Pole zangu kwa RC Makonda

Swali kwako mleta mada. Akishagundua nusu nzima ya wakazi wa Dar es Salaam hawana kazi maalum atawafanyaje? Maana kazi nyingi za watu hazina mikataba au nyaraka unazoweza kuwaonesha hao wakaguzi. Kwa maana kazi nyingi si rasmi. Hili zoezi ni gumu na mimi naona si rahisi kufanikiwa. Akitaka takwimu aende Ofisi ya Takwimu ina makadirio ya kila kitu kinachoweza kumsaidia kupanga mikakati ya maendeleo.
Mbona hili la kutafuta wasio na kazi jijini Dar ni rahisi sana. Atoe tangazo la kuwaita watu wote wasio na kazi aone mafuriko.
 
hivi makonda kasema anatafta wahamiaji halamu au wahalifu?? mtu anaweza akawa mwajiriwa lakini akawa mwizi vle vle!! aliye sema asiye nakazi ndio mwizi ni nani???
Majambazi na wahalifu wote makini wana cover business, si rahisi kuwatambuwa kwa sensa, hii ndio shida ya kuchaguwa mkulima kuongoza Jiji la wafanyabiashara.

Dunia ya leo wapo watu wanaendesha maisha yao mtandaoni na wanamaliza biashara zao mtandaoni sasa ukinihoji nafanya kazi wapi nikikujibu hewani sijui utaona nimekudharau? Mambo mengine ni ya kipuuzi na kuamsha hasira za watu tu.

Kwanza ukimuuliza yeye Makonda aliwahi kuajiliwa wapi sidhani kama anaweza kukujibu.
 
Mkuu huku uswazi kuishi 30 kwenye nyumba moja mbona ni kitu cha kawaida tu, kama wewe unaishi masaki kwenye bungalow wewe na mkeo na mtoto mmoja shukuru Mungu.
Yap umeongea reality,tumeingia tz ya matabaka matamko yanawalenga wanyonge tu.
 
Pole Ndugu yangu RC Makonda.
Naona wengi wamekwandama kukosoa Maagizo yako. Wengine wameenda mbali zaidi na Kuorodhesha maagizo yako Mengi na kuhoji Kwanini usitekeleze moja liishe ndo uende lingine kana kwamba mambo ya nchi yanaendeshwa kama gia ya gari ambazo huwezi kuweka gia zote Mbili kwa wakati mmoja. Ingekuwa nchini inaendeshwa Hivyo basi nafikiri hata bajeti ya nchi tungepanga sector moja mwaka huu nyingine zisubiri lakini Ukweli ni kwamba mambo haya yote yanategemeana Kwahiyo lazimi uyakabiki yote kwa pamoja.

Kuhusu agizo la kukagua watu na shughuli zao. Wapo wanaosema eti unaingilia uhuru wa watu wako, unavunja haki za binadamu mbaya zaidi hata mayor wa jiji ambaye Kimsingi alitakiwa ashukuru kwamba unasaidia kuimarisha usalama wa watu wake lakini anapotosha na kukulaumu.

Binafsi nimekusikia vizuri tena hii sio mara ya kwanza. Tangu ukutane na Wenyeviti wa serikali za mitaa pale ukumbi wa mlm nyerere ulitoa agizo kwa Wenyeviti wetu kuhakikisha kwamba kila mtaa wakazi wanajulikana. Binafsi niliunga mkono kwasababu usalama wetu hapa mjini uko hatarini kutokana na ukazi holela. Yaani nyumba moja wanakaa watu 30 hata hawajulikani wametoka wapi na kama kweli Wenyeviti wa mitaa wakiwa imara wakasimamia hili nina hakika kwamba tutapunguza matishio ya usalama.

Sasa kuna hoja ya Kusema unataka kujua kazi zao ili iweje? Kwanini watu wafuatwe na kuhojiwa wanachofanya mjini hapa? Hivi kweli watu hatuoni kwamba tuna watu wengi hapa mjini wanashughulika na biashara haram na wanakaa mitaani kwetu, wa madanguro, madawa ya kulevya, mashoga, wahamiaji haram n.k. Watu kama hawa bila kuwa na mkakati madhubuti wa kuwabaini walipo itakuwa ngumu sana kuwakamata. Hivi kama kweli mimi nipo mjini na shughuli zangu halali naogopa nini kukaguliwa. Njooni hata usiku wa manane hata bila taarifa kwa watu wema sio Tatizo. Ila kwa waficha maovu ndio Tatizo na hata wanao tetea nina wasiwas kwamba wanahusika na biashara haram.

Yaani siku hizi umezuka mtindo wa kujificha kwenye kichaka cha haki za binadamu. Ukikamata mashoga haki za binadamu, Ukikamata mafisadi haki za binadamu, Ukikamata wauza unga haki za binadamu, mtu akivunja sheria za nchi akikamatwa basi kelele za watetezi huja na sauti za haki za binadamu.

Najua jiji hili lina kero nyingi na nikipima maagizo yako yote naona kabisa Dhamira njema na ya dhati kutaka kuondoa changamoto zilizopo suala la kufanikiwa au kutofanikiwa hilo ni lingine. Endelea kukemea, Endelea kuagiza, Endelea kubuni mbinu mbali mbali, Endelea kuja na mawazo mapya Mengine yatafanikiwa asilimia Mia, Mengine yatafanikiwa kidogo, Mengine itashindikana don't worry songa. Wengine watakupinga na wengine wataunga mkono.

Kusema Ukweli mimi naona unajitahidi sana na naweza kusema kwa muda mfupi huu wa Uongozi wako umevunja record ya wengi waliowahi kuongoza Dar. Usafi wa jiji umeboreka, vurugu na uporaji umepungua in short Dar is becoming more safe.
Sasa nakupa pole kwa kubezwa na kukejeliwa kwa mambo ufanyayo tena unafanya kwa faida ya watu wako. Huna ubinafsi. Katika ujana huo una Mengi ungeweza kuyaangalia kwa ajili yako Binafsi but wewe kila siku uko busy na kazi za serikali. Lakini bado unabezwa na viongozi wenzio ambao ilitakiwa msaidiane kutekeleza haya unayopanga.

Usirudi nyuma katika hili hayo Mengine ya kuondoa ombaomba unaweza ukasamehe lakini hili la ukaguzi wa nyumba kwa nyumba usiliache tena Ikiwezekana jeshi muombe JPM akupe WANAJESHI ndio wafanye kazi hii. Dar hii imejaa viwanda vya wamejazana mtaani huku na wanajenga kuta ndefu sana. Ikifika usiku Utasikia kelele tu huwezi hata kujua nini linafanyika, mchana huwaoni ila usiku Alaf eti mtu anapinga ukaguzi usifanyike. Mimi nyumban kwangu ruksa kuja kukaguliwa muda wowote.

Tanzania ilikuwa salama zaidi enzi za mwalimu nyerere kwasababu ya utaratibu wa ulinzi ulikuwa unaanzia nyumba kumi. Ilikuwa hakuna mtu kuingia mahali bila report ya barozi. Unasema utakuwepo kwa muda gani na utakuwa unafanya nini. Kama haitoshi Ukifika Ndugu yako asipotoa taarifa shughuli anayo. Na hii haikusemwa kama ni kuvunja uhuru wa kikatiba maana katiba yetu inatoa uhuru wa raia kuishi mahala popote bila kuvunja sheria. Lakini sasa tumekuwa na nchi holela na ndio maana jukumu la ulinzi limekuwa gumu.

Lele mama haiwez kutusaidia kuvuka hasa ukizingatia kwamba sisi wengi hatuna ustaarabu wa kufuata sheria
kha hivi akishakagua and then what next.kuna kero nyingi sana zaidi ya kujua maisha ya watu wa mjini wanafanya nini kila siku watu wanakuja na kuondoka hata kama utamkagua mtu leo kesho akija mwingine ndo kwamba zoezi litakua kila siku maana sina ndugu mmoja wa village na kama wanakuja kwa season je?kwa hapo sijaona mantiki kabisa wao waimarishe ulinzi kwa njia nyingine tu maana mtu anaeza akakwambia mimi nalima huko chato na naishi mjini wakati sio then itakuaje.afikirie challenge ya hili zoezi zaidi kuliko kukurupuka .No research no rigt to speak.so ajipange na wakati anajipanga atekeleze kero muhimu.Wale aliowaita wasiokua na kazi aliwapa nini au aliwasaidiaje?
 
Pole Ndugu yangu RC Makonda.
Naona wengi wamekwandama kukosoa Maagizo yako. Wengine wameenda mbali zaidi na Kuorodhesha maagizo yako Mengi na kuhoji Kwanini usitekeleze moja liishe ndo uende lingine kana kwamba mambo ya nchi yanaendeshwa kama gia ya gari ambazo huwezi kuweka gia zote Mbili kwa wakati mmoja. Ingekuwa nchini inaendeshwa Hivyo basi nafikiri hata bajeti ya nchi tungepanga sector moja mwaka huu nyingine zisubiri lakini Ukweli ni kwamba mambo haya yote yanategemeana Kwahiyo lazimi uyakabiki yote kwa pamoja.

Kuhusu agizo la kukagua watu na shughuli zao. Wapo wanaosema eti unaingilia uhuru wa watu wako, unavunja haki za binadamu mbaya zaidi hata mayor wa jiji ambaye Kimsingi alitakiwa ashukuru kwamba unasaidia kuimarisha usalama wa watu wake lakini anapotosha na kukulaumu.

Binafsi nimekusikia vizuri tena hii sio mara ya kwanza. Tangu ukutane na Wenyeviti wa serikali za mitaa pale ukumbi wa mlm nyerere ulitoa agizo kwa Wenyeviti wetu kuhakikisha kwamba kila mtaa wakazi wanajulikana. Binafsi niliunga mkono kwasababu usalama wetu hapa mjini uko hatarini kutokana na ukazi holela. Yaani nyumba moja wanakaa watu 30 hata hawajulikani wametoka wapi na kama kweli Wenyeviti wa mitaa wakiwa imara wakasimamia hili nina hakika kwamba tutapunguza matishio ya usalama.

Sasa kuna hoja ya Kusema unataka kujua kazi zao ili iweje? Kwanini watu wafuatwe na kuhojiwa wanachofanya mjini hapa? Hivi kweli watu hatuoni kwamba tuna watu wengi hapa mjini wanashughulika na biashara haram na wanakaa mitaani kwetu, wa madanguro, madawa ya kulevya, mashoga, wahamiaji haram n.k. Watu kama hawa bila kuwa na mkakati madhubuti wa kuwabaini walipo itakuwa ngumu sana kuwakamata. Hivi kama kweli mimi nipo mjini na shughuli zangu halali naogopa nini kukaguliwa. Njooni hata usiku wa manane hata bila taarifa kwa watu wema sio Tatizo. Ila kwa waficha maovu ndio Tatizo na hata wanao tetea nina wasiwas kwamba wanahusika na biashara haram.

Yaani siku hizi umezuka mtindo wa kujificha kwenye kichaka cha haki za binadamu. Ukikamata mashoga haki za binadamu, Ukikamata mafisadi haki za binadamu, Ukikamata wauza unga haki za binadamu, mtu akivunja sheria za nchi akikamatwa basi kelele za watetezi huja na sauti za haki za binadamu.

Najua jiji hili lina kero nyingi na nikipima maagizo yako yote naona kabisa Dhamira njema na ya dhati kutaka kuondoa changamoto zilizopo suala la kufanikiwa au kutofanikiwa hilo ni lingine. Endelea kukemea, Endelea kuagiza, Endelea kubuni mbinu mbali mbali, Endelea kuja na mawazo mapya Mengine yatafanikiwa asilimia Mia, Mengine yatafanikiwa kidogo, Mengine itashindikana don't worry songa. Wengine watakupinga na wengine wataunga mkono.

Kusema Ukweli mimi naona unajitahidi sana na naweza kusema kwa muda mfupi huu wa Uongozi wako umevunja record ya wengi waliowahi kuongoza Dar. Usafi wa jiji umeboreka, vurugu na uporaji umepungua in short Dar is becoming more safe.
Sasa nakupa pole kwa kubezwa na kukejeliwa kwa mambo ufanyayo tena unafanya kwa faida ya watu wako. Huna ubinafsi. Katika ujana huo una Mengi ungeweza kuyaangalia kwa ajili yako Binafsi but wewe kila siku uko busy na kazi za serikali. Lakini bado unabezwa na viongozi wenzio ambao ilitakiwa msaidiane kutekeleza haya unayopanga.

Usirudi nyuma katika hili hayo Mengine ya kuondoa ombaomba unaweza ukasamehe lakini hili la ukaguzi wa nyumba kwa nyumba usiliache tena Ikiwezekana jeshi muombe JPM akupe WANAJESHI ndio wafanye kazi hii. Dar hii imejaa viwanda vya majumbani, Wachina wamejazana mtaani huku na wanajenga kuta ndefu sana. Ikifika usiku Utasikia kelele tu huwezi hata kujua nini linafanyika, mchana huwaoni ila usiku Alaf eti mtu anapinga ukaguzi usifanyike. Mimi nyumban kwangu ruksa kuja kukaguliwa muda wowote.

Tanzania ilikuwa salama zaidi enzi za mwalimu nyerere kwasababu ya utaratibu wa ulinzi ulikuwa unaanzia nyumba kumi. Ilikuwa hakuna mtu kuingia mahali bila report ya barozi. Unasema utakuwepo kwa muda gani na utakuwa unafanya nini. Kama haitoshi Ukifika Ndugu yako asipotoa taarifa shughuli anayo. Na hii haikusemwa kama ni kuvunja uhuru wa kikatiba maana katiba yetu inatoa uhuru wa raia kuishi mahala popote bila kuvunja sheria. Lakini sasa tumekuwa na nchi holela na ndio maana jukumu la ulinzi limekuwa gumu.

Lele mama haiwez kutusaidia kuvuka hasa ukizingatia kwamba sisi wengi hatuna ustaarabu wa kufuata sheria
USHAURI WA BURE KWA RC. PAUL MAKONDA!

Na. Mtatiro J.

Mkuu wetu wa mkoa na kijana mwenzetu, huna haja ya kuzungusha Polisi mitaani kukamata Raia wasio na hatia kwa kutumia mamlaka yoyote unayodhani unayo. Common Sense peke yake haikubaliani na jambo hilo;

1. Zoezi lenyewe haliwezekani na halitekelezeki hata kidogo. Halina BASIS za kisheria wala KIMAADILI, kwa hiyo ni NULL and VOID tangu tu ulipolitangaza.

2. Litazua vurugu, balaa na machafuko mitaani na litashindwa kwa asilimia 100 na ni aibu sana kwa kijana mwenzetu ku attempt vitu visivyowezekana.

3. Nakupa ushauri wa bure ndugu yangu, kwamba kama anataka kuwabaini na kuwakamata wakazi wa DSM wasiofanya kazi na wasio na ajira, hebu pitia daftari la Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2012. Takwimu za sensa zimeeleza vizuri sana, mtaa gani una vijana wangapi na hali zao zikoje. Usiwahangaishe polisi.

4. Kisha, toa maelekezo kuwa vijana hao na wananchi wasio na shughuli za kufanya waje wenyewe ofisini kwako, taja tarehe na muda. Mimi kwangu ninao kama 7 hivi, ntawaleta mimi mwenyewe kisha ntakuachia uchukue hatua stahiki kwa mujibu wa sheria kwa makosa yao ya kutokuwa na shughuli za kufanya.

5. Wewe ni kijana mwenzetu na kila unapotoa matamko dhaifu na yasiyo na tija kwa taifa unafanya wananchi wote waamini kuwa VIJANA wa taifa hili hawajakomaa na hawako tayari kuongoza nchi. Ikiwa viongozi vijana tunashindwa kupigania ajenda muhimu za kijamii pindi tunapokabidhiwa mamlaka ya uongozi wa nchi, tunaiandaa jamii itupe hukumu gani mbeleni?

6. Comrade Paul, wewe ni kiongozi mwenye utashi na kwa tunaokufahamu tunajua unayo talanta bora ya uongozi, lakini umeiweka kando. Hivi sasa unaendeshwa na ukuu na kutikisa watu bila sababu. Yuko wapi yule Makonda ambaye aliendesha kampeni ya usafi jijini DSM? Iliishia wapi kampeni ile? Mbona wananchi walikuunga mkono brother? Usafi uliona hautoshi sasa unataka kuwasaka wasio na kazi? Ili iweje? Na unadhani nani atakubali kusakwa na kukamatwa kwa sababu hana kazi, kazi ambayo hajawekewa mazingira ya kuipata kwa kuajiriwa au kujiajiri?

7. Ndugu Paul, unakumbuka ulitangaza kuendesha msako wa ombaomba? Unakumbuka tulivyokuunga mkono? Jamii nzima ya DSM. Ombaomba ni kero kubwa sana na hawapaswi kuchekewa, ukifanya zoezi la kuwarudisha vijijini kila mtu atakuunga mkono. Unakumbuka zoezi la kukamata SHISHA na watumiaji wake? Unakumbuka tulikupongeza na tulikuusia kuwa ungelianza na wasambazaji wa madawa ya kulevya kwanza? Maana COCAINE na HEROIN zinauzwa kama njugu hapa jijini tena huenda unawajua wauzaji hadi majumbani mwao, tulikushauri tu.

8. Kaka Paul, kwa mtizamo wangu, anza kujifunza kujenga DAR yenye utulivu, yenye mipango inayotekelezeka na yenye maelewano. Kamwe usijifunze kuanzisha mazoezi yasiyotekelezeka au ambayo yakitekelezeka yanaweza kuleta balaa kubwa. Unaikumbuka ARAB UPRISING? Ilianzaje? Kijana hana ajira, anajiuzia mbogamboga askari wakaenda kulivunja na kulichoma banda lake na mboga zake, kijana yule akaamua kujitia PETROLI, akaungua hadharani, video zake zikasambazwa, jamii ikashikwa na ghadhabu, maandamano yakaanza mataifa ya Uarabuni, watawala wakang'olewa. Chanzo cha maafa ya Uarabuni ni watawala kushindwa kuweka mazingira rafiki ya ajira kwa jamii zao na kisha watawala hao hao wakaanza kuwanyanyasa watu wasio na ajira.

9. Kiongozi wangu Makonda, UKOSEFU WA AJIRA au SHUGHULI ZA KUFANYA ni bomu lililotulia mahali na aliyelilea anafahamika, ni chama chako, CCM. Chama ambacho kimekupa ukuu wa mkoa ndicho kimeongoza taifa hili kwa miaka 50 sasa, kimeshindwa kuitumia nguvu kazi ya taifa na leo tuongeapo, mamilioni ya vijana hawajui nini wafanye. Hata ajira za kuuza pipi zinafanywa na WACHINA. Hawa vijana unaotaka kuwasaka majumbani watafanya nini? Kwa nini unataka kulitegua BOMU lililojituliza huku hauna utaalamu huo? Likilipuka kwa vyovyote vile hautabaki salama! Utapata madhara. Bomu hili linahitaji PATIENCE na CALMNESS, linahitaji wataalamu waliobobea waje na vifaa vyao. Huwezi tu kubeba ndugu zetu POLISI na kuwabambikizia oparesheni isiyo na nguvu ya kisheria na inayoweza kuleta vurugu na matatizo mitaani.

10. Mdogo wangu Paul Makonda, wanasiasa wengi huwa hawapebdi kushauriwa hadharani, hukasirika na kuwaona washauri wa namna hiyo kama watu wanaowachukia. Mimi ni mwanasiasa kijana kama wewe na huwenda nimewahi kushika majukumu makubwa sana. Huwa nafurahi sana kila nionapo watu wananishauri hadharani, hasa kwa lugha ya heshima kama niliyotumia hapa. Mara kadhaa umewahi kuwa na hofu nami hasa nilipowahi kukukosoa sana kwa hatua ya kumkamata mbunge Kubenea na kumuweka ndani, niliwahi kukukosia pia ulipowaweka ndani watumishi wa halmashauri kwa kuchelewa kazini. Sijawahi kufanta hivyo kwa nia mbaya ,mara zote dhamira yangu inanisuta napoona kijana mwenzangu anaharibu kwenye uongozi. Huwa natoa ushauri huo kwa kijana yeyote yule bila kujali anatoka chama gani. Ni kama mimi mwenyewe navyopenda kupokea ushauri kutoka kokote, ilimradi utumie lugha inayokubalika. Mimi ni kati ya watu ambao wataendelea kukushauri na kukukosoa, bila kujali kuwa unaweza kuchukia na kukasirika kama wanavyoogopa wanasiasa wazee, wanapokosolewa hadharani. Sitajali, ntaendelea na kazi. Kumbuka, anayekukosoa ANAKUPENDA NA KUKUTAKIA MEMA, anayekusifia wakati unakwenda kutegua mabomu bila wataalamu, ANAKUTAKIA MABAYA.

Julius Sunday Mtatiro,
+255787536759 (Whatsup and Text only) juliusmtatiro@yahoo.com
Dar Es Salaam.
 
Majambazi na wahalifu wote makini wana cover business, si rahisi kuwatambuwa kwa sensa, hii ndio shida ya kuchaguwa mkulima kuongoza Jiji la wafanyabiashara.

Dunia ya leo wapo watu wanaendesha maisha yao mtandaoni na wanamaliza biashara zao mtandaoni sasa ukinihoji nafanya kazi wapi nikikujibu hewani sijui utaona nimekudharau? Mambo mengine ni ya kipuuzi na kuamsha hasira za watu tu.

Kwanza ukimuuliza yeye Makonda aliwahi kuajiliwa wapi sidhani kama anaweza kukujibu.
Mwacheni aendelee kutuongezea machungu ili mwaka 2020 tusafishe kabisa dar
 
Swali kwako mleta mada. Akishagundua nusu nzima ya wakazi wa Dar es Salaam hawana kazi maalum atawafanyaje? Maana kazi nyingi za watu hazina mikataba au nyaraka unazoweza kuwaonesha hao wakaguzi. Kwa maana kazi nyingi si rasmi. Hili zoezi ni gumu na mimi naona si rahisi kufanikiwa. Akitaka takwimu aende Ofisi ya Takwimu ina makadirio ya kila kitu kinachoweza kumsaidia kupanga mikakati ya maendeleo.
Kesho utaelewa ufafanuzi zaidi
 
Basi inatakiwa afanye kweli kuwaumbua watu laa sivyo itakua maneno ya kimakonda
 
Pole Ndugu yangu RC Makonda.
Naona wengi wamekwandama kukosoa Maagizo yako. Wengine wameenda mbali zaidi na Kuorodhesha maagizo yako Mengi na kuhoji Kwanini usitekeleze moja liishe ndo uende lingine kana kwamba mambo ya nchi yanaendeshwa kama gia ya gari ambazo huwezi kuweka gia zote Mbili kwa wakati mmoja. Ingekuwa nchini inaendeshwa Hivyo basi nafikiri hata bajeti ya nchi tungepanga sector moja mwaka huu nyingine zisubiri lakini Ukweli ni kwamba mambo haya yote yanategemeana Kwahiyo lazimi uyakabiki yote kwa pamoja.

Kuhusu agizo la kukagua watu na shughuli zao. Wapo wanaosema eti unaingilia uhuru wa watu wako, unavunja haki za binadamu mbaya zaidi hata mayor wa jiji ambaye Kimsingi alitakiwa ashukuru kwamba unasaidia kuimarisha usalama wa watu wake lakini anapotosha na kukulaumu.

Binafsi nimekusikia vizuri tena hii sio mara ya kwanza. Tangu ukutane na Wenyeviti wa serikali za mitaa pale ukumbi wa mlm nyerere ulitoa agizo kwa Wenyeviti wetu kuhakikisha kwamba kila mtaa wakazi wanajulikana. Binafsi niliunga mkono kwasababu usalama wetu hapa mjini uko hatarini kutokana na ukazi holela. Yaani nyumba moja wanakaa watu 30 hata hawajulikani wametoka wapi na kama kweli Wenyeviti wa mitaa wakiwa imara wakasimamia hili nina hakika kwamba tutapunguza matishio ya usalama.

Sasa kuna hoja ya Kusema unataka kujua kazi zao ili iweje? Kwanini watu wafuatwe na kuhojiwa wanachofanya mjini hapa? Hivi kweli watu hatuoni kwamba tuna watu wengi hapa mjini wanashughulika na biashara haram na wanakaa mitaani kwetu, wa madanguro, madawa ya kulevya, mashoga, wahamiaji haram n.k. Watu kama hawa bila kuwa na mkakati madhubuti wa kuwabaini walipo itakuwa ngumu sana kuwakamata. Hivi kama kweli mimi nipo mjini na shughuli zangu halali naogopa nini kukaguliwa. Njooni hata usiku wa manane hata bila taarifa kwa watu wema sio Tatizo. Ila kwa waficha maovu ndio Tatizo na hata wanao tetea nina wasiwas kwamba wanahusika na biashara haram.

Yaani siku hizi umezuka mtindo wa kujificha kwenye kichaka cha haki za binadamu. Ukikamata mashoga haki za binadamu, Ukikamata mafisadi haki za binadamu, Ukikamata wauza unga haki za binadamu, mtu akivunja sheria za nchi akikamatwa basi kelele za watetezi huja na sauti za haki za binadamu.

Najua jiji hili lina kero nyingi na nikipima maagizo yako yote naona kabisa Dhamira njema na ya dhati kutaka kuondoa changamoto zilizopo suala la kufanikiwa au kutofanikiwa hilo ni lingine. Endelea kukemea, Endelea kuagiza, Endelea kubuni mbinu mbali mbali, Endelea kuja na mawazo mapya Mengine yatafanikiwa asilimia Mia, Mengine yatafanikiwa kidogo, Mengine itashindikana don't worry songa. Wengine watakupinga na wengine wataunga mkono.

Kusema Ukweli mimi naona unajitahidi sana na naweza kusema kwa muda mfupi huu wa Uongozi wako umevunja record ya wengi waliowahi kuongoza Dar. Usafi wa jiji umeboreka, vurugu na uporaji umepungua in short Dar is becoming more safe.
Sasa nakupa pole kwa kubezwa na kukejeliwa kwa mambo ufanyayo tena unafanya kwa faida ya watu wako. Huna ubinafsi. Katika ujana huo una Mengi ungeweza kuyaangalia kwa ajili yako Binafsi but wewe kila siku uko busy na kazi za serikali. Lakini bado unabezwa na viongozi wenzio ambao ilitakiwa msaidiane kutekeleza haya unayopanga.

Usirudi nyuma katika hili hayo Mengine ya kuondoa ombaomba unaweza ukasamehe lakini hili la ukaguzi wa nyumba kwa nyumba usiliache tena Ikiwezekana jeshi muombe JPM akupe WANAJESHI ndio wafanye kazi hii. Dar hii imejaa viwanda vya majumbani, Wachina wamejazana mtaani huku na wanajenga kuta ndefu sana. Ikifika usiku Utasikia kelele tu huwezi hata kujua nini linafanyika, mchana huwaoni ila usiku Alaf eti mtu anapinga ukaguzi usifanyike. Mimi nyumban kwangu ruksa kuja kukaguliwa muda wowote.

Tanzania ilikuwa salama zaidi enzi za mwalimu nyerere kwasababu ya utaratibu wa ulinzi ulikuwa unaanzia nyumba kumi. Ilikuwa hakuna mtu kuingia mahali bila report ya barozi. Unasema utakuwepo kwa muda gani na utakuwa unafanya nini. Kama haitoshi Ukifika Ndugu yako asipotoa taarifa shughuli anayo. Na hii haikusemwa kama ni kuvunja uhuru wa kikatiba maana katiba yetu inatoa uhuru wa raia kuishi mahala popote bila kuvunja sheria. Lakini sasa tumekuwa na nchi holela na ndio maana jukumu la ulinzi limekuwa gumu.

Lele mama haiwez kutusaidia kuvuka hasa ukizingatia kwamba sisi wengi hatuna ustaarabu wa kufuata sheria
Sasa huku ndo kujipendekeza au.. Andiko lefu pumba tupu. Tambua malalamiko ya wetu wengi ha ni constructive kama Makonda atayachukulia postively. Wengi wa wanaomtetea ni wanafiki tu
 
Nimesoma wee,niIpofika hapo unaposema "Dar is becoming more safe" nikaishia hapo hapo.
Hata kama mmetumwa kuja kutetea vitu vingine muwe realistic kidogo jamani..aargh!
 
Mtoa mada umeongea kweli tupu na una maono ya mbali zaidi. Hii nchi imejaa wahalifu na wahamiaji haram sasa kwa mpango huu wa Makonda lazma watoke mapovu. Ukifika Tabata Segerea wachina wamejaza Viwanda majumban wanatengeneza Mabati, misumari, yeboyebo viatu na Gypsum Board yaaan makelele usiku kucha. Makonda harakisha huo mpango wako usafishe jiji. Viwanda vya kukata magari ya wizi, kuhifadhi nyara za serikali na kuna wengine ni kupaki kwenye makontena magogo ya Mininga na Mipingo. Nina hasira na hiii mijiz inayopinga agizo la RC...... Kenge kabisa hao
Ingependeza hao unaowajua hiyo mita, ukapeleka information kwa mheshimiwa aanze nao. Kumbe tunawatambuwa halafu tunashindwa kusema! Huoni kama utakuwa umempunguzia kazi kuwabaini hawa wahalifu?
 
Back
Top Bottom