Osaka Raha, Bukoba to Dar siyo gari la kupanda

Wasalaam wanaJF kama ilivyo kawaida huwa tunapeana taarifa na habari mbalimbali zenye lengo la kujenga. Jana nilisafiri kutoka Bukoba kuja Dar na nikapanda gari la Osaka Raha niliyoyashuhudia ndiyo yamenisukuma kuleta uzi hapa.

Kiukweli ni gari mpya wala haina tatizo lolote la kiufundi au kwa lugha nyingine niseme gari haijachakaa wala haliharibiki hovyo njiani mwendo wake wa kawaida tu hamna shida.

Tatizo linakuja kwenye tabia za madereva na wafanyakazi wa hilo gari kwanza hawana ustaarabu ukishakata tiketi basi unaonekana huna maana tena wana lugha chafu kama makonda wa daladala.

Shughuli imeanza asubuhi wakati wa abiria kupanda wanalipisha mizigo kama hawana akili nzuri mzigo wako ukizidi 20kg basi wanachaji elfu moja kwa kila kilo iliyozidi na wala hawana punguzo basi abiria kakata tiketi 60,000/= analipishwa na mzigo elfu20, 15, 30. Kibaya zaidi hawatoi risiti ya hizo hela za mizigo. Mimi niliwakomalia nijue kwanza hiyo rate ya 1,000/= kwa kila kilo imepangwa na nani? Na pili nikilipa nipewe risiti lakini waligoma almanusura niachwe stendi huku nikipewa matusi ya kila aina na kuambiwa nitarudishiwa nauli ofisini wakati gari limeshaondoka nilisaidiwa na askari aliyewaamuru kama wananiacha basi wanirudishie nauli yangu kabla hawajaondoka nipande gari nyingine. Hapo wakaona pagumu kurudisha nauli ikabidi wanipakie tu kumbe walitaka wanitapeli ionekane nimechelewa gari imeniacha.

Baada ya sereka hiyo safari ikaanza kisanga kingine kikaja kwenye kuchimba dawa duh hawa jamaa ukizubaa wanakuacha na hawajali watu wanalikimbilia gari wakati linaondoka. Tumepiga mwendo kutoka Kahama hadi Singida 302km masaa matano bila kuchimba dawa wakati magari mengine tunaona wanachimba dawa sisi ni mwendo tu hadi abiria tukaomba watusaidie lakini wapi wanajidai eti wana haraka wao wakipata kinafasi kidogo cha kupakia abiria wanaenda kuchimba dawa wanatuacha sisi abiria.

Mziki ukaja pale mtoto alipolilia kujisaidia wakamshusha halafu wakampandisha kabla hajajisaidia eti wana haraka mwishoe dogo akaaharisha kwenye gari na harufu ikasambaa gari zima lakini hawakujali kama abiria tunapata shida wakaendelea na safari hadi kelele za abiria zilivyozidi ndo wakasimamisha kwa kutupa dk5 tu almanusura tuwaache baadhi ya abiria. Aisee sipandi tena hili gari.


Badala ya kupoteza muda humu ulitakiwa kutoa taarifa SUMTRA CC taasisi ya walai wa huduma zinzosimamiwa na SUMATRA. Hata ukigoogle utwapata anuani zao.
 
sie w

Sisi wapole sana ati... asikwambie mtu
ila hawa wenye mabasi wanajionaga ni miungu watu

Magufuli tuleteeni treni watu wawe na heshima mjini hapa
Mubarikiwe kwa upole wenu/wetu !! ila Biashara na Tajiri hilo la upole na huruma halipo ktk kamusi lao!!
mabasi wananunua kwa mkopo wa Benki... na benki haina huruma wala Upole !!
Sasa wenye mabasi wapo kikazi zaidi !!!!
 
Mlishindwa nini kuwapa kibano? Na wanafanya kazi kutokana na utaratibu mnaoutaka nyie...
 
Kwani hamkupewa namba ya police maana kila basi kubwa ya masafa malefu kabla ya kuondoka askari hupanda kutoa lecture including namba ya police mnapewa. Niliiandika hii wakati natoka dar kwenda kahama. By the way Osaka raha nadhani ni moja ya mabasi yanayoendeshwa kwa umakini mkubwa and is one of my favourite

Police Tanzania
0682887722
Piga namba hiyo popote ulipo msaada ni instant
 
Watu karibia 60......mlikubalije kunyanyaswa hivyo na watu 4/5.....?.......mlishindwa kuwazaba vibao.....?.......
sio wanne wala watano ni wawili tu kondakta na dereva, yaani hawa watu walikua goigoi sana.
 
Mngekunya basi zima humo humo ndani ya basi lao, wangeipata fresh.

By the way, Sumatra walikataza watu kusimamishwa porini kuchimba dawa, wakisimama wanafanya kosa.
sumatra yenyewe imejenga vyoo wapi, msitu kujazwa mbolea sio vibaya, hata ukiwa shambani, unatafuta kichaka kidogo unachimba dawa, kuchimba dawa polini raha ukiwa na karatasi ngumu eheeee
 
OSAKA ROUT YA BUKOBA -Dar , mawakala wenu ni wezi wamenichuma pesa ya kusafirisha mzigo na mzigo haujafika kwa muhusika , mzigo ulikuwa na thamani ya laki tano na elfu hamsini na pesa ya usafiri 25000 vyote wamekula namba za wa husika ni:0762965601(Juma) na mwingine sijamfahamu jina namba yake ni 0755532137, kwakweli nimeumia Mungu ndiye anajua
 
Back
Top Bottom