Picha ya Karume kubandikwa maofisini

Prince-Mjanja

Member
Apr 29, 2016
18
8
Wazee wa jukwaa habarini.

Nilikua najaribu kujiuliza kuwa, katika maofisi mbalimbali ya serikali na binafsi huwa kunakua na picha ya baba wa taifa na picha ya rais aliyepo madarakani. Sasa nilitaka kujua, kama waasisi wa muungano ni Mzee Nyerere na Mzee Karume, hakuna haja ya uongeza picha ya Mzee Karume katika maofisi ili kumuenzi kama muasisi wa muungano???
 
Karume ni kwa ajili ya Zanzibar tu...!! Ila Nyerere ni BABA WA TAIFA... la Tanzania..na ni Rais wa kwanza wa Tanzania.. sio KARUME..!! umeelewa..?

Tanzania = Tanganyika + Zanzibar...!!

Karume alikuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar.. sio Tanzania..!!

Kama bado hujaelewa wa UDOM wee..!!
 
Huku Tanganyika iwekwe ya Kawawa pia kwa sababu amewahi kuwa Mkuu wa Nchi ya Tanganyika kwa wakati fulani
 
Eti na wewe mjanja? Au kuongeza idadi za thread? Umeishiwa hoja kiasi hiki? Watanzania bana! Utadhani nchi tajiri tumejitosheleza kwa kila kitu,mtu anaanzisha mada isiyo na maana kabisa!!
 
Eti na wewe mjanja? Au kuongeza idadi za thread? Umeishiwa hoja kiasi hiki? Watanzania bana! Utadhani nchi tajiri tumejitosheleza kwa kila kitu,mtu anaanzisha mada isiyo na maana kabisa!!
Kitendo cha Nyerere na Karume kuunganisha nchi mbili kilikua kitendo cha kishujaa kabisa na kinachostahili pongezi au wewe hulioni hilo?? au wewe ni wale wapinga muungano?
 
Karume ni kwa ajili ya Zanzibar tu, hata wao Umewahi kukuta picha ya Nyerere ofisini kwao?

Umewasiliana na KESSY kabla ya kupost hii mada?
Picha Ya mwalimu Nyerere iko katika kila ofisi Zanzibar. Labda point tu ni kuwa Yeye Alikuwa Rais wa Zanzibar wakati baab Wa Taifa alikuwa Rais wa Tanzania yote ikiwemo Zanzibar!
 
Picha ya Mwalimu ipo kama Baba wa Taifa, muasisi wa taifa la Tanganyika, sio Muungano! Karume ni muasisi wa nchi inaitwa Zanzibar, Nenda Zenj zipo kibao, huku ni Tanganyika!
 
nYONGEZA YA HAPO
Karume hakuwai kuwa rais wa Tanzania
 
Kitendo cha Nyerere na Karume kuunganisha nchi mbili kilikua kitendo cha kishujaa kabisa na kinachostahili pongezi au wewe hulioni hilo?? au wewe ni wale wapinga muungano?
Hivi kama muungano wetu ni wa kupigiwa mfano iweje hadi leo hii hakuna nchi imeonesha kutaka kujiunga tofauti na EAC au EU kila kukicha nchi zinawasalisha maombi ya kujiunga.
 
Karume ni kwa ajili ya Zanzibar tu, hata wao Umewahi kukuta picha ya Nyerere ofisini kwao?

Umewasiliana na KESSY kabla ya kupost hii mada?
Kwa kukupa taarifa ofisi zote za serikali Zanzibar,picha ya Nyerere imebandikwa ofisini

Ama kuhusu Kessy, mwanasiasa asiejitambua,nimeusikiliza sana unafiki alioutoa bungeni hivi karibuni na "kuufyata" kwake kwenye bunge la Katiba. Alikuwa mtetezi mkubwa wa serikali mbili na kupinga serikali tatu, ambayo yote alioongea yalikuwa yameshapata jibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…