Kuna zoezi la ubomoaji wa jengo la zamani la DDC Kariakoo karibu na kituo cha Mwendokasi Msimbazi B, zoezi hilo linaloendelea linafanyika bila uwepo wa kizuizi chochote kulingana na madhari ya eneo husika, kutokana na hali hiyo sasa inasababisha ajali kubwa sana wanaokatiza eneo hilo kwa magari, bodaboda na watembea kwa miguu.
Jambo hilo limeleta taharuki kubwa huku Watu tukibakia kushangaa tukijiuliza kama wanaoendesha zoezi hilo hawakufikiria umuhimu wa kuzingatia usalama wa raia na mali zao.
Ni muhimu Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), wakawachukulia hatua za kisheria wahusika ambao wanatekeleza zoezi hilo hususani mkandarasi ambaye anatakiwa kuzingatia taratibu hasa kwenye eneo kama hilo.
Hali hii ikiendelea itaibua taharuki kubwa kwa wananchi ikiwemo kujichukulia Sheria mkononi maana zoezi hilo linafanyika kwenye mazingira yanayohatarisha usalama wa Watu.