Paka Kufungwa Kengele, Siyo la Panya Wote!

Divide and rule!
 
Wenye kumpigania paka asifungwe kengele, bila shaka wana maslah makubwa kutoka kwake, na hao ndo wasaliti waliamua kuwaangamiza wenzao kwa maslah yao, bt wamesahau kua wakimalizika wale wenza paka atawageukia wao na kuanza kumla mmoja mmoja maana hatokubali kubaki na njaa...
 
Ipo siku watakiri kuwa walifanya kosa kubwa sana kulikarisha joka nyumbani mwao. Sasa limetamalaki cha kufanya hawana. Wanaumia kimya kimya wasijue wajinasue vipi. Kabla Magufuli hajamaliza miaka miwili, kuna wataolipuka. Labda wakati huo matumaini mapya yatazaliwa. Lakini madereva hawawezi kuwa hawa hawa wa sasa. Lazima waje wengine kuanza safari upya.
 
Baada ya panya kupelekeshwa na paka, ilibidi wakae kikao kushauriana jinsi ya kumdhibiti paka. Basi paka mmoja akashauri wamfunge paka kengele ili waweze kumsikia anapokua anawawinda (panya). Panya wote wakakubaliana hilo no wazo zuri sana na wakakubaliana wamfunge panya kengele, wote naam, yes, tumepata paka mwaka huu atakoma. Tutaishi maisha yetu bila woga, Mungu mkubwa, at kast, finally, wow basi kila mmoja akishangilia kivyake. Akasimama panya mmoja akauliza, jamani nani atajitolea kumfunga paka kengele?. Ghafla ikawa kimya, panya wooote jiiii!. Nani ajitolee kwenda kumfunga panya kengele, akikamatwa na kuliwa je? Basi mpango wa panya hao ukaishia hapo kwani hakuna aliyejitolea kwenda kumfunga paka kengele.

Hapa kwetu Tanzania, baadhi ya Watanzania tuliokua tunatafuta wa kumfunga fisadi kengele, tumwone, tumkamate, tumtimue kazi na tumchukulie hatua. Basi Magufuli kajitolea kama mfunga kengele. Si wenzetu wametugeuka, wengine hawamtaki mfunga kengele na wengine wanataka mfunga kengele fisadi (paka in panyas' story) wao. Sasa paka atamfunga paka mwenzoe kengele? Fisadi atamshughulikia fisadi mwenzie, mshkaji wake kwenye issues za ufisadi?
 
Mwanakijiji
Mtu ambaye nasikia unaishi nje ya nchi ya nchi tusaidie ni kipi utakacho kwa watu wenye mawazo tofauti?
Watu ambao wanakosoa utendaji wa serikali waelezaje hoja zao?
Waandike kwa kutumia lugha ya namna gani?
Tusaidie illi angalau malumbano,mashairi,kejeli vipungue humu ndani?
Nakuuliza hivyo kwa kuwa kipindi kirefu umekuwa mkosoaji na mwelekezaji katika mambo mengi yanayohusiana na serikali.
Tunaomba ushauri wako.
 
Mwanakijiji
Mtu ambaye nasikia unaishi nje ya nchi ya nchi tusaidie ni kipi utakacho kwa watu wenye mawazo tofauti?

Mbona sijawahi kuwa tatizo na watu wenye mawazo tofauti; labda ni kuwauliza wao kwanini watu wenye mawazo tofauti nao inakuwa ni ugomvi na uadui uliopitiliza? Wana haki ya kutoa mawazo yao tofauti; na wakishayatoa mawazo hayo (kama vile mimi ninavyotoa) wanayo haki ya kusikilizwa au kupingwa; vinginevyo tutajuaje kuwa ni mawazo tofauti?
 
Tulikuwa wamoja katika kuikosoa serikali kw amustakabali mwema wa taifa letu lakini ghafla mwezetu umegeuka hata tunapoonyesha ya wazi unatutungia mashairi.Haya bwana!!
 
Tulikuwa wamoja katika kuikosoa serikali kw amustakabali mwema wa taifa letu lakini ghafla mwezetu umegeuka hata tunapoonyesha ya wazi unatutungia mashairi.Haya bwana!!
Tatizo sio kuunga mkono au kukosoa serikali. Tatizo ni kuunga mkono au kupinga mawazo au matendo ya wanasiasa bila kujali kama wapo serikalini au upinzani!
 
Mzee Mwanakijiji maandiko yako yamepoteza mvuto yaani kama ungekuwa ni bendi basi wewe ni Sikinde ngoma ya ukae.
Paka aliwaambia, tena kwa kuwaapia,
Amebadili tabia, tabia ya kurukia,
Wao wakikubalia, kamwe hatowabugia!
Paka kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…