Akasankara
JF-Expert Member
- Feb 28, 2015
- 4,101
- 5,610
Mkuu Mcubic, kwanza asante kwa kuangalia kipindi changu cha Saba Saba na PPR, andelea kunifuatilia. Vipindi hivyo vinatangazwa katika vituo vitano vya TV, TBC, ITV, Star TV, Channel Ten, Clouds TV, na ZBC.
Kwa wale wazamani wanaonifahamu tangu enzi zangu za kipindi cha Kiti Moto, wananifahamu na wanafahamu type ya maswali yangu, nikweli jana nilikutana na rais Magufuli kule Saba Saba na baada ya kumsalimia nilimuhakikishia Watanzania wanampenda sana ila pia amezidisha ukali kwa kuzuia mikutano ya siasa.
Katika maisha yangu yote ya miaka 25 ndani ya tasnia ya habari, sijawahigi kuwa muoga, au kuhofia lolote wala yeyote!.
Ni kweli kwenye maonyesho, nilipata fursa ya kumsalimia Mhe. Rais, kwa msiofahamu, Rais Magufuli ni mtu wa kabila langu, na nikienda Chato, nafikia hotelini kwake, na kuna wakati nilifika na wageni fulani wazungu, kula vyakula vya pale kuliwashinda, Mama Janet Magufuli in person, aliingia jikoni kutupikia!. Hivyo ningekuwa ni mtu wa kujikombakomba kwa wakubwa, huu sasa ndio ungekuwa wakati wenyewe!.
Mimi ni muumini wa ukweli daima (nothing but the truth), na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, (freedom of expression and opinion), yaani kuwa mkweli daima, truthfully na kuwa huru kujieleza na kutoa maoni yangu freely kwa kuitumia, freedom of speech, kusema chochote, freedom of expression, uhuru wa kujieleza, freedom of opinion, uhuru wa kutoa maoni yoyote, freedom of movement, uhuru wa kwenda popote, freedom of employment, uhuru wa kuajiriwa kazi yoyote hadi freedom of love, uhuru wa kumpenda yoyote, tena bila limit number ya mtu mmoja mpenzi mmoja, etc!.
Ni kweli Magufuli ni mkali sana, na ukali mwingine hauna sababu za msingi, waliomzunguka wanamuogopa kumwambia ukweli!, kwa vile mimi ni muumini wa ukweli daima, sikuona shida kushauri kwa kuwa Magufuli ni mtumishi wetu, sisi ndio tuliomuajiri kwa kura zetu, na sisi ndio tunaomlipa mshahara kwa kodi zetu, hivyo sisi ndio mabosi wake!. Kwa vile yeye ndie tuliyemchagua kuwa kiongozi wetu mkuu, tunapaswa sio kumuogopa, bali kumuheshimu, na ndicho nilichokifanya, kumuheshimu na kumueleza ukweli kwa unyenyekevu.
Paskali.
'Rais Magufuli ni mtu wa kabila langu, na nikienda Chato, nafikia hotelini kwake...............' Naomba kukuuliza hilo kabila la wasukuma, wasubi au wazinza? ni hayo tu kwa leo. Hongera kwa misimamo isiyoyumba