Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 181,130
- 1,095,066
Eti Slaa "Kirusi"Mkuu inaonesha kunyimwa nafasi 'kirusi' Slaa kugombea urais ilikuuma sana eh?
Binadamu sisi haki ya nani kiboko!
Eti Slaa "Kirusi"Mkuu inaonesha kunyimwa nafasi 'kirusi' Slaa kugombea urais ilikuuma sana eh?
kiongozi, ulamba lamba ni mbaya sana.Ukitaka ukuu wa wilaya kupitia ccm lazima ujitoe ufahamu
Wa kibamba beni pia, msije mkasinzia,
Sio peke mwaumia, hata kina sisi pia,
Majina twavumilia, wasaliti tumekua,
Paka kuja linda panya, panya gani atapona?
Divide and rule!
Ukiona hawa wote, utadhani wako wote,
Wanalia panya wote, wasikika kotekote,
Kumbe lao si lolote, hawamaanishi wote,
Paka kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Paka afungwe kengele, analia panya yule,
Tujue akija pale, anaongeza na yule,
Tumkimbie paka yule, wanasema panya wale,
Paka kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Ulipoanza mkasa, leo nawasimulia,
Panya walifanya kosa, paka kumkumbatia,
Ni kosa la kisiasa, wakaja kulijutia,
Paka kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Paka aliwaambia, tena kwa kuwaapia,
Amebadili tabia, tabia ya kurukia,
Wao wakikubalia, kamwe hatowabugia!
Paka kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Panya wakafikiria, mwisho wakakubalia,
Paka mwana jumuiya, ya panya akaingia,
Vikao kahudhuria, vya panya wale mamia,
Paka kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Kila wanapokutana, kuna panya katoweka!
Ndipo wakaulizana, wameingiwa mashaka,
Kweli inawezekena, paka amekuwa paka!?
Paka kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Paka na akanenepa, huku panya wapungua!
Undugu waliompa, vipi watautumbua!
Ni vipi watamkwepa, bila ya kumshtua?
Paka kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
“Na tumfunge kengele”, wazo likakubaliwa!
Tukisikia kelele, anakuja tutajua!
Hatotushika milele, adui ameshakuwa!
Paka kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Tatizo wakatambua, panya wakafadhaika
Nani watamchagua, aende kwa uhakika,
Na kengele kuinua, kumfunga huyo paka,
Paka kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Wote wakaanza ruka, tena kuruka kimanga!
Wanamuogopa paka, yasijekuwa matanga!
Mabingwa wa kuropoka, midomo waliifunga!
Panya kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Akatokea mmoja, panya asiye na jina,
Akasema neno moja, neno lile alinena,
Yatosha mimi mmoja, kujitoa kiaina!
Panya kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
“Nitamfunga kengele”, na kumfunga huyo paka!
Utawala wake ule, utakoma kwa hakika!
Mwisho wake paka yule, umefika natamka!
Panya kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Akatoka panya yule, kwa mbinu za uhakika,
Yakimcheza machale, akilindwa na mahoka!
Kamkuta paka yule, ameshiba na kuchoka!
Panya kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Paka yule kasinzia, na ndoto zimenogea,
Shujaa kamvizia, huku ananyemelea,
Kaanza kumfungia, huku anamtegea,
Panya kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Mara panya kasikia, wapo wengine walia!
Paka wanamlilia, ati mwanajumuiya!
Ya wale panya mia, paka anaojilia!
Paka kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Waliomsema paka, wakaanza kutetea!
Ana haki za kipaka, vipi tunamuonea,
Amelala amechoka, vipi twamnyemelea!
Paka kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Paka afungwe kengele, au tumuache ale?
Tumtwange na gobole, tumtupe mbali kule?
Twende naye pole pole, paka huyu paka yule?
Paka kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Kwenye himaya ya panya, mfalme hawi paka!
Kuna neno ninaonya, kwa tungo niloandika,
Wakigawanyika panya, ndiyo furaha ya paka
Paka kufungwa kengele, siyo lao panya wote!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Mwanakijiji

Watetezi wa paka wana maslahi na paka siyo panya!
Mwanakijiji
Mtu ambaye nasikia unaishi nje ya nchi ya nchi tusaidie ni kipi utakacho kwa watu wenye mawazo tofauti?
Tulikuwa wamoja katika kuikosoa serikali kw amustakabali mwema wa taifa letu lakini ghafla mwezetu umegeuka hata tunapoonyesha ya wazi unatutungia mashairi.Haya bwana!!Mbona sijawahi kuwa tatizo na watu wenye mawazo tofauti; labda ni kuwauliza wao kwanini watu wenye mawazo tofauti nao inakuwa ni ugomvi na uadui uliopitiliza? Wana haki ya kutoa mawazo yao tofauti; na wakishayatoa mawazo hayo (kama vile mimi ninavyotoa) wanayo haki ya kusikilizwa au kupingwa; vinginevyo tutajuaje kuwa ni mawazo tofauti?
Tatizo sio kuunga mkono au kukosoa serikali. Tatizo ni kuunga mkono au kupinga mawazo au matendo ya wanasiasa bila kujali kama wapo serikalini au upinzani!Tulikuwa wamoja katika kuikosoa serikali kw amustakabali mwema wa taifa letu lakini ghafla mwezetu umegeuka hata tunapoonyesha ya wazi unatutungia mashairi.Haya bwana!!
Hapo umeniacha,sijaelewa.Tatizo sio kuunga mkono au kukosoa serikali. Tatizo ni kuunga mkono au kupinga mawazo au matendo ya wanasiasa bila kujali kama wapo serikalini au upinzani!
Hakuna "kama" kama MTU kaelewa, hivyo unakili kuwa sijaelewa ila kwa Kuwa unataka kwa "lazima" Mimi kuelewa kamwe huwezi jua "kama" nimeielewa.Mbona kama umemuelewe vile! Halafu unajikurupua mwana!
Paka aliwaambia, tena kwa kuwaapia,Mzee Mwanakijiji maandiko yako yamepoteza mvuto yaani kama ungekuwa ni bendi basi wewe ni Sikinde ngoma ya ukae.