Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,171
Hivi bado ana ambitions zozote za kisiasa au lengo lake ni kutetea tu?
HIVI yeye ni nani hasa! unajua tembo akisifiwa!! huyu fisadi kisumo kasifiwa sana eti mdhamini wa CCM etc,
Hivi bado ana ambitions zozote za kisiasa au lengo lake ni kutetea tu
Muda mfupi uliopita ametoa statement ya kukanusha mambo yote yaliyoandikwa gazetini kumhusu yeye kumkandia Kilango na mareale. Anasema anazungumza na wakili wake juu ya hatua za kumchukulia mwandishi aliyeandika kwa sababu yeye hajawahi kufanya naye mahojiano kuhusiana na jambo lolote
Pasipo kuwataja kwa majina wale anaoamini kuwa wamemtuma Kisumo, mbunge huyo alisema alikuwa bado haamini sawasawa iwapo kauli dhidi yake zimetolewa na mwanasiasa wa kariba ya Kisumo, aliyejijengea heshima ndani ya chama na serikali kwa miaka mingi iliyopita.
"Hivi kweli maneno hayo ni ya Kisumo ninayemfahamu mimi! Kisumo yupi? Kisumo ninayemjua mimi ni yule mwanachama mkongwe wa CCM, anayepaswa kuilinda CCM na serikali ili isidhalilishwe na mafisadi.
"Kisumo ninayemfahamu mimi ni kiongozi wa siku nyingi, ambaye amewahi kuwa mbunge, waziri na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, anapaswa kujielekeza kwenye majukumu ya chama," alisema Kilango kwa kujiamini na kwa sauti kali.
Huyo Kisumo hopeless, sasa anataka ku spin mambo!
Huyu Mama anachemka kama kawaida yake, kwanza anasema anawajua waliomtuma Kisumo na hawezi kutetereka, halafu anasema haamini kama Kisumo kasema maneno hayo..
Sidhani kama mama anachemka. Hii ni njia ya kistaarabu ya kumwambia bwana Kisumo kuwa hakupaswa kutamaka maneno kama yale...
Kwa vyovyote wote wawili wanajua kwanini wanapeana maneno hayo..siye tunachoweza kufanya ni kusikiliza na ku harzard a guess kama wengi wanavyofanya sasa ...all in all wana haki ya kuzungumza ili kuondoa yaliyo mioyoni mwao.
Eeeeeeeee shshshssh kumbe alikuwa house boy? ama kweli alidhani kwa sababu ni mzee watu hawamuelewi vizuri? na adharauliwe kwa umbumbu wake....huyu Mzee Ni Mjinga...nimeshasema Mara Nyingi Hapa....nimebahatika Kukaa Naye Na Kumsikiliza Hasa Wakati Ule Wa Uteuzi...maneno Mabaya Aliyokuwa Akiongea Dhidi Ya Salim Na Malecela Hayaandikiki......
Lakini Si Kosa Lake....ni Mjinga Tangu Zamani Miaka Ya Mwisho Ya 50 Alipokuwa House Boy Na Kuli Wa Wahindi Pale Arusha....na Funza Miguuni...daima Mdomo Wake Mchafu Umemlisha..hassa Alipoweza Kuchaguliwa Kuwa Kiongozi Wa Wafanyakazi Wa Ndani..kwenye Chama Cha Wafanyakazi Enzi Zile Na Ikawa Njia Yake Kuingia Siasa....
Huyu Mama anachemka kama kawaida yake, kwanza anasema anawajua waliomtuma Kisumo na hawezi kutetereka, halafu anasema haamini kama Kisumo kasema maneno hayo.
Sasa lipi ni lipi? Hivi lini viongozi wetu watajifunza kuwa na breki za mdomo?
Kama huamini kwamba Kisumo kasema maneno hayo utaendaje kumu attack na kusema unajua waliomtuma?
Kama una confidence ya kusema unajua waliomtuma itakuwaje useme huamini kama Kisumo kasema maneno haya?
Hii inaonyesha low IQ, kukosa mantiki, kupenda misifa na kupenda kubwabwaja tu.
Mama Kilango,
Amesema kuwa haamini kuwa Kisumo anayemjua kuwa anaweza within himself ku-create hayo maneno aliyomrushia, ni kwa sababu haaamini hivyo ndio maana amesema kuwa anawajua waliomtuma Kisumo, ili amrushie hayo maneno yasiyokuwa na heshima kwa kiongozi jasiri wa taifa kama yeye, Mama Kilango,
Kwa hiyo hapa ni clear kuwa kuna mtu mwenye Low IQ, sasa sielewi ni nani kati ya Kisuma aliyetumwa kusema asichokijua, au yoyote yule aliyeshindwa kuelewa maneno ya Mama Kilango,
Tuache kukurupuka na kuropoka manenio ya chooni bila ya kuwa na haja!
In any other case, neno "apologist" lingetumikwa na my good friend FMES.
Hapa Mama Kilango anakuwa "Kisumo apologist" simple and clear.