FananiMedia
Member
- Jul 29, 2021
- 28
- 84
PART-1
"Mapambano tunayowaitia hayana mahusiano na mijadala ya Socrates wala mawazo ya plato wala diplomasia za Aristotle.
Yana mahusiano na mijadala ya mauaji, ulipuaji na uharibifu.Serikali ya Kiislam Kamwe haijawahi kutokea wala kutokea kuanzishwa kupitia ufumbuzi wa amani na mabaraza ya ushirikiano.
Walianzisha kwa kutumia peni na bunduki, maneno na risasi...ulimi na meno" --Sehem ya nukuu ya utangulizi katika kitabu cha mafunzo ya Al-qaeda kinachoitwa "Military Studies in the Jihad Against the Tyrants".
September, 1997 Kuna Kijana mwenye asili ya Sudan alikuwa anatembea pembezoni mwa barabara ya watembea kwa miguu katika makutano ya barabara ya Moi na Haile Selassie kuelekea ilipo ubalozi wa Marekani ndani ya jiji la Nairobi.
Kijana huyu Alikuwa ni Double Agent, Jina lake anaitwa Jamal Ahmad, alienda ofisi za Ubalozi wa Marekani kupeleka taarifa nyeti za watu saba ambao wanafanya kazi katika mashirika binafsi wenye uhusiano wa karibu na kundi la Al-qaeda lililochini ya Bin Laden.
Taarifa alizozitoa zilihusu mipango ya siri ya mashambulizi iliyokuwa inapangwa na kundi hili.Maofisa wa Ujasusi wa ubalozi walizipuuza Taarifa zile za Jamal Ahmad na kuziona hazina uhakika.Walichokifanya ni kuwaomba serikali ya Kenya kuzifanyia kazi.
Mwezi ule ule wa November kuna mtu mwingine mwenye uraia wa Misri, Jina lake ni Mustafa Ahmed aliomba nafasi ya kuonana na Balozi wa Marekani jijini Nairobi, Prudence Bushnell.
Alivopata nafasi ya kuonana na Balozi alimpa taarifa kuhusu kikundi cha watu chenye mafungamano na Mtandao wa Al-qaeda kuwa wanampango wa kulipua Ubalozi wa Marekani jijini Nairobi kwa kutumia mlipuko wa kupandikiza katika gari.
Taarifa hizi mbili zilikuja tofauti lakini zilikuwa ni zenye kufanana. Maofisa wa CIA waliokuwa ubalozin walimfanyia Mustafa Ahmed mahojiano yaliyochukua muda mrefu ili kuona kama kuna uhakika wa taarifa zake.
Baada ya kumfanyia mahojiano yale, CIA wakahitimisha(Analysis) kuwa taarifa za Bwana Mustafa Ahmed pia ni za Uongo. Ila Wakamuomba Balozi Prudence Bushnell kuomba msaada wa kutafuta ukweli wa hizi taarifa.
Balozi Bushnell akaandika barua kwenda Washington lakini maombi yake hayakupewa kipaumbele Kikubwa.
Kilichofanya taarifa hizi kupuuzwa sababu ya kwanza: hakukuwa na viasharia vya kiitelejensia(Threat Intelligence) vya wanamgambo wa Al-qaeda katika nchi ya Kenya.
Hii inathibitishwa na kauli aliyoitoa aliyekuwa mratibu wa kitengo cha kudhibiti ugaidi Henry Crumpton.
." Hadi kufika August 1998 CIA walikuwa bado hawajaamka" Kauli ya Mratibu wa Idara ya udhibiti wa ugaidi, Henry Crumpton akizungumzia tukio la shambulio la 1998 na chombo cha habari cha declassified Uk.
Alimaanisha kuwa CIA ilikuwa bado haijaamka na kushindwa kuwa Al-qaeda wataweka Target yao kwa nchi za Afrika.Huenda kama wangezifanyia kazi taarifa hizi simulizi zingekuwa tofauti.
Sababu nyengine ni ya kihisia Inawezekana sababu ya kutoziamini ni kuhofia Dezinformatsiya( Taarifa za uongo zinazotolewa kwa adui ili kumpoteza katika mipango ya kweli).
Hii ni opereshen iliyofanywa na wanamgambo wa Al-qaeda kulipua ubalozi wa Marekani jijini Nairobi na Dar es salaam. Usipate tabu kugoogle.... Operation Bang and Burn Sio jina rasmi ya hii operesheni iliyofanywa na Al-qaeda. Nimeiita Operation Bang na Burn ni kutokana na maafa na madhara yaliyotokea katika hii operesheni.
Nini kilitokea kabla na baada ya mashambulizi?.
Tukirudi nyuma mwaka 1989, Baada ya jumuia ya Soviet kushindwa vita nchini Afghanistan, Osama bin laden aliamua kurudi katika nchi yake ya Saudi Arabia.
Akiwa nchini Saudi Arabia alikuwa anajihusisha na usimamizi wa kampuni ya Ujenzi iliyokuwa inamilikiwa na Baba yake. Aliishi maisha ya kawaida kama ya wafanyabiashara wengine.
Mwaka mmoja mbele alichukizwa sana na kitendo cha Serikali ya Saudi Arabia kuruhusu nchi ya Marekani kuweka kambi ya kijeshi kuipiga Iraq iliyokuwa inaongozwa na Saddam Hussein katika vita ya Persian Gulf.
Kitendo kile alikiona kama ni usaliti kwa nchi yenye Utamaduni wa kiislaam kuruhusu Marekani kuweka kambi yake kuipiga Iraq.
Aliendesha harakati za kuikosoa vikali serikali ya Saudia kwa maamuzi yale. Licha ya serikali ya Saudia kumuonya, Hakusita wala kuogopa, aliendeleza harakati zake.
Ilivofika 1991 serikali ya Saudia ikaamua kumfukuza na kumfutia Uraia wake Osama Bin Laden. Katika jitihada za kuondoka alifanikiwa kupata hifadhi nchini Sudan chini ya Raisi Omar Al- Bashar.
Hifadhi ya nchini Sudan ilimsaidia sana kujiimarisha na kupanga mikakati ya Kisasi kwa taifa la Marekani. Kwa nyakati tofauti Viongozi wa dini wa kundi la Al-qaeda walitoa matamko kuhalalisha mauaji kwa raia wa Marekani.
Kwa mujibu wa 3,000 word report ya shambulio la 1998 Ubalozi wa Marekani uliofanywa na Wamerekani wakishirikiana na mamlaka za kenya ilitoa orodha ya watu 7 muhimu waliopanga operesheni hii.
PART-2
FBI wanaamini watu hawa ndo waliohusika kwa kiasi kikubwa na shambulio la Nairobi ;
1-Fazul Abdullah mohammed( Nitamtaja kwa kifupi kama Fazul)
2-Abdullah Ahmed Abdullah( Nitatumia jina lake la utani la Salehe au Abuu Mariam).
3-Mohammed Sadiq Odeh( Nitatumia jina lake la mwisho la Odeh).
4-Fahad Mohammed Ally( huyu ni mmiliki wa pick up iliyotumika kubebea mlipuko).
5- Abdul Rahman( Huyu ni mtaalamu wa milipuko/ mabom).
6-Mohammed Rashid Daoud Al-owhali( Nitatumia jina la Al-owhali).
7-Jihad Mohammed Ali( Nitatumia jina lake maarufu la Azzam).
Ili kupata picha ya jinsi mpango ulikuwa unahusisha watu hatari ambao waliitwa wanamgambo lakini walikuwa na ujuzi mkubwa wa mambo ya kijeshi.
Nitaalezea historia fupi za baadhi ya watu muhim waliofanikisha operesheni hii kwa wakati mmoja ndani ya miji miwili mikubwa kibiashara ya Nairobi na Dar es salaam.
FAZUL ABDULLAH MOHAMMED.
Ni mwezi wa sita mwaka 2000 kuna kelele za boti yenye kasi zilikuwa zinasikika katika pwani kisiwa cha Siyu kilichopo karibu na mji wa Lamu.
Ndani ya boti kulikuwa na dereva na abiria watano, mmoja kati ya abiria wa tano alikuwa ni kipenzi cha wakazi wa kijiji cha Siyu chenye jumla ya makadirio ya watu 1500. Kipenzi huyo cha watu wakazi wa kijiji chake walimfaham kwa jina la Abdul karim.
Abdul karim alikuwa ni kijana mpole, mwenye huruma na mkimya sana.
Wakazi wa kijiji walimfaham kama ni mhubiri wa dini.Alikuwa akilingania watu kufanya matendo mema na kutoa mafunzo ya dini ya kiislaam.
Alianzisha madrasa(shule za kiislam) nyingi na misikiti ikiwa ni juhudi zake za kuendeleza uislam. Baada ya kulowea alimuoa Binti wa miaka 16 wa mfanyabiashara maarufu wa kijiji iko anaietwa Amina Bint kubwa.
Wanakijiji wanamuelezea Abdul karim alikuwa anamiliki simu nyingi na ni mtu anaetumia muda mwingi sana kuongea na simu.
Abdul karim mara kwa mara alikuwa anatembelewa na wageni wengi waliokuwa wanatoka nje ya kijiji iko.
Miaka miwili baadae, November's 2002 kuna kundi la maofisa wa jeshi la polisi la kenya wakiambatana na maofisa wa shirika la ujasusi la marekani ( FBI) liliwasili katika kijiji cha siyu. Lengo la ujio wao ni kukusanya taarifa za Abdul karim.
Ujio wa kikosi kazi cha jeshi la polisi uliwashtua wakazi wengi wa kijiji baada ya kugundua mtu ambae kwao ni kipenzi chao alikuwa anatafutwa na jeshi la polisi kwa kutuhuma za ulipuaji hotel ya Paradise iliyoua watu 16 na mamia ya watu Kuachwa majeruhi.
Pia mtu huyu alihusishwa na ulipuaji wa ubalozi wa Marekani jijini Nairobi.
Wanakijiji walimtambua kama Abdul karim ila kikosi kazi kilimtambua kama Fazul Abdullah Mohammed.Kijana mwenye asili ya Comoro aliechukua uraia wa kenya.
Ni mbobezi katika fani ya lugha mwenye uwezo wa kuongea lugha nne tofauti: kiswahili, Kingereza, Kifaransa na Kiarabu. Na nii mtaalam pia wa kompyuta.
Baadhi ya wanakijiji walizidi kushangaa baada ya kuambiwa Abdul karim ni mtu anaetafutwa sana na FBI, walizidi kupagawa zaidi walivoambiwa kuna donge nono la 5 million Us dollar kwa ataekafanikisha kutoa taarifa zitakozosaidia kumpata Abdul karim.
Katika Tovuti ya FBI walimulezea kama ni mtu hatari, mwenye majina zaidi ya 18 akiyatumia sehem tofauti tofauti. FBI walishindwa kujua ni tarehe ipi sahihi aliyozaliwa sababu alishatumia passport za kusafiria zaidi ya tatu zenye miaka tofauti.Haikushangaza sababu huyu jamaa ni mtaalam wa kufoji.
Alihusishwa na matukio mengine mengi ya ugaidi yalitokea katika pembe na pwani ya Afrika Mashariki.
Alihusishwa na mashambulio ya mauaji ya askari 18 wa marekani mwaka 1993 katika mji wa mogadishu.
Katika 3,000 word report ya shambulio la 1998 Ubalozi wa Marekani uliofanywa na Wamerekani wakishirikiana na mamlaka za kenya Fazul ni mmoja wa makamanda muhimu wa Osama Bin Laden aliyepewa mafunzo nchini Pakistan aliyekuja kurith nafasi ya Kamanda Al-banshir aliefariki katika Ajali ya Mv Bukoba.
Fazul baada ya kupewa mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Al-qaeda nchini Afghanistan alienda nchini Sudan kuonana na Bin Laden, Fazul alipewa majukumu kwenda kuwasaidia viongozi wa Al-shabab kupigana na Wamerekani katika Operation restore hope.
Baada ya kupigana Somalia,Mwaka 1993 Fazul alipewa maelekezo ahamie kenya kwa ajili ya opereshen itakayofuata.Fazul alihamia kenya akiwa na rafiki yake aliyesilim mwenye asili ya Lebanon ambaye alichukua uraia wa marekani anaitwa Wadih El Hajj.
Fazul alichagua kisiwa cha Siyu kama kambi ya operesheni yake kwa sababu kisiwa cha siyu ni sehem ambayo serikali ya kenya ilikitenga kwa muda mrefu kwa kuwa nyuma kimaendeleo ya jamii.
Pia Kisiwa cha siyu kipo karibu na Somalia, ni umbali wa dakika 40 kwa boti yenye spidi.Kwake ilikuwa rahisi kufanya safari za kenya- Somalia.
Kisiwa cha siyu kilikuwa nyuma kimaendeleo, wakati fazul anahamia kisiwa cha siyu kulikuwa hakuna hata Signal( mawimbi) ya sauti ya Radio ya Taifa ya kenya. Shirika la umeme la kenya lilikuwa halifahamiki kwa wakazi wa mji huu.
Walikuwa nyuma sana, kuna utafiti ulifanywa baadae na Gazeti la Sunday Nation mwaka 2004 ilionesha katika kundi la watoto saba waliwahoji hakuna hata mmoja alieweza kutaja jina la Raisi wa Kenya.
Miongoni mwa mambo aliyoyafanya Fazul ili kuteka mioyo ya jamii alianzisha timu mbili za mpira wa miguu.
Aliwapa vifaa vya michezo,timu ambayo yeye mwenyewe alikuwa ni golikipa aliipa jina la Al-qaeda na timu nyingine akaipa jina la Kandahar ( ni mji upo Afghanistan ambao Fazul alichukua mafunzo ya kijeshi).
Fazul alipendwa sana na wakazi wa kisiwa cha siyu kutokana na misaada mingi aliyoitoa kwa jamii. Alioa katika ukoo wenye hadhi wa Kubwa.
___________________________________________
PART-3
MOHAMMED SADIQ ODEH( ODEH)
Huyu Kijana mwenye asili ya Palestine alizaliwa nchini Saudia Arabia na familia yenye asili ya Palestina.Baadae akaenda kusoma elimu ya ngazi za juu (HIGH LEVEL) nchini Jordan.
Mwaka 1986 akajiunga na chuo cha Far Eastern University cha Nchini Filipino.Nchini Filipino alisomea fani ya Usanifu na Uhandisi( Architecture and Engineering).
Akiwa nchini Ufililipino alikuwa anapenda kusikiliza mawaidha ya Sheykh Abdallah Azzam( Alikuwa ni Kiongozi wa kidini wa Mujahideen katika vita ya Afghan na Jumuia ya SOVIET). Mawaidha ya Sheykh Abdallah Azzam yalimshwaishi kuingia katika Jihad.
October,1990 akiwa mwaka wa mwisho wa masomo, Odeh aliamua kuacha chuo na kwenda Pakistan , Pakistan hajakaa sana akaenda Afghanistan kujiunga na Mujahideen.Alikaa Afghanistan kwa miaka miwili na miezi mitano. Akiwa Afghanistan alijifunza utaalam wa milipuko.
1992 alipewa maelekezo kutoka kwa Bin Laden kupitia Saiful Adil kuwa yeye na baadhi ya ya wenzake waliambiwa waende nchi Somalia kumsaidia Sheikh Hassan katika vita yake dhidi ya Wamerekani.
Baada ya kupambana vita Somalia kwao waliita vita yenye mafanikio.1994 alipewaa maagizo aende nchini Kenya kwa kazi maalumu.Nchini Kenya alipewa Jukumu la kuwa sleeper cell ( Ni Jasusi aliyesinzia anaejifanya kuishi maisha ya watu wa kawaida ili kuficha siri ya kazi yake).
Alioa binti mwenye asili ya Kiarabu aliyekuwa anaishi nae Witu. Akiwa nchin Kenya, Odeh aljihusisha na kazi ya uvuvi na ufundi seremala kwa nyakati mbili tofauti.
MOHAMMED RASHID DAOUD AL OWHAL
Huyu nae alikuwa ni mtu muhim sana katika hii operesheni.Al-owhali alizaliwa 18, January,1997 jijini Liverpool, England ila Malezi yake alikulia nchin Saudi Arabia.
Baada ya kumaliza Elim yake ya Sekondari alijiunga na chuo cha dini cha Muhammad Bin Saud, Saudia Arabia.Katika ukuaji wake alikuwa anapenda kufuatilia mawaidha ya Shaykh Omar Abdal- Rahman raia wa Misri.
Sheykh Abdal-Rahman alikuwa akisifika kwa kutoa mawaidha yenye misimamo mikali na isiyoyumba ya kidini.
1996, Al- Olwhal akiwa na baadhi ya washkaji zake walienda hadi Afghanistan katika kambi ya Khaidan kujiunga na kundi la Al-qaeda. Akiwa katika kambi ya Khaidani alipewa mafunzo mbalimbali ya kijeshi ikiwemo utekaji na ujuzi wa kutumia Mizinga mikubwa( Artillery)
WADIH- EL HAJJ
Wadih El Hajj alizaliwa 1960 nchini Lebanon na familia ya Roman Catholic. Alikulia nchini kuwait sababu Baba yake alikuwa anafanya kazi katika moja ya kampuni ya mafuta nchini Kuwait.
Akiwa bado kijana mdogo chini Umri wa miaka 18 alibadili dini na kuingia katika Uislam baada ya Kusoma baadhi ya Aya katika kitabu cha Qur-an.
Wazazi wake hawakukubaliana na imani ya mtoto wao kusilim wakaamua kukata baadhi ya huduma, ilivofika 1979 kwa msaada wa Sheykh alipata fursa ya msaada katika chuo cha University of Southwestern Louisiana.Akiwa chuoni alisoma fani ya Mipango miji(Urban Planning).
Kama ilivyo kwa wanachama wengine wa Al-qaeda. El hajj alikuwa anapenda sana mawaidha ya Sheykh Abdallah Azzam. Huyu Abdallah Azzam ndo aliependekeza Jina la Al-qaeda.
KHALFAN KHAMISS MOHAMMED ( Kk Mohammed)
KK alizaliwa kisiwani Zanzibar nchini Tanzania. Makuzi yake yalikuwa katika misingi ya dini. Alikuwa anatumia muda mwingi kujifunza mambo mbalimbali ya dini yake ya Kiislam.
Alipenda kujifunza elimu ya dini kuliko elimu dunia( Secular Education), ivyo ilimpelekea hadi kuacha shule akiwa Elimu ya upili( Secondary) na kujikita zaidi kwenye Elim ya dini.
Akiwa na miaka 17 alitoka Zanzibar na kuhamia jijini Dar es salaam kwa kaka yake aliyekuwa anakaa Mtaa wa Arusha, Ilala. Kaka yake alikuwa anajihusisha na biashara ya uzaji chakula, ivyo na yeye aliingia katika biashara hiyo kumsaidia kaka yake kukidhi mahitaji ya familia.
Akiwa Mtaa wa Arusha alikuwa ni mhudhuriaji mzur wa ibada katika Msikiti wa Arusha. Mwaka 1995,Pale Masjid alipata connection ya kwenda Afghanistan kujiungana kundi la Al-qaeda.Baada ya kumaliza mafunzo yake aliambiwa arudi Dar es salaam asubiri kazi atakayopangiwa. Alivorudi Dar es salaam akarudi tena kufanya kazi kwenye biashara ya kaka yake.
...........
MPANGO KAZI WA ULIPUAJI.
Vyombo vingi vya habari vilikuwa vinawaita wanamgambo ila mipango na mikakati waliyopanga ilionesha kuwa ni watu wenye ujuzi wa kijeshi.
Katika mipango yao walitumia njia ya Counterintelligence Principle ambayo inatumiwa na CIA katika opereshen zao.
Al-qaeda walitumia njia ya Tactical deception and Strategics Suprise ( Mbinu za ulaghai na Mikakati ya kushtukiza).
Kwenye mafunzo ya kitabu Cha " "Military Studies in the Jihad Against the Tyrants" kilichoandikwa na Double Agent wa Al-qaeda ambaye alijichomeka katika Jeshi la Marekani , Sergeant Ali Mohammed aliwafundisha wanamgambo wa Al-qaeda mbinu za "TACTICAL DECEPTION AND STRATEGIC SUPRISE" ili kuficha utambulisho wao ( Disguise Identity).
Moja ya njia waliyotumia kuficha utambulisho wao ni kuanzisha biashara na mashirika yasiyo ya kiserikali na kutumia majina ya uongo. Kwa mfano FAZUL ABDULLAH MOHAMMED ameshawahi kutumia majina zaidi ya 18 katika nyakati tofauti.
Asilimia kubwa ya mipango ya ulipuaji wa balozi izi mbili ulifanywa nchini Kenya. Viongozi wengi wa hii operesheni walikuwa wapo Kenya wakioongozwa na Mohammed Sadiq Odeh aliyekuwa ni mshauri na mtaalam wa mabomu pamoja na Fazul Abdallah waliokuwa chini ya Usimamizi wa Kamanda Abu Ubaidah Al- Banshiri aliyekuwa anaishi Tanzania.
...................
Hizi ni baadhi ya taasisi na biashara walizofungua ambazo nyuma yake zilikuwa zinahisaniwa na mabilion ya pesa za Billionea Osama Bin Laden:-
Mwaka 1993, Kundi la Al-qaeda lilisajili kampuni ya Kibiashara Nchini Kenya.Kampuni iyo waliita Asma Limited iliyojisajili kwa ajili ya biashara ya kuagiza na kuuza bidhaa nje ya nchi( Import- Export business). Lilisajiliwa na Bwana Khalid Fawwaz ambae baadae alihamisha umiliki kwenda Kamanda wa Al-qaeda Abu Al banshiri.
Lengo la kunzisha kampuni hii ni kutafuta urahisi wa kuendesha mipango yao mbalimbali ya kulipiza kisasi kwa Serikali ya Marekani ( Undercover Operation).
ZIADA:Huyu Al-banshir pia akishirikiana na shemeji yake walifungua kampuni ya madini nchini Tanzania.Baadae wakafungua biashara ya daladala.
Baadae,Baada ya El-haji kuingia Kenya.El-Haji kwa kushirikiana na mshkaji wake Fazul walianzisha shirika lisilo la kiserikali(NGO's) waliloita Help African people ambalo asili yake nchini Ujerumani.
Taswira ya nje ya taasisi ilikuwa tofauti na ndani, nje ilikuwa ni shirika kwa ajili ya kusaidia watu mbambali wasiojiweza kwa kutoa misaada ya huduma za kijamii, walisaidia kutoa chakula, mavazi, madawa na makazi. Licha ya misaada waliyokuwa wakiitoa lengo lao mama Ilikuwa kupitisha hela za Al-qaeda kusaidia operesheni zao.
Nae kwa upande wa Mohammed Odeh naye akaanzisha kampuni yake ya kuvua samaki. Biashara hii ilimsaidia kufanya matembezi bila kikwazo akienda kuchukua mzigo wa magendo Kismayo, Somalia anakuja kuuzia Kilifi nchini Kenya na kuna nyakati alikuwa anakuja kuuza hadi Tanzania.
Biashara hii ilisaidia kueneza taarifa kwa wana mtandao wa Al-qaeda. Mara nyingi Odeh alikuwa anauza na kusafirisha samaki usiku. Taarifa hizi zilipowafikia idara ya uvuvi nchini Kenya. Mwishoni mwa mwaka 1997 idara ya uvuvi ikampa onyo kuacha kufanya biashara usiku.
Odeh alikuwa anatumia muda wa usiku sababu kuna nyakati alikuwa anachukua mizigo hatari ya magendo kutoka Somalia ivyo kwa mchana ilikuwa vigumu kuipitisha.
Baada ya kupewa onyo Odeh akaamua kuiacha biashara hii ya uvuvi na kwenda kufungua biashara ya ufundi Seremala na shemeji yake. Alifungua biashara na shemeji yake sababu Odeh hakuwa na ujuzi wa ufundi seremala ivyo alihitaji mtu ambaye anajua kuifanya.
Haikuchukua muda mrefu kuna mtu mwengine akaanzisha kampuni nyingine iliyoitwa Tanzanite King iliyohusika na biashara za madini hasa madini ya Tanzanite. Hii kampuni ilipiga sana mkwanja.
Kampuni hii ni moja ya kampuni iliyofanya kenya kutambulika na baadhi ya nchi kama ni mzalishaji wa madini ya Tanzanite wakati Madini ya Tanzanite yanapatikana nchi moja tu ya Tanzania.
Baada ya kuanzishwa kampuni hii ya Tanzanite King, Fazul na El- Hajj waligawana majukumu. Fazul alibaki kusimamia shirika la Help African people. Na El hajj akawa anasimamia biashara za Tanzanite king.
Mwaka 1994, Al-qaeda walimtuma mtu mwengine anaeitwa Mustafa Ahmed kuanzisha kampuni nyingine iliyoitwa Bin Laden Taba Investment Company lilikuwa na tawi lake jijini Nairobi na baadae ikatanua shughuli zake hadi nchini Tanzania.
May 1996, Mipango ya shambulio ilififia baada ya kiongozi mwandamizi wa Al-qaeda Abu Al banshiri kufariki katika ajali ya MV Bukoba. Abdullah Ahmad Abdullah ( Saleh) alirithi nafasi ya Abu banshir.
ZIADA:Huyu Saleh alikuwa mwanachama wa Egyptian Islamic Jihad na ni mchezaji wa mpira wa miguu, aliichezea timu ya Ghazl El Mahalla ya Misri
1996 Wadih El hage( muuza vito) Kupitia kampuni yake ya Tanzanite King alipokea dola 7,000 na kumpa Bwana Odeh( mvuvi) kuanza maandalizi ya oparesheni.
Odeh alitumia hii hela kwenda kununua vifaa vya ulipuzi vilivyonunuliwa jijiji Luanda na kusadikika kupitia nchin Tanzania kupitia kwa mtu mwenye asili ya Mombasa aliyefahamika kwa jina la Fahid Mohammed Ally Msalam.
Katika kipindi cha mipango yao walitumia code za maneno( Cryptology)katika kuwasiliana. Ilikuwa vigumu kwa mtu aliye nje ya mpango kazi kufaham.
Kwa mfano TNT na vilipuzi waliita ZANA, Bomu la mkono walikuwa wanaita VIAZI, Passport za kutembelea waliita BIDHAA.
21, December,1996 El- Hage alituma barua ya siri kwenda Baku nchini Azerbaijan, barua iyo ilikuwa na passport tatu za bandia ili kuwawezesha vijana hao watatu wasafiri kutoka Azerbaijan kwenda Kenya. Kati ya watu hao watatu mmoja wao ni Daoud Al- owhali.
February, 1997 El Hage alisafiri kwenda Pakistan kuonana na Bin Laden kumpa mrejesho wa Intelligencia walizozifanya ukanda wa Afrika Mashariki.
Alienda Pakistan sababu Kipindi iki ambacho Bin laden aliondoshwa Sudan na Rais Omar Al Bashar baada ya kupokea shinikizo kubwa kutoka kwa Mataifa ya kiarabu na Marekani kwa kumhifadhi Osama Bin Laden.
Baada ya taarifa zile za El Hage,March 1997, bin Laden akamuagiza Odeh kwenda Somalia kutathmin hali ya mambo inavoenda kwenye operesheni zinavofanywa na Al- Shababa.
Odeh alikaa Somalia kwa miezi saba kisha akarudi kenya kijiji cha witu kilichopo mpakani mwa somalia na kenya kuendelea na maandalizi ya shambulio.
Alivyorudi Kenya toka Somalia akawa anaijihusisha na kazi ya ufundi seremala uku akisubiri tamko la mwisho la Osama Bin Laden.
Sababu ilyomfanya Bwana Odeh abadili kazi. Wakati Odeh alikuwa anajihusisha na biashara ya samaki, biashara yake alikuwa anaifanya usiku alivokatazwa kuifanya usiku akaamua kuiacha baada ya kuona serikali ilishaanza kumshtukia kwa kumfanyia upelelezi.
ZIADA;Huyu Bwana Odeh Licha ya kujiingiza katika kazi ya useremala kuna kipindi alipewa kazi na Shirika la Help Africa, rafiki yake Fazul alimpatia kitambulisho cha kazi ili aende kuwadanganyia familia yake kuwa amepata kazi jijini Nairobi.
Hii ilimsaidia Bwana Odeh kupiga trip nyingi za Mara kwa mara za Mombasa-Nairobi.
...........
Nchin Afghanistan kuna mtu mwengine alitumwa. Mtaalam wa Mbinu za kiitelejensia, mauaji,utekaji na milipuko. Alitumwa jijini Nairobi kukamlisha mipango ya opereshen.
Mtu huyu ni nani ? Na nini kitafuatia ? Kaa Tayari kufuatilia uzi huu.
PART-4
Tarehe 2, August kuna mtu alikuwa anatua uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Nairobi akitokea nchini Afghanistan. Kazi yake ilikuwa kwenda kujitoa mhanga siku ya tukio.
Huyu jamaa ni Mtaalam wa Mbinu za kiitelejensia, mauaji,utekaji na milipuko. Mtu huyu jina lake ni Rashid Daoud Al-Owhali.
Alivoshuka alikodi taxi hadi Hotel ya Ramada na alipewa chumba namba 24.
Alipiga simu Pakistan kutoa taarifa kuwa ameshafika. Mfanya mawasiliano wa Pakistan akapiga Simu Nairobi kwa Fazul kumpa taarifa kuwa Al-owhal kashafika umna na amefikia katika hotel ya Ramada.
Hapa kuna funzo kubwa jinsi hawa jamaa walivokuwa ni wataalam wa ulinzi wa mawasiliano( Communication security). Walifanya hivi ili kutunza usalama wa agent wao wa Nairobi.
Baada ya Fazul kupata taarifa.Siku iyo iyo Fazul aliendesha gari hadi nje ya hotel ya Ramada na kwenda kumchukua mgeni wake. Zililipwa gharama zote za hotel licha ya mgeni kutokaa kama muda alioweka booking.
Alimchukua na kumpeleka nyumba namba 43 mtaa wa Runda Estate.
Kabla wiki haijaisha kuna raia mwengine wa Afghanistan anaitwa Jihad Mohammed Ali " maarufu kama Azzam" alipokewa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyeta akapelekwa kujiunga na wenzake katika kambi ya Runda Estate.
Huyu kazi yake ilikuwa ni kwenda kuendesha gari itakayobeba mlipuko toka Runda Estate kwenda Ubalozini.
Baada ya watu muhim kuwasili Na kumaliza kufanya upembuzi yakinifu na kukusanya taarifa nyingi za Intelligence kuona kama ni muda sahihi wa kuendesha operesheni.Osama Bin Laden au "The Manager"Kama walivyopenda kumuita alituma taarifa ya kuruhusu kufanya opereshen ya ulipuzi.
Taarifa zile alipewa Fazul ambae alikuwa master mind wa Nairob.Kipaumbele chake cha kwanza cha Fazul kilikuwa ni kununua gari kwa ajili ya kubebea vifaa vya kutengenezea mlipuko na kupanga nyumba kwa ajili ya kuitengeneza mlipuko.
Kwa msaada wa dalali Mr Sikander Juma alifanikiwa kupata nyumba Mtaa wa Runda House nyumba namba 43 iliyokuwa inamilikiwa na Bwana Tamarra Ratemo.
Mr Tamarra aliambiwa na Dalali Mr Sikander Juma kuwa Fazul atapangisha kwa muda wa miezi mitatu.
Dalali alimwambia mmiliki kuwa Fazul anahitaji kuishi na familia yake pamoja na wageni anaotarajia kuwasili siku za iv karibuni.
Kumbe Malengo sio haya aliyoambiwa malengo hii nyumba itumike kama ghala la kutengeneza mlipuko.Familia ya Fazul ilikuwa inaishi nyumba aliyokuwa anaish Mr Sikander pamoja na El-Hage sehem nyengine ndani ya jiji la Nairobi.
Mazingira ya Nyumba ya Runda Estate yalikuwa mazuri,kulikuwa na vyumba vinne vya kulalia, vyoo vitatu na sehem ya gereji kwa ndani.
Kazi ziliendelea ndani ya nyumba namba 43, gari aina ya Toyota Dyna iliingizwa ndani ya mjengo na kuna gari ndogo ya pick up ilikuwa inaingia na kutoka ikiwa na kazi ya kukusanya malighafi ya kutengeneza mlipuko.
Fazul alisimamia utengenezwaji wa milipuko miwili mikubwa yenye uzito wa tonne 1 ( Sawa na Kilograms 1000) iliyotengenezwa kwa kutumia TNT, mbolea na unga wa Aluminium.
Baada ya Fazul kumaliza kazi yake aliitwa Abdel Rahman kwenda kufanya kazi ya kuzungusha umeme katika mlipuko.
Baada ya kazi kukamilika, Tarehe 1 August ya mwaka 1998, Kamanda wa Al-qaeda Afrika Mashariki aliyerith nafasi ya Abuu Ubaida Al- banshir.
Huyu alikuwa Mchezaji mpira katika moja ya timu ya ligi kuu nchini Misri anaitwa Saleh au Abuu Mariam alitoa amri kwa wahusika wote nchini kenya isipokuwa wale wenye kazi ya kupeleke mlipuko ubalozini itakapofikia Tarehe 6, August wote wanatakiwa waondoke nchini kenya walekea Pakistan.
Nini kitafuat usikose part- 5 ya simulizi hii
AT THE END OF YOUR WORLD.
WELCOME TO OUR WORLD.