PICHA: Wananchi Bunda wakusanyika nyumbani kwa Bulaya wakipinga kusimamishwa

Wananchi wa Bunda wamekusanyika nyumbani kwa mbunge wa Bunda Mjini Esther Bulaya wakipinga hatua ya Bunge kumsimamisha Mbunge huyo..
Wamekusanyika au kawakusanya kwa pesa yake?
Hiyo nyumba iko wapi mbona siioni?
 
Kuna watu humu walikuwa wanasema hao wabunge hawana ushawishi wala mashabiki tena ...

Watch this space...
Wakati akitangazwa mshindi nyomi ilikuwa mara nne ya hao. Huenda waungwana wamesusa wamebaki nyumbu.
 
Tatizo letu kama wataanzania tunashindwa au tunapenda kudharau matukio madogo madogo ambayo huashilia vitu fulani vikubwa huko mbeleni.

Nyumba yako inapovuja unaweza kuona ni vitone vidogo vidogo tu na ukadharau lakini baada ya muda vitonevikiunganika huleta mafuriko kwenye nyumba.

Mfano Zenji kuna vikundi vya watu vilianza kumshangilia mgombea wa upinzani "Rais, Rais" watu wakabeza, sasa hivi huduma zinatolewa kwa ubaguzi wa vyama tunaendelea kubeza na kudharau dalili hizi, mwishowe yakishakuja matokeo yake ndio tunaanza kutafutana. Rejea ya amboni pia hali ni hiyo hiyo.

Ushauri wangu: Serikali ianze kuangalia jinsi ya kurudisha nchi iwe moja kwani ni dhahiri nchi inaanza kuvunjika vipande vipande taratiibu.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Serekalio madarakan sio sikivu, ata wakeshe hapo miaka 5, awawez kubadili kitu
 
ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE; wananchi wa Jimbo LA Bunda wamekusanyika nyumban kwa mbunge wao Ester Bullaya wakimsubilia mbunge wao. Mwandishi wetu alieko Bunda amefanya mahojiano na baadh ya wananchi hao."Tutamsubili mtoto wetu mpaka arudi walau tumpongeze na kumtia moyo kuwa aikate tamaa lakini huu ni ujumbe kwa serikali ya ccm na Magufuli wao wakiendelea kumsumbua Ester IPO siku tutaenda huko huko Dodoma tukawaoneshe kazi " alisikika mama huyo akisema Maneno hayo. Habari na picha Lucas Muhavile TN
 
Back
Top Bottom