Petisheni dhidi ya Diamond Platnamz ili kumzuia kushiriki BET Awards haina mashiko

Doctor Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,057
2,621
1623098260494.png

Diamond Platnums

Mtandaoni kuna petisheni inayoratibiwa na mwanaharakati anayejitambulisha kwa jina la Liberatus Mwang'ombe, na kunadiwa kupitia akaunti za twita za Maria Sarungi, Hilda Newton, kigogo2014, Tundu Lissu, pamoja na gazeti la mtandaoni la Ansbert Ngurumo liitwalo Sauti Kubwa. Petisheni hii imenishangaza sana.

Kila mtanzania mwenye kiu ya haki anachukia itikadi ya umagufuli kwa mawazo, kwa maneno na kwa vitendo. Lakini, kwa mujibu wa petisheni hii naona kuna watu wanaupinga umagufuli kwa Kiswahili na kuutetea kwa Kiingereza.

Na kwa ajili ya bandiko hili, nataka ieleweke kuwa, umagufuli ni itikadi ambayo inahalalisha mambo yafuatayo:

  • Kutengeneza habari feki na kuzisambaza (disinformation),
  • Kusambaza habari feki bila kuchukua hatua za kuzithibitisha kwanza (misinformation),
  • Kusambaza habari za maisha binafsi ya mtu baki bila ridhaa yake (malinformation),
  • Kujipa mamlaka ya kubadilisha ukweli kuwa uwongo au kubadilisha uwongo kuwa ukweli jambo ambalo hata Mungu hafanyi (constructivism),
  • Kuthamini matokeo bila kujali kama njia mbaya zimetumika kufikia matokeo hayo (machiavellism),
  • Kulaghai wasikilizaji kwa kutumia neno lenye maana zaidi ya moja bila kubainisha maana inayokusudiwa (equivocation),
  • Kupotosha kauli ya mtu baki kwa kutafsiri maneno yake kinyume na maana aliyoikusudia yeye (spinning),
  • Kumlaumu mtu kwa sababu ya kosa linalotendwa na rafiki, jirani, ndugu, mtangulizi, au mshirika wake (fallacy of association),
  • Kuwatendea watu baki kana kwamba hakuna tofauti yoyote kati yao na vitu kama vile roboti na wanyama hayawani visivyo na akili wala utashi (objectification),
  • Kubagua watu kwa sababu ya misimamo yao ya itikadi za kisiasa kwa hoja kwamba wao ni kama watoto wa kambo (ideologism).
  • Kutumia dini kama kuchaka cha kuficha uhalifu wa kitaasisi (institutional diabolism)
Ukiweka kando watu wachache waliokuwa wanajipendekeza kwa Magufuli (Magufuli sycophants), watu wengine wote, wakiwemo wafuasi wa Chadema katika uchaguzi mkuu wa 2020, waliukataa umagufuli kwa sababu hizo hapo juu.

Ni kwa sababu hii nimeshangazwa na watu wanaunga mkono
petisheni yenye kuenzi umagufuli kwa kutumia makukwa yanayotumia lugha ya Kiingereza na wakati huo huo kupinga umagufuli kaa kutumia majukwaa mengine yanayotumia Kiswahili.

Tundu Lissu, Ansbert Ngurumo na Maria Sarungi wanaishi nje ya nchi kwa sababu ya kukimbia nchi kutokana na makali ya itikadi ya umagufuli. Lakini sasa naona wao wenyewe wameamua kufanya umagufuli kwa njia ya mtandao kutokea nje ya nchi.

Kuna hoja sita zilizotajwa katika petisheni hii nazo ni hizi hapa:

  1. Kwamba, Diamond Platnamz hakupaza sauti wala kuonyesha mshikamano na wasanii kama vile Roma Mkatoliki, Nay wa Mitego na Idris Sultan, waliopinga utawala dhalimu wa hayati Magufuli.
  2. Kwamba, Diamond Platnamz alitumia bishara yake ya sanaa ya muziki kutakatisha ukatili wa hayati Magufuli na washirika wake kwa kuwajengea taswira chanya mbele ya jamii. Anatajwa kutunga wimbo wa "Magufuli Baba Lao," kupanda katika majukwaa ya kampeni za CCM mwaka 2015 na 2020, na kumfanya Paul Makonda Mlezi wa biashara zake, wakati Marekani tayari imetoa taarifa ya kusema kuwa Makonda anahusika katika kusababisha utendwaji wa uhalifu dhidi ya ubinadamu.
  3. Kwamba, Tuzo za luninga ya BET zimekuwa na heshima mbele ya Waafrika wengi kwa sababu ya kutambua kazi za wasanii ambao wanazo sifa za kuinuliwa kwa sababu wao ni mfano wa kuigwa katika jamii, wakati Diamond Platnamz hana sifa hiyo, kwani yeye ni mbinafsi, mchoyo, bendera fuata upepo, na mtu mwenye kufungamana na mifumo dhalimu.
  4. Kwamba, Diamond Platnamz alitumia bishara yake ya sanaa ya muziki kutakatisha ukatili wa Paul Makonda aliyetajwa na Marekani kuwa anahusika na makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa kumjengea taswira chanya mbele ya jamii.
  5. Kwamba, Diamond Platnamz alitumia bishara yake ya sanaa ya muziki kutakatisha ukatili wa Paul Makonda aliyetajwa na Marekani kuwa anahusika na makosa ya uvunjaji wa haki za watu wenye jinsi tata (GLBITs) kwa kumjengea taswira chanya mbele ya jamii.
  6. Kwamba, Diamond Platnamz ni mwanachama wa CCM, chama kilichokuwa kinaongozwa na hayati Magufuli anayelaumiwa kwa udikteta.

Ninazo sababu kadhaa za kupinga petisheni hii. Nitaeleza kwa kifupi.

Mosi, kitendo cha mfanyabiashara kutafuta faida kwa kuuza huduma kwa mteja mwenye tabia tofauti na yake sio kosa kimaadili wala kisheria.

Pili, kuchagua kukaa kimya juu ya tabia mbaya ya mteja wako ili kukinda uteja kati yenu sio kosa kimaadili wala kisheria.

Tatu, kuchagua itikadi na sera za chama kinachoongozwa na watu wenye tabia mbaya sio kosa kimaadili wala kisheria.

Nne, matamko ya Marekani juu ya uchaguzi wa 2020 na dhidi ya Makonda yanataja tuhuma za jumla (statements of offense) lakini bila kutaja mchanganuo wa tuhuma hizo (particulars of offense).

Matamko ya Marekani nimeyasoma. Hayaonyeshi nani alifanya nini, nani alifanyiwa nini, lini, wapi, kwa vipi, na kwa kushirikiana na nani.

Hivyo, matamko haya hayawezi kutumika kama msingi wa kumtia hatiani mtuhumiwa. Hayana msaada katika mfumo wabutoaji haki kwa mujibu wa sheria. Wanasheria kama vile Lissu wanajua ukweli huu japo wanaonekana kujitoa ufahamu.

Tano, kumshambulia Diamond kwa sababu zilizotajwa hapo juu ni sawa na kubomoa umagufuli kwa mkono wa kushoto na kuujenga tena kwa mkono wa kulia.

Sita, Diamond Platnums ni mfanyabiashara anayeuza sanaa ya muziki kwa yeyote bila kujali itikadi ya kisiasa. Sanaa ni huduma inayonunuliwa kama bidhaa baki, kama vile nguo, mabango, vitabu, vipeperushi, fremu za biashara, magari ya abiria, na kadhalika. Walaji wa huduma hizi wanaweza kuwa na mitazamo tofauti na mitazamo ya muuzaji.

Na muuzaji yeyote anaweza KUTABIRI kuwa kwa kuwauzia huduma/bidhaa yake ILI APATE FAIDA wao wataweza kutumia bidhaa/huduma hiyo kuendeleza mitazamo yao, ambayo hata hivyo, muuzaji hazikubali, bali ANAZIVUMILIA tu.

Saba, Diamond Platnums anayo haki ya kuchagua chama cha siasa na haki ya kubagua vyama baki, tena bila hofu ya kuadhibiwa na yeyote kwa sababu hiyo.

Hapo juu nimeongea kwamba, hakuna "kosa la kimaadili" katika maamuzi yua Diamond. Naeleza kwa nini.

Kisa cha ushirikiano kati ya Diamond Platnums na kina Magufuli, kinaweza, na kinapaswa kutetewa, kwa mujibu wa kanuni ya matokeo pacha (principle of double effect). Kanuni hii inatofautisha kati ya dhana zifuatazo:

  • matokeo yanayotarajiwa (foreseen outcomes);
  • matokeo yanayovumiliwa (tolerated outcomes);
  • matokeo yaliyochaguliwa (intended outcomes);
  • matokeo yaliyochaguliwa moja kwa moja (directly intended outcomes); na
  • matokeo yaliyochaguliwa kwa njia ya mzunguko (indirectly intended outcomes);

Katika kisa cha sasa, pointi yangu ni kwamba, Diamond hakuchagua moja kwa moja makosa ya viongozi wa CCM, yaani hakuchagua umagufuli.

Badala yake, Diamond amejikuta anachagua umagufuli kwa njia ya mzunguko. Aliuvumilia umagufuli wakati anafukuzia malengo yake makuu--faida itokanayo na mauzo ya burudani kwa CCM, itikadi na sera za CCM.

Kuna mifano mingi ya kawaida kwa ajili ya kueleza jambo hili mpaka likaeleweka. Nitatoa mifano kadhaa.

Mfano wa kwanza: Julai 2020, Msajili wa Vyama, Jaji Mtungi, alitamka kuwa kanuni ya 6.5.2(d) ya Chadema ni batili kwa kuwa inapingana na ibara 5.2.4 ya katiba ya Chadema, toleo la 2019.

Lakini Novemba 2020, Kamati Kuu ya Chadema ilitumia kanuni batili ya 6.5.2(d) kuwaadhibu kina Mdee, na hivyo kuvunja ibara 5.2.4 ya katiba ya Chadema.

Sasa hivi wajumbe wa Kamati Kuu wanazunguka nchi nzima kueneza chama, na wanapokelewa na wanachama wa Chadema. Kitendo cha wananchi kuwapokea wajumbe waliovunja Katiba ya chama kinamaanisha kwamba wamechagua matokeo mawili.

Kwanza ni kuchagua moja kwa moja usikilizaji wa sera na itikadi za Chama. Na pili ni kuchagua kwa njia ya mzunguko ushirikiano na viongozi wa Chadema waliovunja Katiba ya Chama.

Hili tokeo la pili linavumiliwa, kwa mujibu wa kanuni ya matokeo pacha, kwa kuwa wanachama hawana mamlaka ya kuwaadhibu viongozi hawa. Chombo chenye mamlaka juu ya Wajumbe wa Kamati Kuu ni Baraza Kuu na sio wanachama wa ngazi za chini.

Katika mazingira haya, wanachama wa Chadema hawajatenda kosa kimaadili.

Mfano wa pili: Askofu Mkatoliki aliyekula kiapo cha useja anazaa mtoto na muumini wake parokiani. Habari zinasambaa kwa waumini. Waumini wanaamua kuendelea kuhudhuria ibada zinazoendeshwa na Askofu. Uamuzi wa waumini unamaanisha matokeo mawili.

Kwanza, wamechagua moja kwa moja kunufaika na haki yao ya kuhudhuria ibada za kawaida. Na pili, wamechagua kwa njia ya mzunguko kushirikiana na Askofu aliyevunja sheria za Kanisa.

Waumini hawa hawana mamlaka ya kumwadhibu Askofu. Wanamvumilia wakiwa wanasubiri mamlaka za juu kuchukua hatua stahiki. Waumini hawa hawajatenda kosa lolote kimaadili.

Mfano wa tatu: Askofu Mkatoliki analo jukumu la kusimamia kiapo cha nadhiri za milele kwa masisita wa jimbo lake. Anatunga kanuni isemayo kwamba, kuna sakramenti mpya iitwayo "sakramenti ya mapenzi." Kisha anatunga kanuni nyingine kwamba, kila sista atakayepewa nadhiri za milele inabidi pia akubali kuwa anapokea "sakramenti ya mapenzi" kutoka kwa askofu, mara moja kila mwezi.

Masista wanaotaka kula nadhiri za milele wanakubali shingo upande kula kiapo cha nadhiri za milele huku wakijua kuwa watapaswa kupokea sakramenti ya mapenzi kila mwezi baada ya hapo.

Masisita hawa, watakuwa wamechagua moja kwa moja nadhiri za milele, na kuchagua kwa njia ya mzunguko sakramenti ya mapenzi kutoka kwa Askofu. Wanavumilia haya matokeo ya pili. Na hawatakuwa na hatia ya kimaadili katika mazingira haya.

Kwa hiyo, kama tunakubaliana na hoja kwamba katika mifano iliyotajwa hapo juu hakuna hatia ya kimaadili, basi, tunapaswa kuona kuwa katika kisa cha Diamond hakuna hatia ya maadili pia.

Hivyo ndivyo, kanuni ya kutojikanganya (consistency), ambayo ni kiashiria cha kanuni ya ukamilifu (integrity) inavyotaka tuenende. Na siasa adilifu zinatutaka kuheshimu kanuni hizi.

Kwa ujumla, umagufuli ni itikadi hatari kwa usalama wa nchi bila kujali kwamba inatekelezwa na wana CCM, wana CHADEMA, watu walio ndani ya nchi, watu walio nje ya nchi, au vinginevyo.

Na propaganda hasi zinazotegemea fallacy of association ni mkakati wa kupakana matope bila uhalali. Ni vivyo hivyo kwa matumizi ya tamathali ya semi iitwayo sitiari (satire) kumchafua mtu.

Siasa za aina hii zinatuweka kundi moja na wafuasi wa itikadi ya umagufuli.

Hivyo, mtu yeyote, awe ni mfuasi wa chama tawala au mfuasi wa chama cha upinzani, anayehalalisha moja kwa moja itikadi ya magufuli hatufai.

Hivyo, namwalika Diamond Platnums kujitokeza na kuthibitisha kwamba anapinga umagufuli kwa vitendo kwa kutunga na kuimba wimbo unaopiga marufuku mambo yafuatayo:

  • Kutengeneza habari feki na kuzisambaza kwa umma (disinformation),
  • Kusambaza habari feki bila kuchukua hatua za kuzithibitisha kwanza (misinformation),
  • Kusambaza habari za maisha binafsi ya mtu baki bila ridhaa yake (malinformation),
  • Kujipa mamlaka ya kubadilisha ukweli kuwa uwongo au kubadilisha uwongo kuwa ukweli jambo ambalo hata Mungu hafanyi (constructivism),
  • Kuthamini matokeo bila kujali kama njia mbaya zimetumika kufikia matokeo hayo (machiavellism),
  • Kulaghai wasikilizaji kwa kutumia neno lenye maana zaidi ya moja bila kubainisha maana inayokusudiwa (equivocation),
  • Kupotosha kauli ya mtu baki kwa kutafsiri maneno yake kinyume na maana aliyoikusudia yeye (spinning),
  • Kumlaumu mtu kwa sababu ya kosa linalotendwa na rafiki, jirani, ndugu, mtangulizi, au mshirika wake (fallacy of association),
  • Kuwatendea watu baki kana kwamba hakuna tofauti yoyote kati yao na vitu kama vile roboti na wanyama hayawani visivyo na akili wala utashi (objectification),
  • Kubagua watu kwa sababu ya misimamo yao ya itikadi za kisiasa kwa hoja kwamba wao ni kama watoto wa kambo (ideologism).
 
Mfano wa pili: Askofu Mkatoliki aliyekula kiapo cha useja anazaa mtoto na muumini wake. Habari zinasambaa kwa waumini. Lakini, jambo hili linavumiliwa na waumini, kwa mujibu wa kanuni ya matokeo pacha, kwani waumini wanaendelea kuhudhuria ibada zinazoongozwa na askofu huyo.

Kwa kitendo hiki waumini wanachagua ibada na kuvumilia uovu wa askofu, wakiwa wanasubiri mamlaka za juu kuchukua hatua stahiki. Nje ya kanuni ya matokeo pacha, waumini wanapaswa kumsusa askofu.

Hebu niambie ni akofu gani wa kanisa katoliki amewahi kuthibitika kuzaa na muumini na hajachukuliwa hatua?
 
Mfano wa pili: Askofu Mkatoliki aliyekula kiapo cha useja anazaa mtoto na muumini wake. Habari zinasambaa kwa waumini. Lakini, jambo hili linavumiliwa na waumini, kwa mujibu wa kanuni ya matokeo pacha, kwani waumini wanaendelea kuhudhuria ibada zinazoongozwa na askofu huyo. Kwa kitendo hiki waumini wanachagua ibada na kuvumilia uovu wa askofu, wakiwa wanasubiri mamlaka za juu kuchukua hatua stahiki. Nje ya kanuni ya matokeo pacha, waumini wanapaswa kumsusa askofu.

Hebu niambie ni akofu gani wa kanisa katoliki amewahi kuthibitika kuzaa na muumini na hajachukuliwa hatua?

Akikujibu nitag
 
View attachment 1812671
Nimesoma petisheni dhidi ya Diamond Platnamz ili kumzuia kushiriki BET Awards lakini haina mashiko. Hoja tatu zilizotolewa ni hizi hapa...
Kwa kweli inasikitisha sana...watanzania tunapoelekea tutachekwa na dunia...Diamond akipewa tuzo ni heshima kwa nchi yetu..anaiweka nchi yetu kwenye ramani ya dunia..hizi frakasi za siasa zibaki ndani nchini kwetu...issue za kimataifa zinazohusu nchi yetu tuwe wamoja kwa maslahi ya nchi yetu..hv Tumelogwa.

Naamini kila mtanzania ana haki ya kumchagua na kumpenda kiongozi anaye resonate nae...ndio maana kuna watu walibusu barabara wakati mwili wa JPM unapita na kunawengine walifurahia. Diamond nae anahaki ya kumsimamia na kusupport kiongozi anayempenda..

Mpigieni kura mtanzania mnaehisi ni likely kushinda hizi tuzo...its unbelievable Nigeria,Uganda etc kumsupport Diamond wakati Tanzania wanafikiria otherwise....jamani!
 
Kwa kweli inasikitisha sana...watanzania tunapoelekea tutachekwa na dunia...Diamond akipewa tuzo ni heshima kwa nchi yetu..anaiweka nchi yetu kwenye ramani ya dunia..hizi frakasi za siasa zibaki ndani nchini kwetu...issue za kimataifa zinazohusu nchi yetu tuwe wamoja kwa maslahi ya nchi yetu..hv Tumelogwa...
Heshima kwa nchi ipi, Yaani mtu aliye upande wa watesi wetu tumuunge mkono kwa kisingizio cha Heshima ya nchi, hiyo heshima inatusaidia nini kama wananchi
 
Mfano wa pili: Askofu Mkatoliki aliyekula kiapo cha useja anazaa mtoto na muumini wake. Habari zinasambaa kwa waumini. Lakini, jambo hili linavumiliwa na waumini, kwa mujibu wa kanuni ya matokeo pacha, kwani waumini wanaendelea kuhudhuria ibada zinazoongozwa na askofu huyo. Kwa kitendo hiki waumini wanachagua ibada na kuvumilia uovu wa askofu, wakiwa wanasubiri mamlaka za juu kuchukua hatua stahiki. Nje ya kanuni ya matokeo pacha, waumini wanapaswa kumsusa askofu.

Hebu niambie ni akofu gani wa kanisa katoliki amewahi kuthibitika kuzaa na muumini na hajachukuliwa hatua?
Wengi tu
 
Kwa kweli inasikitisha sana...watanzania tunapoelekea tutachekwa na dunia...Diamond akipewa tuzo ni heshima kwa nchi yetu..anaiweka nchi yetu kwenye ramani ya dunia..hizi frakasi za siasa zibaki ndani nchini kwetu...issue za kimataifa zinazohusu nchi yetu tuwe wamoja kwa maslahi ya nchi yetu..hv Tumelogwa..
Sisi tunamuunga mkono achana na hao nyumbu wao ni wafuata upepo tu.
 
Wakuu hivi ni mtu gani maarufu ama tajiri ambaye hakuwa "intimidated" na utawala wa mwendazake ili akapate tu kunyookewa na mambo yake? Tuliwaona viongozi wangapi wa kisiasa na kidini, wanaharakati, wanamuziki na hata viongozi wa vyama vya upinzani wote wakiwa "very submissive" kwa mkuu aliyepita ili waweze kuendesha shughuli zao kwa amani.

Tumuunge mkono kijana wetu kwa kuwa naye ni miongoni mwa watu wengi waliokuwa wahanga wa matukio yaliyomhusu mwendazake. Yeye kama yeye Diamond ktk kipindi hicho ilimpasa kumtumikia kafiri kwa ajili ya mradi wake, kama ni uthubutu wa kumpinga ama kumkosoa yaliyowapata wakina Roma Mkatoliki yangaliweza kumtokea pia.

Kijana huyu ni mwenye kipaji cha kipekee ambaye ni kwa vyovyote vile anapaswa kuungwa mkono na wale wote wenye nia njema na mafanikio yake katika masuala ya kimziki. Haitusaidii chochote kile kumuadhibu tu kwa sababu ya yeye kutoonyesha uthubutu wa kupingana na matendo yasiyopendeza yaliyofanyika ktk utawala uliopita.

Naam! Kama tumeamua kumuadhibu kijana wetu basi pia tuwaadhibu viongozi wengine wote wa kisiasa, kidini, wanaharakati hali kadhalika na wengine wote wale waliokuwa wakimuunga hadharani mwendazake.
 
Wakuu hivi ni mtu gani maarufu ama tajiri ambaye hakuwa "intimidated" na utawala wa mwendazake ili akapate tu kunyookewa na mambo yake? Tuliwaona viongozi wangapi wa kisiasa na kidini, wanaharakati, wanamuziki na hata viongozi wa vyama vya upinzani wote wakiwa "very submissive" kwa mkuu aliyepita ili waweze kuendesha shughuli zao kwa amani...
Achana na nyumbu mkuu hawana akili sawasawa wao ni wafuata upepo!
 
Mfano wa pili: Askofu Mkatoliki aliyekula kiapo cha useja anazaa mtoto na muumini wake. Habari zinasambaa kwa waumini. Lakini, jambo hili linavumiliwa na waumini, kwa mujibu wa kanuni ya matokeo pacha, kwani waumini wanaendelea kuhudhuria ibada zinazoongozwa na askofu huyo. Kwa kitendo hiki waumini wanachagua ibada na kuvumilia uovu wa askofu, wakiwa wanasubiri mamlaka za juu kuchukua hatua stahiki. Nje ya kanuni ya matokeo pacha, waumini wanapaswa kumsusa askofu.

Hebu niambie ni akofu gani wa kanisa katoliki amewahi kuthibitika kuzaa na muumini na hajachukuliwa hatua?
Dr mihogo wa sweeden
 
Kwahio angekuwa upande wako ndio angekuwa wa maana na msaada kwa nchi...

Kama wewe haikusaidii haimaniishi wengine haiwasadii...the world does not revolve around you
Hao anaowasaidia wampigie kura. Uzuri ujumbe umefika kuwa siku nyingine asijihusishe na siasa za kiongozi dhalimu, kisha atake kura za wote hata waliokuwa wakinyanyaswa na kiongozi muovu.

Kuna wakati Makonda alijifanya kwenda Egypt kuipa nguvu timu ya taifa, kwa jinsi tulikuwa tunashangilia timu ya ccm kufungwa ilikuwa ni raha ya aina yake. Ifahamike Makonda alishiriki moja kwa moja kwenye uovu na siasa za yule rais dhalimu.

Hata Tanzania ilipoivamia Uganda wakati wa dictator Iddy Amini, waganda hawakusimama na rais wao aliyekuwa mtu muovu. Hivyo Diamond kwa kushirikiana na kiongozi muovu, ni lazima apewe somo kuwa hatuendekezi washirika wa viongozi waovu fullstop.
 
Wakuu hivi ni mtu gani maarufu ama tajiri ambaye hakuwa "intimidated" na utawala wa mwendazake ili akapate tu kunyookewa na mambo yake? Tuliwaona viongozi wangapi wa kisiasa na kidini, wanaharakati, wanamuziki na hata viongozi wa vyama vya upinzani wote wakiwa "very submissive" kwa mkuu aliyepita ili waweze kuendesha shughuli zao kwa amani...
Atoke hadhara aombe radhi, vinginevyo karma itamtandika Kama ilivyo mtandika magufuli, sabaya, na wenzake
 
Back
Top Bottom