Orodha ya waliosomeshwa na serikali lakini hawataki kurudisha mkopo ili watoto wetu wasome

hakya nanihii hata kwa upanga wa moto mie silipi! Nilipigwa mabomu baada ya mkopo kuchelewa kwa miezi 2 tuapigwa mibomu, nikavunjwa mguu na ndani nikalala bila kupelekwa Hosp. hadi leo natembea mguu huu nauvuta kwani haukurudi sawa tena! Silipi! silipi! labda nao waandamane tuwapige maweee! Na bado sitolipa! WAENDE WAKADAI ZA ESCROW, EPA.MEREMETA, RADER, RALCO, NSSF na IPTL.
Naunga mkono hoja, usilipe, usilipe, usilipe, usilipe, usilipe, usilipe milele yote hadi mungu atakapokupenda zaidi.
 
Acha umbea wewe, tulipe kwani tulikopeshwa kwa raha? Mkopo gani kupata hadi upigwe mabomu? wakitaka tuwalipe waje nao tuwapige na mabomu ya machozi sio wanadai hela tu wakati kuna watu waliwatoa hadi ulemavu. Silipi ng'oooo hadi hela za escrow zirudi.


Mkuu umenichekesha sana. Maana hakuna namna nyingine, ili twende sawa...
 
Uwezo wa serikali kuwasomesha wanafunzi wote elimu ya juu, kwa ruzuku inawezekana! Urasimu umewajaa viongozi wa nchi hii, hadi kufikia hatua ya kuwanyima haki ya msingi watoto wa kimaskini, hatuna haja ya kuwakopesha na kuwadai wanafunzi wanaosoma elimu ya juu.Maliasili na rasilimali tulizojaliwa hapa nchini, kodi mapato mengine tunayoyapata pamoja na misaada mbalimbali tukichukua angalao asilimia moja au mbili, inatosha kabisa kugharamia elimu ya juu.
 
Naazimia kuwafichua waliosomeshwa na serikali kwa pesa ya walala hoi lakini hawataki kurudisha, tunaomba tuwataje hapa na sehemu wanazo fanya kazi ili serikali ichukue hatua wakamatwe na ikiwezekana wafikishwe mahakamani.

1. Word vision wapo zaidi ya 100
2. UN wapo zaidi ya 20
3. UDSM wapo zaidi ya 2000
4. SUA wapo zaidi ya 1000
5. NACTE wapo zaidi ya 100
6. BODI YA MIKOPO wapo zaidi ya 120
7. BENKI KUU wapo zaidi ya 800
8.
9.
Majina nitawela kila baada ya muda leo naachia hapa.
Mkuu hebu tuwekee taarifa rasmi ya kuaminika kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika. Weka taarifa inayojitosheleza.
 
Tupe na orodha ya waliokula hela za EPA,ESCROW,MEREMETA,KAGODA,DEEP GREEN n.k na hawataki kuzirudisha ili zifanye mambo mengine ikiwa ni pamoja na kusomesha wengine.
Rudisha hela,, acha kupoteza mada
 
Kwanza wengi ni watoto wa walalahoi unawatakia nini?, unaacha kupinga kitendo cha jecha unatuongezea machungu
Duuu!! Wazee.
Mmemgeuka Magu mapema hivi.

Sasa naona watu watapiga mambo kwa makusudi wakikipizia Zenji
 
Acha umbea wewe, tulipe kwani tulikopeshwa kwa raha? Mkopo gani kupata hadi upigwe mabomu? wakitaka tuwalipe waje nao tuwapige na mabomu ya machozi sio wanadai hela tu wakati kuna watu waliwatoa hadi ulemavu. Silipi ng'oooo hadi hela za escrow zirudi.
Sasa na nyie kukopa gani kwa vurugu hivyo?
 
Nyie hamna tofauti na wahujumu uchumi, safari hii mtalipa. majembe yupo njiani kila mwajiri amepeleka majina mtakutana na wito wa mahakamani. either ulipe au kifungi miezi 6. we subiri.
Sisi tusiokuwa na kazi nani anapeleka majina yetu
 
Kamshahara kenyewe kadogo, kanakatwa katwa tuuu, lakini hakuna noma tunao uzoefu na maarifa tutaenda sawa tu
 
Mtoa mada unapaswa kufahamu jambo moja.70% ya wadaiwa wa bodi ni watoto wa maskini.80 ya waliokopeswa ni walimu.unaposema wafungwe watoto utafundisha wewe?
 
Back
Top Bottom