Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
3,892
9,199
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ikifika Aprili 15, 2024 atawataja kwa majina Watu wakiwemo Mawaziri wanaotoa fedha za kuwalipa Watu ili wamtukane Rais Samia mitandaoni kama hawataacha.

Akizungumza wakati wa Kumbukumbu ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, amesema "Kaka zangu mnaotuma na kulipa watu kumchokoza Mama yangu Samia mnanijua na mimi nawajua, wengine ni Mawaziri leo tarehe 12 iwe mwisho"

Aidha Makonda amemwomba Rais Samia kutoa Fedha za ujenzi wa Kilomita 20 za Lami Jijini humo na kueleza kuwa Wananchi wamemtuma amuombe Mama yake na wanampima kama ni Mama yake kweli

=========

Akitoa salaam za mkoa kwenye kongamano la kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine leo hii 11 April 2024, amesema kuna watu, wakiwemo mawaziri wanawatuma watu kumtukana Rais Samia mitandaoni.

Makonda kasema anawajua na wao wanamjua. Amewataka waache kufanya hivyo leo hii. Ameonya wasipoacha atawataja majina yao siku ya Jumatatu tarehe 14 April 2024.

Unaweza kubashiri ni mawaziri gani wanafanya hujuma hizi dhidi ya bosi wao? Au Makonda anatafuta kiki?

Maana hata jiwe alimdanganya kama hivi, ndiyo maana jiwe akawa karibu sana na Makonda. Jiwe alipokuja kugundua kuwa aliingizwa chaka akamtema.

Your browser is not able to display this video.

Source:. Kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine
=========For English Audience Only==============​
Delivering remarks at a commemorative event for Edward Moringe Sokoine today, April 11, 2024, Makonda stated that there are individuals, including ministers, who are sending people to insult President Samia online.

Based on his claims Makonda stated that he is aware of those individuals and some of them are even ministers. He has warned them to stop and if they won't stop he is going to publicly name them on 14 April 20204.

He further pleaded President Samia to allocate funds for construction of 20 kilometers tarmac road in Arusha city

However based on Makonda's claims one might wonder which ministers are behind these attacks against the President of United Republic of Tanzania. Or is Makonda seeking attention?


Pia, soma=> Rais Samia akiashiriki Misa Maalumu ya miaka 40 ya kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…