Pinda: gesi kutonufaisha watanzania hadi baada ya miaka kumi hadi ishirini

Kawatega....wakitegeka...wakakurupuka....wakasababisha machafuko.....atarudi....atafafanua....ataeleweka....hawataeleweka.....siasa bwana
 
Ni kweli gas haitatunufaisha chini ya uongozi wa CCM km ilivyo kwa madini mengine...Na kasema "Tusishangae gesi inauzwa na faida sifuri" Mh mie nadhani kwa mantiki hii ni bora tuungane wote na gas isichimbwe kabisaa kwani Faida itakayo patikana sio kwa ajiri ya waTanzania ila ni kulipa 10% zao na kuwalipa hao wezi wanaoitwa wawekezaji
 
Sasa haraka yote ya nini?

Kwa hiyo tusiwe na haraka kwa sababu serikali yetu ina pesa nyingi.

Watoto wetu wanasoma bila matatizo, hatuna shida ya barabara, Wafanyakazi Wanalipwa mishahara ya kutosha Na halmashauri zinapata budget yao bila matatizo, etc, etc
 
Nakubaliana na wewe hoja yangu ni uharaka wa kujenga bomba kwa miezi 18 na manufaa yaje baada ya miaka 20.....unless something is missing or misinformed!
 
Waziri Mkuu Mh. Pinda aka mtoto wa mkulima katika taarifa ya saa mbili kituo cha Star TV amewataka watanzania wasiwe na mategemeo kwamba wataanza kunufaika na gesi ya Mtwara katika muda mfupi ujao.

Mh. waziri Mkuu amefafanua kwamba watanzania wataanza kunufaika na gesi yao baada ya miaka kumi (10) hadi ishirini (20).

Amesema hii ni kutokana na maandalizi yanayopaswa kupitia kabla ya kuanza kupata faida kwa sababu uchimbaji wa gesi unahitaji uwekezaji Mkubwa.
Pia ametahadhalisha wananchi mshishangae gesi ikawa inauzwa ila haiwanufaishi watanzania!
!

Haitatunufaisha watanzania kwa uzembe wa serikali ya ccm maana wamekaa madarakani tangu uhuru hadi sasa na miundo mbinu, rasimali watu na elimu zote hakuna au ni legelege mno kama kampuni ya GB oil and GAS inyosema.... sasa ajabu iko wapi kama si kuendelea kuitia CCM kitanzini zaidi? CCM wamechoka na akili zao pia.. ya nini wanakuwa vinganganizi wa madaraka....

hata baba na mama wakizaa watoto baada wanawaacha watoto hao wajitegemee na kujiamulia mambo yao wenyewe.. kwa nini ccm isiwape nafasi wengine yaani iseme haitasimamsiha mgombea yeyote katika uchaguzi ujao ili kutoa nafasi kwa mawazo mbadara...
 
Ni kweli gas haitatunufaisha chini ya uongozi wa CCM km ilivyo kwa madini mengine...Na kasema "Tusishangae gesi inauzwa na faida sifuri" Mh mie nadhani kwa mantiki hii ni bora tuungane wote na gas isichimbwe kabisaa kwani Faida itakayo patikana sio kwa ajiri ya waTanzania ila ni kulipa 10% zao na kuwalipa hao wezi wanaoitwa wawekezaji

Mkuu hapo umenifungua macho
 
wanaofaidika baada ya miaka ishirini ni watanazania gani, wanao piga kura au wanaopigiwa kula.

eEH yeye kapewa vitabu vya kihasibu na wawekezaji ndivyo vinasema hivyo ili wasilipe kodi miaka kumi. Anyway my take is why TPDC isipewe japo 2% share iwe na sauti kwenye board za hao mabwenyenye.
 
Kama ndivyo PM alivyosema, basi kuna kitu hakiko sawa.. Watanzania ni akina nani? Watanzania ni pamoja na watu wa Mtwara, Lindi n.k Kwa haya makampuni ya gesi kuweka 'base' Mtwara badala ya Dar Es salaam tu inatosha ku 'stimulate' uchumi wa Mtwara . Kunufaika na gesi siyo lazima mpaka gesi iuzwe...hata huduma mbalimbali zinazoambatana na miradi hii kama hospitali,mashule, sehemu za michezo,masoko ya kisasa,huduma za usafiri, huduma za ulinzi n.k ni faida kwa wakazi hawa na nchi kwa ujumla..
 
Wenzangu naombeni tuchangie tueleweshane.
Au ndio watanzania tushaliwa na gesi yetu mafisadi wameshachakachua na kubeba chao kwenye mikataba![/QUOTE]
katika uelewa wangu pinda anamanisha kweli kwa sababu siku zote faida ya mtanzania ni mashimo na uharibifu wa mazingira,kwa hiyo baada ya miaka ishirini(20) sie wajanja tutakuwa tunafurahia faida(uharibifu wa mazingira) wakati wao wajinga(wawekezaji) watakuwa wanasherekea hasara(stock ya gesi),waulize kanda ya ziwa wanachokiona leo hii ndiyo faida yenyewe
 
PINDA amelidanganya bunge na rais kuwa sakata la gesi Mtwara limeisha. Ukweli ni kwamba wakati wa majumuisho aliongea yeye kama protocal inavyotaka hata mawaziri aliowaita kuja kupiga kampeni za mwaka 2015 hawakupata nafasi ya kuulizwa maswali ingawa wenyewe waliomba waulizwe maswali, wananchi wa Mtwara wanasema gesi haitoki mtwara wataruhusu umeme kusafirishwa kwa njia ya waya na nguzo kupitia songea kama mpango wa awali ulivyokuwa kujenga power plant ya kufua umeme wa megawatt 300 na kujenga grid yenye urefu wa kilomita 1,100 kupitia songea kabla ya serikali kukubali ushawishi mbaya wa TPDC wa kuisafirisha gesi kwa njia ya bomba kutoka Mtwara - Dar. Jenzi wa bomba unakadiliwa kugharimu trilion 2.2 mkopo kutoka Exim Benki ya China na ujenzi wa power plant ungegharimu dola za marekani milioni 684 sawa na shilingi trilioni 1.09 ( 1,094,400,000,000) KWA EXCHANGE RATE YA DOLA 1 shililingi 1600 pia mkopo kutoka benki ya Exim ya China. rejea taarifa ya ikulu 12 Octoba 2011.
 
Wenzangu naombeni tuchangie tueleweshane.
Au ndio watanzania tushaliwa na gesi yetu mafisadi wameshachakachua na kubeba chao kwenye mikataba!
katika uelewa wangu pinda anamanisha kweli kwa sababu siku zote faida ya mtanzania ni mashimo na uharibifu wa mazingira,kwa hiyo baada ya miaka ishirini(20) sie wajanja tutakuwa tunafurahia faida(uharibifu wa mazingira) wakati wao wajinga(wawekezaji) watakuwa wanasherekea hasara(stock ya gesi),waulize kanda ya ziwa wanachokiona leo hii ndiyo faida yenyewe[/QUOTE]

Kwa kweli watanzania tuna safari ndefu
 
Duh!

Mungu wetu wa mbinguni eeeeeeee!!!!!!!! Hii ni sinema nyingine ya CCM. WaTanganyika ndiyo tushaingizwa choo cha kike jamani!!!!! Yaani juzi wanantuambia kwamba Gesi bomba la gesi litajengwa ndani ya miezi 18, leo hii wanakuja na muvi nyingine!!!!!???

Kweli wameshatuona waTanganyika tu mazezeta kabisa. Kwamba hata tufanyweje na hicho kikundi kidogo cha mafisadi hatuwezi kuwafanya lolote. Kwa hiyo hata hizo ahadi walizo ahidiwa wana Mtwara zilikuwa kiini macho!!!!

Bila kukomaa, watanzania tutaambulia kufukia mashimo walah![/QUOTE

Kama huelewi,bora uulize.how & why ili walioelewa wakusaidie kuliko kukurupuka.
 
Haitatunufaisha watanzania kwa uzembe wa serikali ya ccm maana wamekaa madarakani tangu uhuru hadi sasa na miundo mbinu, rasimali watu na elimu zote hakuna au ni legelege mno kama kampuni ya GB oil and GAS inyosema.... sasa ajabu iko wapi kama si kuendelea kuitia CCM kitanzini zaidi? CCM wamechoka na akili zao pia.. ya nini wanakuwa vinganganizi wa madaraka....

hata baba na mama wakizaa watoto baada wanawaacha watoto hao wajitegemee na kujiamulia mambo yao wenyewe.. kwa nini ccm isiwape nafasi wengine yaani iseme haitasimamsiha mgombea yeyote katika uchaguzi ujao ili kutoa nafasi kwa mawazo mbadara...

Nadhani kinyume chake ndio sahihi. Wanatamani hata wangeweza wafute vyama vyote vya upinzani wabaki wenyewe.

Watanzania kazi tunayo. Nafasi zote za kutuwezesha kuendelea zinateketea ndani ya CCM.
 
Kawatega....wakitegeka...wakakurupuka....wakasababisha machafuko.....atarudi....atafafanua....ataeleweka....hawataeleweka.....siasa bwana

Mkuu, Nadhani hapa Mh mwenyewe kajitega. Sema tu watanzania wengi bado usingizi Wa pono unawasumbua.
 
Everyday is a new story come out, myself i am not believe and trust for what Pinda
say, that (IDC): could effect the period of ten years.? no-no" and i am telling
you direct that this is not ,,TRUE."
"Intangible Drilling Costs" is generally taken as a deduction in the tax year in which
intangible costs occurred. In short all these Gas drilling contract , are false and
corruptible.
 
You are right, this is another movie story!

But it doesn't matter anyway, cause most tanzanians are in deep and unarousable sleep!
 
Hii nayo kali.

Pinda anaona kuwa watu wa Mtwara waligomea kona ya JK, wakakubali penalti kwake.

Anamalizia tu sasa kuweka ngoma kimiani. Liwalo na Liwe.
 
Back
Top Bottom