Pendekezo la“Ukanda Mmoja, Njia Moja” ni chachu ya maendeleo ya nchi za Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,099
1,095
VCG111175896225.jpg


Mwaka 2023 utakuwa muhimu sana kwa nchi zinazojali ushirikiano wa kimataifa, na mwaka huu utaandikwa katika vitabu vya historia kwasababu nchi zote duniani zilizojiunga na Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” (BRI) lililotolewa na rais Xi Jinping wa China zinaadhimisha kumbukumbu ya miaka kumi tangu pendekezo hili lianzishwe.

Mwezi Septemba na Novemba mwaka 2013, Rais Xi Jinping wa China alipendekeza kujengwa kwa Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri na Barabara ya Hariri ya Baharini ya Karne ya 21, ambayo inajulikana kama “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Pendekezo hili tangu kuanza kutekelezwa kwake limekuwa chachu kubwa sana ya maendeleo ya nchi zilizojiunga zikiwemo za Afrika, ambapo fedha za ufadhili zenye thamani ya mabilioni ya dola zimetolewa, na makampuni mengi ya China yamejenga barabara, bandari, reli, vituo vya umeme na miundombinu mingine muhimu kote duniani kwa lengo la kuchochea biashara na ukuaji wa uchumi.

Katika muongo uliopita, zaidi ya nchi 150 na mashirika 30 ya kimataifa yamejihusisha na mpango wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” , na hivyo kuashiria hatua muhimu katika ushirikiano wa kimataifa. Akizungumzia kuhusu matunda na faida zinazopatikana kwa nchi zilizojiunga na pendekezo hili, balozi wa Senegal Ibrahima Sory Sylla amesema pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” ni muhimu sana kwa Senegal ambayo imesaini pendekezo hili mwaka 2018, kwasababu Senegal inatilia maanani ushirikiano wake na China. Kwa sasa anaona lengo la BRI limetimia kwa kiasi fulani kwani pengo lililokuwepo hapo awali la muunganisho wa nchi za Asia, Ulaya na Afrika pamoja na ukosefu wa miundombinu, nchini Senegal na nchi nyingine za pendekezo hili hasa za Afrika tayari limezibwa.

“Lengo kubwa la pendekezo hili kwa Afrika ni kuhimiza maendeleo ya uchumi na kijamii, jambo ambalo ni muhimu sana kwetu. Kwenye mkutano huu wa BRI tumekwenda na vipaumbele vyetu vikiwa ni pamoja na kuongeza miundombinu kwa ajili ya muunganisho, kilimo ambacho ndio mada kubwa kwa nchi za Afrika na mchakato wa ukuzaji viwanda”.

Katika Afrika, Kenya ni miongoni mwa nchi za mwanzo kujiunga na Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, ambalo kwa sasa linajumuisha nchi 46 za bara hili. Akiwa kiongozi wa taifa hilo, Rais Ruto amehudhuria kwenye Mkutano wa Kilele wa BRI ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini China tangu aingie madarakani. Hata hivyo ujio wa rais Ruto umeacha matumaini makubwa kwa wananchi wa Kenya, na ushiriki wake kwenye mkutano huu una umuhimu wa hali ya juu, kwasababu Kenya sio tu ni nchi inayoongoza kwa uchumi mkubwa katika Afrika Mashariki bali pia ni nchi ambayo imeingia makubaliano ya miradi mingi kupitia mpango huu wa BRI, ambayo baadhi yake inalenga kuiunganisha Afrika Mashariki.

Hassan Khannenje ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya HORN ya Tafiti za Kimkakati, amehudhuria kwenye kongamano la ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’ na kusema ni kweli moja ya lengo la rais Ruto kuja kwenye mkutano huu ni kujadili kuhusu uwekezaji zaidi nchini Kenya kupitia pendekezo hili, na kwa sasa pande zote mbili yaani China na Kenya zinaonekana kuwa tayari kuendelea na ushirikiano walio nao katika miaka ishirini iliyopita.

“Baada ya uchaguzi wa mwaka 2003, Kenya ilianza kuegemea zaidi upande wa Beijing na hilo limefanya sasa kushuhudiwa ukuaji na mabadiliko makubwa nchini Kenya. Mtu yeyote anayekwenda kutembelea Kenya kwa saa atayaona mabadiliko hayo waziwazi.”

Hata hivyo amefafanua kuhusu suala la mzigo wa madeni wa Kenya, na kusema kuwa ni kweli deni la Kenya limeongezeka, lakini deni hili sio tu linachangiwa na uwekezaji wa China pekee bali linatokana na nchi nyingine washirika pia.

Ametetea kwamba deni linalotokana na uwekezaji wa China, limeleta matokeo mazuri ya waziwazi na kubadilisha maisha ya mwananchi mmoja mmoja na kila mmoja analijua hilo. Ametupilia mbali kauli za kwamba deni linaitafuna Kenya na kusema kauli hizi ni uongo mtupu zinalenga tu kuvunja moyo wawezekezaji na kuondoa fursa za uwekezaji za Kenya.
 
Back
Top Bottom