Poleni sana Wabongo ambao ni homeless huko Marekani kwa sababu baridi huko kwa sasa sio ya mchezo.

Mtambachuo

JF-Expert Member
May 6, 2023
1,903
3,555
Ni vizuri kuwa diaspora ila kama huna kazi inayoeleweka huko au umeenda kinyemela na kupelekea kuishi kwa kubahatisha kiasi cha Cha kukosa makazi (homeless) hiyo ni hatari sana.

Katika kipindi hiki cha hali mbaya ya hewa huko hasa baridi kali kiasi kwamba baadhi ya majimbo yametangaza hali ya hatari kama huna sehemu salama ya kujisitiri ni hatari kwa afya na uhai.

Juzi nimesoma kwenye habari miili ya wanaume wawili homeless huko Houston jimbo la Texss imeokotwa stand tayari wamepoteza uhai.

So ni bora kama huna uhakika na uendako fanya mapambano ya maisha hapa hapa nchini au nchi nyingine ambazo una uhakika wa kupata huduma za msingi za kibinadamu.
 
Natural calamities unazifahamu Africa ndo inaongoza calamities kama njaa, mafuriko, ukame, miripuko ya magonjwa nk.
Mkuu lini ulisikia kuna tetemeko la ardhi Afrika? au Tsunami au winter storm kama Marekani?
Kuhusiana na njaa na milipuko ya magonjwa hizo siyo natural calamities ni matatizo yanayosababishwa na binadamu na yanaweza kuepukika.
 
Kweli kabisa mkuu umeleza vizuri naona haelewi vizuri maana ya Natural Calamities .
 
Back
Top Bottom