DOKEZO Pangani: Taka hatarishi za hospitali zinaokotwa ufukweni, Serikali ichunguze wanaofanya michezo hii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Sindano Tanga 1.jpg

Sindano Tanga.jpg
Wilaya ya Pangani, Kijiji cha Ushongo Mtoni kumekuwa na taka hatarishi za hospitali zinazoonekana ufukweni.

Wanakijiji wameshuhudia Drip, Sindano na chupa za dawa mbalimbali ufukweni.

Kuna Hospitali au Kituo cha Afya ambacho haifahamiki kinatupa taka zake baharini, yawezekana zinatoka hata nchi jirani.

Hali hii ni hatari sana kwa utalii wa Pangani na wakazi wa Kijiji chetu. Serikali ifanye uchunguzi kuhusu utupaji taka hizi hatatishi kwa kuwa Kijiji hakina Wataalamu wa kufuatilia.
 
Ni hatari. Na haifai kabisa kutupa taka hizo hovyo. Madhara yake ni linaweza kuibuka janga la kiafya ambalo hatutaelewa ni kemikali? Sumu? Au ni mdudu?

Lakini tusiwaachie mzigo wao tu hata hivyo tuziangalie na sera zetu mnafahamu kuwa kuteketeza taka za madawa chini ya tani moja, si chini ya milioni mbili!!....... hapo NEMC wanakudai milioni na laki mbili keshi kwanza af ndo wanakusikiliza bado TMDA asee ni gharama

Nnajiuliza haya mashirika yanayolipwa na serikali (tunawalipa wafanyakazi kupitia kodi zetu) ni kwanini tena linapokuja suala la kutekeleza sehemu ya wajibu wao, yaani kazi zao wadai tena malipo makubwa hivyo!!?🙄

Anyway, haihalalishi kutupa taka ovyo. Na hilo ni jambo la kukemewa sana. Wakipatikana wapigwe faini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom