivyo tokea?!!! Sasa kwa namna mkongoto si bora tu?
Akhsante kwa kunipa kibali Mkuu na kiukweli nawapa mno " kipondo " na watanyooka tu. Ni matumaini yangu kuwa Police Tanzania wanaupitia na kuufuatilia kwa umakini huu uzi ili kama wakipokea tu Kesi yoyote ihusuyo ( akina siye ) tunaopiga " waphotoaji " hovyo wakati wa ajali au mikasa ya kuhuzunisha badala ya wao kuokoa watatuunga mkono. Mkuu hivi ninavyoandika tu nimesikia kuna " mzinga " sasa hivi umetokea mtaa wa nyuma hivyo naomba ruhusa yako niende kwanza nikavizie nani nitamfuma anapiga picha ili nifanye yangu japo siku hizi nimekuwa mbunifu zaidi ambapo kabla ya kutoa " kipigo " kwanza huangalia sura ya nitakae kumpiga, mwonekano wake na ukomavu wake wa kimuonekano ili usije ukajifanya kimbelembele kumpiga ukajikuta baadae Ndugu zako wanapigiwa simu na Watu wa Mochwari kwenda " kuhakiki " mwili wako kutokana na kwamba umeharibiwa vibaya na kipigo.