Picha: Hawa ndio viongozi shupavu ambao Joyce Banda, PAKA na washirika wake M23 hawatokuja kuwasahau kamwe

6 Pack

JF-Expert Member
Apr 17, 2022
2,812
5,989
Niaje waungwana

Chini ya miamba hii, nchi yetu ilikuwa salama, imara na tishio zaidi kuliko kipindi chochote kile kilichopita, kilichopo na pengine kinachokuja.

Joyce Banda alitest mitambo, kuona kikosi tu na vifaa vichache kwenye taarifa ya habari, huku boss mkuu Kikwete akizungumzia swala la kumshikisha adabu, na kuteka au kuchukua hata kile kipande kidogo walichokuwa nacho, mwenyewe akaondoa wanajeshi wake mipakani, akawaambia wakae mbali na mpaka ili wasijikute wameangukiwa na vitu vizito kutoka Tz.

Congo napo mdhamini mkuu wa M23 na boss wa nchi fulan akataka kumletea Kikwete dharau, akiamini kuwa yeye ndio mbabe wa eneo zima (EAC). Kikwete akawaita vijana wake ikulu ili kujadili namna ya kumshikisha adabu huyo boss na mdhamini wa M23(pichani).

Baada ya kikao kile, kilichofuata ilikuwa ni msiba mkubwa kwa boss wa M23 na genge lake. Na ndomaana mpaka leo hawawezi kusahaulika kamwe kwa operations kabambe na uwezo mkubwa wa kulinda mipaka ya nchi. Mpaka JK anabana meno hapo pichani, basi ujue boss wa nchi nyingine alikuwa amezingua kweli kweli.

Tanzania kwanza, mengine baadae 🇹🇿💪🇹🇿
 
Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    22.7 KB · Views: 4
  • Screenshot_20250202-121209.jpg
    Screenshot_20250202-121209.jpg
    304.6 KB · Views: 5
  • images (2).jpeg
    images (2).jpeg
    46.8 KB · Views: 5
  • images (1).jpeg
    images (1).jpeg
    51.3 KB · Views: 6
Niaje waungwana

Chini ya miamba hii, nchi yetu ilikuwa salama, imara na tishio zaidi kuliko kipindi chochote kile kilichopita, kilichopo na pengine kinachokuja.

Joyce Banda alitest mitambo, kuona kikosi tu na vifaa vichache kwenye taarifa ya habari, huku boss mkuu Kikwete akizungumzia swala la kumshikisha adabu, na kuteka au kuchukua hata kile kipande kidogo walichokuwa nacho, mwenyewe akaondoa wanajeshi wake mipakani, akawaambia wakae mbali na mpaka ili wasijikute wameangukiwa na vitu vizito kutoka Tz.

Congo napo mdhamini mkuu wa M23 na boss wa nchi fulan akataka kumletea Kikwete dharau, akiamini kuwa yeye ndio mbabe wa eneo zima (EAC). Kikwete akawaita vijana wake ikulu ili kujadili namna ya kumshikisha adabu huyo boss na mdhamini wa M23(pichani).

Baada ya kikao kile, kilichofuata ilikuwa ni msiba mkubwa kwa boss wa M23 na genge lake. Na ndomaana mpaka leo hawawezi kusahaulika kamwe kwa operations kabambe na uwezo mkubwa wa kulinda mipaka ya nchi. Mpaka JK anabana meno hapo pichani, basi ujue boss wa nchi nyingine alikuwa amezingua kweli kweli.

Tanzania kwanza, mengine baadae 🇹🇿💪🇹🇿
Mwamba JK alikua anakuchekea mkiwa sebuleni ila akiingia chumbani anakunyooshea rula hadi mwisho wa kitabu. Yule mzee anayeongoza mkoa akidhani ni nchi ilibidi atulie tuliiiiii.😃😃😃😃😃
 
Kule Nyasa haikuishia kwenye maonesho tu, chopa zilipaa juu kidogo tu ya walipoweka kambi kulinda eneo walilokuwa wanadai, wote wakalala chini kuinuka kitu kilishapita na wakatoa taarifa kwa JB kuwa wana wana vitu vizito hapa omba mazungumzo ya amani na usuluhisha kwani madude yaliyopita hapa si ya dunia hii.
 
Waende sasa hv m23 kajiimarisha anagawa doz kwa kutumia drone, hadu HIMMARS, JAVELIN anazo sasa nendeni kichwa kichwa mrudishe maiti.

M23 hawacheki na wowote.
Pitia huu uzi mkuu utajua tu sababu ya sasa ivi kuwaacha M23 watambe.

Tanzania sio Burundi au Congo ndomaana hakuna muasi anaepata chaka la kujificha kwetu.
 
Attachments

  • Screenshot_20250202-134600.jpg
    Screenshot_20250202-134600.jpg
    299 KB · Views: 3
Hapana huyo ni major general Mwakibolwa. Alieongoza operation ya kuwanyang'nya silaha M23 na walipokaidi akawasambaratishia mbali.
Unavyotupanga uongo utafikiri tunavyosimuliwa vita ya kagera. Wote tulikuwepo, usiweke sana chumvi

M23 kama ilisambaratishwa kama unavyosema leo hii isingekuwepo tena. Labda neno kusambaratishwa limebadilika maana. M23 wapo, walikuwepo hawajawahi kusambaratishwa
 
Ndiyo nashangaa kama walisambaratishwa mbona wanaendelea kuzingua
Soma historia. Walisambaratishwa mwaka 2014, chini ya JK baada ya PAKA kutaka kumletea dharau JK.

Hivyo JK akaamua aichukulie issue ya M23 serious ili kumuonesha PAKA kuwa anaweza. Baada ya JK kumuonesha PAKA kuwa anaweza kwa kuisambaratisha M23. Tukarudisha vijana nyumbani na kuwaachia Congo wenyewe jukumu la kuilinda nchi yao.

M23 Wamejikusanya tena mwaka 2021 Congo ikiwa chini ya raisi mungine Tshesekedi na Tz ikiwa chini ya Samia ambae hili swala anashindwa kulichukulia serious kwa vile Congo na Rwanda zote ni majirani zetu. Kisha hii vita haipiganwi katika ardhi yetu wala mpaka wetu.
 
Unavyotupanga uongo utafikiri tunavyosimuliwa vita ya kagera. Wote tulikuwepo, usiweke sana chumvi

M23 kama ilisambaratishwa kama unavyosema leo hii isingekuwepo tena. Labda neno kusambaratishwa limebadilika maana. M23 wapo, walikuwepo hawajawahi kusambaratishwa
Soma post namba 18 mkuu. Lakini pia inashangaza wewe unaejifanya unajua kiswahili haujui maana ya neno kusambaratishwa.

Neno kusambaratishwa linamaana ya kusambazwa ambapo kitu kilichosambazwa au kusambaratishwa kinaweza kujikusanya kulingana na mazingira kiliyopo.
 
Back
Top Bottom