Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,635
- 8,946
Wanabodi,
Huu ni uzi kuhusu kitu kinachoitwa "trend Reading" kwa jina la Kiswahili ni "kusoma mielekeo". Katika uzi huu, nazungumzia mielekeo ya Kisiwa cha Pemba, baada ya lile igizo la uchaguzi wa Marejeo wa Zanzibar.
Jee mielekeo ni nini? . Mielekeo ni mambo yatakayokuja kutokea ambayo yamesababishwa na mambo yaliyotangulia kutokea kabla na mambo yanayotokea sasa, ili kujua mambo yatakayokuja kutokea siku zijazo. Kwa kifupi hii ndio maana halisi ya somo la Historia ambayo ni " the study of the past in relation to the present to determine the future". Kujua mambo ya kale na kuyahusianisha na mambo ya sasa ili kujua mambo yajayo.
Kwa kisiwa cha Pemba, hii ndio ilikuwa ngome kuu ya Chama cha CUF, ambapo tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, Pemba yote imekuwa ikishikiliwa na chama cha Wananchi CUF katika nafasi zote za Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, na Uwakilishi wa Baraza la Wawakilishi, na hadi sasa, wabunge wote wa Pemba ni kutoka Chama cha Wananchi CUF, lakini kufuatia Chama cha CUF kususia Uchaguzi, Chama cha Mapinduzi, kimeiteka ngome kuu ya CUF na kuikalia kufuatia ushindi wa kishindo uliopatikana na kutokana na igizo la uchaguzi huo wa marudio.
Japo CUF kina wabunge ndani ya bunge la JMT, wabunge hawa, hawana impact yoyote kule Pemba kwa sababu Bunge la JMT, ni Bunge jina tuu, kuwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Spika wa Bunge ni Spika wa Bunge la Muungano jina tuu, kiukweli, Bunge la JMT, sio Bunge la Muungano, ni Bunge la Iliyokuwa Tanganyika, ila linashughulikia na Mambo yote ya Muungano kwa huku Tanzania Bara Tuu!. Hivyo Bunge ni la Bara, ila limevaa koti tuu la Muungano, hivyo Wabunge wa CUF ndani ya Bunge, hawana impact yoyote kwa Pemba, kwa sababu Bunge la JMT ni bunge jina tuu la JMT ila kiuhalisia ni Bunge la Bara hivyo sio Bunge la Muungano.
Kuthibitisha kuwa Bunge letu sio bunge la Muungano, sheria zote za muungano zinazotungwa na Bunge 'Bara' hazina mamlaka ya kutumika Zanzibar, hadi sheria hizo ziridhiwe na Baraza la Wawakilishi, hii inamaanisha BLW ndiocho supreme organ ya utungaji wa sheria Zanzibar, kituo ambacho wajuvi wa mambo ya katiba, wanakiona kama ni kichekesho, yaani kikatiba, Zanzibar ni sehemu ya JMT, na katiba ya JMT ndio the supreme, na Bunge la JMT ndio supreme organ ya utungaji wa sheria, ambapo Spika wa Bunge la JMT was supposed to be the supreme Speaker, na sheria zikitungwa na Bunge, lazima kwanza ziridhiwe na rais wa JMT (accent) ili ziwe sheria na kuanza kutumika ndani ya JMT, lakini eti sheria hizo, haziwezi kutumika sehemu fulani ya JMT, hadi BLW liridhie, kati ya Bunge la JMT na BLW, nani zaidi?!, yaani sheria imepitishwa na Bunge la JMT, na kuridhiwa na rais wa JMT, itumike ndani ya JMT, halafu haiwezi kutumika eneo fulani hadi iridhiwe na mdudu fulani anayeitwa BLW, hiki ni kichekesho na dharau kubwa kwa mamlaka ya rais wa JMT. No wonder, Rais wetu wa JMT, Waziri wetu Mkuu wa JMT, Spika wetu wa Bunge la JMT, Jaji wetu Mkuu wa Mahakama Kuu ya JMT, they are all nobodies kwenye set up ya Zanzibar, kwa sababu ndani ya Muungano, Zanzibar nayo inajiita ni nchi, ina rais wake, bunge lake, na mahakama yake!.
Sasa nikirudi kwenye hatima ya Kisiwa cha Pemba chini ya CCM, Pemba itahesabiwa alikuwa ni yule mwana mpotevu ambaye alipotea toka kwa baba yake, na sasa amerejea kwenye mikono ya baba yake!, hivyo atafanyiwa karamu kubwa. Atapewa kila anachokitaka na kuletewa hata kila sichokitaka ali muadi kitaonekana kina mfaa!.
Jee Pemba ya CCM, itakuwa ni Pemba ya Raha tele?, ulinzi tele?, maendeleo tele?, uwekezaji tele?, ajira tele?, na itapatiwa preferential treatment kwenye kila kitu?, ili kujenga imani kwa Wapemba kuishabikia CUF, ilikuwa ni makosa, ili itakapofika 2020, wakati wa kuamua tena, wananchi wa kisiwa cha pemba wapate fursa ya kuipima hii miaka 5 ya CCM Pemba, na kuilinganisha na miaka 20 ya CUF Pemba, nani amefanya nini?!. Kwa vile 2020, Wapemba watapata fursa nyingine ya kuamua ama CCM ama CUF, then nawahakikishia kipindi hiki, CCM Zanzibar, haitafanya makosa tena, nguvu zote itazihamishia Pemba, ili 2020, Wapemba wenyewe kwa ridhaa yao, wataivote out CUF katika uchaguzi huru na wa haki, na sio kupitia tena kwenye igizo la uchaguzi.
Au kwa vile Pemba walikuwa wanaichagua CUF, na sasa CCM imeishika kimabavu kupitia lile igizo la uchaguzi, hivyo sasa Pemba watajuta kuichagua CUF, hivyo sasa Pemba chini ya CCM, cha moto watakipa, na kujuta kuichagua CUF, hadi wajisikie walifanya makosa kuitegemea CUF, kuliko kuichagua tena CCM 2020, ni heri wakairudisha CUF yao waliyoizoea!. Jee hii miaka 5 ya CCM Pemba, itakuwa ni miaka ya neema kwa Wapemba au majuto?.
Namalizia kwa lile swali la msingi, "Jee Pemba Chini ya CCM, Itaneemeka Au Kujutia Kuichagua CUF Chaguzi Zilizopita?!".
Nawatakia Ijumaa Kuu Njema.
Pasco
KWANI HAPO UNGUJA CCM INATAKIWA ???
UCHAGUZI WA 2010 SHEIN ALIPATA KURA 3000 hata yake hakupiga
Uchaguzi wa marudio wa CCM peke yake SHEIN KAPATA 58000 , tena za kupigwa zaidi ya mara 10 na mtu mmoja.
Pasco unajidanganya , CCM imeshakufa zamani Zanzibar na huko Tanganyika , Hichi mnachokifanya cha kulazimisha ni kujidanganya na kuongeza hasira za watu. Siku mtakayoanguka ndio hamtoibuka milele .
Siku hiyo haiko mbali kwani ndani ya CCM kuna waliochoka na kuna mchwa wanaila ndani