Pole zangu kwa RC Makonda

Malaika Mkuu

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
902
909
Pole Ndugu yangu RC Makonda.
Naona wengi wamekwandama kukosoa Maagizo yako. Wengine wameenda mbali zaidi na Kuorodhesha maagizo yako Mengi na kuhoji Kwanini usitekeleze moja liishe ndo uende lingine kana kwamba mambo ya nchi yanaendeshwa kama gia ya gari ambazo huwezi kuweka gia zote Mbili kwa wakati mmoja. Ingekuwa nchini inaendeshwa Hivyo basi nafikiri hata bajeti ya nchi tungepanga sector moja mwaka huu nyingine zisubiri lakini Ukweli ni kwamba mambo haya yote yanategemeana Kwahiyo lazimi uyakabiki yote kwa pamoja.

Kuhusu agizo la kukagua watu na shughuli zao. Wapo wanaosema eti unaingilia uhuru wa watu wako, unavunja haki za binadamu mbaya zaidi hata mayor wa jiji ambaye Kimsingi alitakiwa ashukuru kwamba unasaidia kuimarisha usalama wa watu wake lakini anapotosha na kukulaumu.

Binafsi nimekusikia vizuri tena hii sio mara ya kwanza. Tangu ukutane na Wenyeviti wa serikali za mitaa pale ukumbi wa mlm nyerere ulitoa agizo kwa Wenyeviti wetu kuhakikisha kwamba kila mtaa wakazi wanajulikana. Binafsi niliunga mkono kwasababu usalama wetu hapa mjini uko hatarini kutokana na ukazi holela. Yaani nyumba moja wanakaa watu 30 hata hawajulikani wametoka wapi na kama kweli Wenyeviti wa mitaa wakiwa imara wakasimamia hili nina hakika kwamba tutapunguza matishio ya usalama.

Sasa kuna hoja ya Kusema unataka kujua kazi zao ili iweje? Kwanini watu wafuatwe na kuhojiwa wanachofanya mjini hapa? Hivi kweli watu hatuoni kwamba tuna watu wengi hapa mjini wanashughulika na biashara haram na wanakaa mitaani kwetu, wa madanguro, madawa ya kulevya, mashoga, wahamiaji haram n.k. Watu kama hawa bila kuwa na mkakati madhubuti wa kuwabaini walipo itakuwa ngumu sana kuwakamata. Hivi kama kweli mimi nipo mjini na shughuli zangu halali naogopa nini kukaguliwa. Njooni hata usiku wa manane hata bila taarifa kwa watu wema sio Tatizo. Ila kwa waficha maovu ndio Tatizo na hata wanao tetea nina wasiwas kwamba wanahusika na biashara haram.

Yaani siku hizi umezuka mtindo wa kujificha kwenye kichaka cha haki za binadamu. Ukikamata mashoga haki za binadamu, Ukikamata mafisadi haki za binadamu, Ukikamata wauza unga haki za binadamu, mtu akivunja sheria za nchi akikamatwa basi kelele za watetezi huja na sauti za haki za binadamu.

Najua jiji hili lina kero nyingi na nikipima maagizo yako yote naona kabisa Dhamira njema na ya dhati kutaka kuondoa changamoto zilizopo suala la kufanikiwa au kutofanikiwa hilo ni lingine. Endelea kukemea, Endelea kuagiza, Endelea kubuni mbinu mbali mbali, Endelea kuja na mawazo mapya Mengine yatafanikiwa asilimia Mia, Mengine yatafanikiwa kidogo, Mengine itashindikana don't worry songa. Wengine watakupinga na wengine wataunga mkono.

Kusema Ukweli mimi naona unajitahidi sana na naweza kusema kwa muda mfupi huu wa Uongozi wako umevunja record ya wengi waliowahi kuongoza Dar. Usafi wa jiji umeboreka, vurugu na uporaji umepungua in short Dar is becoming more safe.
Sasa nakupa pole kwa kubezwa na kukejeliwa kwa mambo ufanyayo tena unafanya kwa faida ya watu wako. Huna ubinafsi. Katika ujana huo una Mengi ungeweza kuyaangalia kwa ajili yako Binafsi but wewe kila siku uko busy na kazi za serikali. Lakini bado unabezwa na viongozi wenzio ambao ilitakiwa msaidiane kutekeleza haya unayopanga.

Usirudi nyuma katika hili hayo Mengine ya kuondoa ombaomba unaweza ukasamehe lakini hili la ukaguzi wa nyumba kwa nyumba usiliache tena Ikiwezekana jeshi muombe JPM akupe WANAJESHI ndio wafanye kazi hii. Dar hii imejaa viwanda vya majumbani, Wachina wamejazana mtaani huku na wanajenga kuta ndefu sana. Ikifika usiku Utasikia kelele tu huwezi hata kujua nini linafanyika, mchana huwaoni ila usiku Alaf eti mtu anapinga ukaguzi usifanyike. Mimi nyumban kwangu ruksa kuja kukaguliwa muda wowote.

Tanzania ilikuwa salama zaidi enzi za mwalimu nyerere kwasababu ya utaratibu wa ulinzi ulikuwa unaanzia nyumba kumi. Ilikuwa hakuna mtu kuingia mahali bila report ya barozi. Unasema utakuwepo kwa muda gani na utakuwa unafanya nini. Kama haitoshi Ukifika Ndugu yako asipotoa taarifa shughuli anayo. Na hii haikusemwa kama ni kuvunja uhuru wa kikatiba maana katiba yetu inatoa uhuru wa raia kuishi mahala popote bila kuvunja sheria. Lakini sasa tumekuwa na nchi holela na ndio maana jukumu la ulinzi limekuwa gumu.

Lele mama haiwez kutusaidia kuvuka hasa ukizingatia kwamba sisi wengi hatuna ustaarabu wa kufuata sheria
 
Swali kwako mleta mada. Akishagundua nusu nzima ya wakazi wa Dar es Salaam hawana kazi maalum atawafanyaje? Maana kazi nyingi za watu hazina mikataba au nyaraka unazoweza kuwaonesha hao wakaguzi. Kwa maana kazi nyingi si rasmi. Hili zoezi ni gumu na mimi naona si rahisi kufanikiwa. Akitaka takwimu aende Ofisi ya Takwimu ina makadirio ya kila kitu kinachoweza kumsaidia kupanga mikakati ya maendeleo.
 
Mtoa mada umeongea kweli tupu na una maono ya mbali zaidi. Hii nchi imejaa wahalifu na wahamiaji haram sasa kwa mpango huu wa Makonda lazma watoke mapovu. Ukifika Tabata Segerea wachina wamejaza Viwanda majumban wanatengeneza Mabati, misumari, yeboyebo viatu na Gypsum Board yaaan makelele usiku kucha. Makonda harakisha huo mpango wako usafishe jiji. Viwanda vya kukata magari ya wizi, kuhifadhi nyara za serikali na kuna wengine ni kupaki kwenye makontena magogo ya Mininga na Mipingo. Nina hasira na hiii mijiz inayopinga agizo la RC...... Kenge kabisa hao
 
80%+ ya watanzania awako kwenye formal sector na serikali wanajua hilo na awawenga mpango wa kupunguza hiyo idadi. Mkoa wa Dar es salaam una watu zaidi ya milioni 5 kati yao wote 10% ndio wako kwenye formal sector hii ni kutokana na sensa ya 2012. Sasa hapa makonda akichunguza atakuta zaidi ya watu milioni 4 awana ajira rasmi. Swali linakuja je atawasaidia vipi hao watu milioni 4 waingie kwenye formal sector?
 
Ninyi ndo mnampa kichwa wakati jamaa amna kitu. Leo anaweza kutuambia wameondoka omba omba wangapi? Wabwia shisha je? Dada poa? Mashoga? Upuuzi mtupu! Ila kwa sababu ni awamu ya amri, itaonekana anafanya kazi
 
Mmeamua kumuingiza mkenge Makonda.
 
makonda anafikiria kuongoza dar km mkuu wa mkoa ni sawa na kuongoza ndani ya ccm
 
wandanye mbumbu wenzio yaani pamoja akili yako ndogo ndio unakuja na uzi wa kipuuzi hivi? makonda hajasema anataka kujua wakazi wa kila nyumba ametangaza kukamata watu wasio na kazi malumu tena kwa msako!! sasa wwe sijui nikulinganishe na nn hvi tutajopendekeza mpaka lini?? unajrbu kubari nyekundu iwe nyeupe ww km c wale wanyama wengi serengeti national park, sijui tukuitaje
 
Hachelewi kuyakana yote hayo kesho kwenye redio gani sijui maana mimi hua nasikiliza Times Fm kwa hapa Tz ila hayo maredio ya mavyama hata siwezani nayo. Nadhani watakaomsikiliza watatuletea hayo makanusho humu kesho.
 
hivi makonda kasema anatafta wahamiaji halamu au wahalifu?? mtu anaweza akawa mwajiriwa lakini akawa mwizi vle vle!! aliye sema asiye nakazi ndio mwizi ni nani???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…