PICHA: Jionee hali ya barabara za Ifakara kipindi hiki cha mvua ni shida, wabunge chukueni hatua!

Ule mto lumemo ulikua ukifurika tu mafuriko ya mto yanavamia mji hasa maeneo ya sokoni pale.
 
Umeongea baba,huko nilisoma huko.Wakati wa kwenda shule kipindi kama hiki lazima ulie.Kiangazi nayo...Wacha ijengwe dar inatosha wote tutaenda kukaa Dar tucheze tu Pool table.Ukisikia Mkoa wa Morogoro usafiri ni shida sababu za kijiographia huwa napinga.Sababu ni kuwa hakuna anayependa wala kuhangaika kuendeleza hizo barabara Kuu za wilaya.Hii miradi mikubwa minne inayoanzishwa Dar serikali imeshindwa kuwekeza kwenye hizi barabara za Wilaya na Kuingia Mikoani?Kuendeleza sehemu moja na kuacha zingine je unafikiri watu wataacha kukimblia Dar?Hawataacha kamwe..kwa kuwa WANAKARIRI TU DAR DAR DAR..
 
Wasafiri poleni , Jua likipiga masaa 4 hadi 5 mutaendelea na safari. Siku nyengine kumbuka kubeba chakula na maji ya kutosha.
 
barabara kama hii lazima ukianza safari lazima ukumbuke kubeba unga na dagaa.
 
ni uvivu wa kufikiri na misifa ya kijinga
 
Mwaka 2016 unaleta leo?
 
Tuliwaambia chagueni CHADEMA. walugulu wabishi washamba sana mlikataa mkatuona majuha sasa mnaonaaa???? safi sana CCM wasomesheni number piga kazi miaka mingine mitano. tuungane tuandamane hamtaki. wacha mukome!!!
 
Dsm barabara ya mwendo kasi ( sijui mwendo kasi kwenda wapi ? ) , wakati vijijini mahandaki ya kutisha !
Hujui kuwa mjini wanawaogopa? hasa Ilala na Kinondoni!! kijijini wengi mamburulaa!!! hayajui zuri wala baya, ndiyo maana wajanja wanahamia mjini, labda Moshi na Tarime tu wanajitahidi kuwafikiria! wale wa sehehmu hizi wamepinda hawakawii kukupiga mawe na msafara wako wa mbomu ya machozi. hata kukuzomea!
 
Tuliwaambia chagueni CHADEMA. walugulu wabishi washamba sana mlikataa mkatuona majuha sasa mnaonaaa???? safi sana CCM wasomesheni number piga kazi miaka mingine mitano. tuungane tuandamane hamtaki. wacha mukome!!!
Walichagua ila KURA zao ziliibiwa...
 
Wabunge wachukue hatua gani nao hawana mamlaka yeyote kikatiba!!!!! Watakachofanya ni kwenda kubembeleza waZiri au katibu mkuu na huko inategemea anayepeleka shida ni mweupe au mweusi!! Walisema tuwe na serikali za majimbo tupeleke shida zetu kwa magavana tuliowachagua wenyewe, wakasema italeta mgawanyiko, tuendelee kuomba hisani tu.
 
we unasema ifakari kote huko, njoo barabara ya makongo juu! hapa karibu kabisa na ikulu, kama yamechimbwa madimbwi ya kufugia samaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…