Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 92,962
- 112,778
Akirudi huko na PhD yake ya mchongo kesho zitaanza teuzi maana atakuwa amemiss sn kuteuaKuna wakati tuliambiwa China walimpa u-profesa JK. Hapo ilikuwa ni baada ya kupewa PhD za heshima huku na huko! Sasa tena mambo yameanza!
La kujiuliza eti chuo kikuu cha India kinaona mchango wa Rais wa TZ ni mkumbwa kwao kuliko Waziri mkuu wao. Watu fulani wanashangilia, lakini kwa tunaojali nchi, hapo kuna jambo. Ni wepesi wa kuelewa udhaifu wa viongozi wetu.
Si mulionesha njia kwa UD kumpa rais wetu PhD ya heshima? Eti baada ya mwaka mmoja tu Chuo kikongwe cha UD kikaona huyu ni kiboko kwa mchango wa maendeleo. Ila hiyo ilikuwa kabla ya kuuza bandari zetu.
India waliona na waliskia na naamini ubalozi wao ulitoa taarifa hizo kwamba PhD ni dili kwa Ikulu yetu. Sasa PhD zitamiminika sana! LAkini tujiandae kupoteza vingi. NI sawa na biashara ya shanga na kwa dhahabu na almasi za shinyanga.