Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,752
- 5,601
Ndugu zangu kwanza nianze kwa kusema kitu kimoja, mimi sio mchawi, mshirikina ama vyovyote vile ila ninakuandikia haya kama kukuelezea nguvu ya vitu alivyoviumba Mungu.
Mungu alimuumba binadamu kutoka kwenye udongo, hii inamaanisha nini? Kwamba kitu cha kuuponya huu mwili upo kwenye udongo. Yaani dawa ya udongo ni udongo. Ndiyo maana dawa zote duniani hutengenezwa kwa kupitia miti. Kwa sababu gani? Miti huchipua udongoni, hivyo dawa ya mwili ulioumbwa kwa udongo huwa ni udongo.
Wakati najifunza mambo mengi, nikapitia suala la chumvi. Chumvi ina nguvu sana, chumvi imetumika tangu enzi hizo za zamani kuonyesha ni kwa namna gani imewaondolea watu mikosi mingi.
Sikiliza! Dunia haipo fea hata kidogo. Maybe unahisi una nuksi zako, watu wamekufanyia mtimanyongo, usigombane nao, chukua chumvi ya mawe, weka kwenye maji, nenda kaoge kwa siku 7, 14 ama 21. Kama kuna mtu alikuwekea nuksi, biashara zako zisiende, amini, baada ya kufanya hivyo kila kitu kitakuwa sawa.
Huu si uchawi, si ushirikina. Mungu amemuumba binadamu na kumpa kila kitu kwenye dunia hii, wale waliobahatika kuwa na uwelewa ndiyo wanawasaidia watu wengine. Leo unaambiwa mti wa mwarobaini unatibu magonjwa zaidi ya 40. Ni bora kutumia dawa za asili kuliko hospitalini, ila lazima uwe na uelewa nazo.
Ukienda kwa waganga, nao wanatumia chumvi kukutibu, makanisani, kuna mtu anasema mpaka maji ya baraka, yale ya ubatizo yamewekewa chumvi, unaambiwa ukiwa na nuksi, nenda kaoge maji ya baharini, kwa nini isiwe maji ya ziwani?
Mwanamke unayenyonyesha, ukiona umetoka kutembea kwenye umati wa watu, unashauriwa chukua maji, weka chumvi ama magadi kisha nenda kaoge, halafu mnyonyeshe mtoto wako. Chumvi ina siri kubwa sana, chumvi inawasaidia watu wengi mno.
Kuna mwingine unahisi umelogwa, usiende kwa mganga, nunua chumvi ya mawe, kaogee, hata kama biashara zako zilikuwa vibaya, kila kitu kinakuwa sawa kabisa.
Nawakumbusha tena na tena! Huu si uchawi na si ushirikina. Kuna watu wengi wametoa ushuhuda kuhusu chumvi, inamaajabu sana, tatizo moja kubwa sasa hivi tunaishi kidigitali, hatujui lolote lile kuhusu umuhimu wa chumvi kuondoa nuksi.
Ukisoma zaidi kuhusu chumvi, imeandikwa mpaka kwenye Biblia, inatumika hata kwenye urafiki, kasome 2 Chronicles 13:5. Pia kasome Hesabu 18:19, chumvi imezungumziwa sana huko.
Kwa wale ambao wanahofu na mambo ya kulishwa limbwata, ukimaliza kula chakula ambacho unahisi kina sumu ama limbwata, chukua chumvi, lamba ya kutosha halafu endelea na mambo yako.
Mungu ameweka nguvu kubwa sana kwenye chumvi. Wazungu walipokuja, waliyajua haya yote, walichokifanya ni kutuficha tu, na Wazungu hawahawa ni watumiaji wakubwa wa chumvi za mawe. Ukienda Marekani ama Ulaya, chumvi halisi za mawe huuzwa kwa bei kubwa mno. Kama huna pesa huwezi kununua. Wao hutumia zaidi chumvi za kutengenezwa kiwandani.
Maybe unafanya biashara zako halafu pesa huioni, usihangaike kwenda kwa waganga eti kuna watu wanakuibia pesa kimazingara, hakuna uchawi wowote utakaokusaidia, chukua chumvi, nenda kaogee kwa siku hizo 7, 14 ama 21, ama hata miezi miwili. Kila kitu kitakuwa kinavyotakiwa kuwa.
Unafanya biashara zako maybe dukani kwako, halafu unahisi kabisa umechezewa, wewe usihangaike, chukua chumvi na nyunyizia tu sehemu hiyo kuzunguka duka lako. Nakukumbusha huu si ushirikina, hiki ni kitu chenye nguvu sana kiimani.
Kutumia chumvi haijalishi wewe ni Muislamu ama Mkristo, yeyote anaweza kutumia, uzuri wa chumvi huwezi kutumia kwa ubaya, eti fulani aharibikiwe maisha nitumie chumvi, hapana, hii hutumika kuondoa mamikosi watu waliyokutumia, kuondoa nuksi ambazo watu wamekutumia ili usifanikiwe.
Kwa wale Wakristo wanaweza kwenda kusoma kuhusu chumvi kwenye vitabu hivi.
2 Wafalme 2:19-22
Waamuzi 9:45
Ezekiel 43:24
Ezekiel 16:4
Walawi 2:13
Sometimes inawezekana kuna dada unahisi watu wamekuzibia riziki zako za kuolewa. Kuna watu hawapendi kuona fulani akiolewa, wewe wala usiende kwa mganga, nenda kaogee maji yenye chumvi bafuni, fanya hivyo kwa siku 7, 14 ama 21 utapata majibu.
Nguvu za giza hazipatani na chumvi. Ukisikia bundi analia nyumbani kwako, sijui paka yaani hakueleweki, chukua chumvi halafu choma huku ukivitaka viumbe hivyo viondoke haraka sana. Majibu utakuja kuyaona tu, tena haraka sana.
Mungu ameipa chumvi nguvu kubwa sana. Ni vile tu hatujui kwa sababu kizazi chetu ni cha kidigitali, tunaamini sana utandawazi kuliko mambo kama haya.
Kuna jamaa aliniambia “Nyemo, hata sisi Wakatoliki ikitokea umekosa maji ya baraka, chukua maji safi, weka chumvi na unaweza kusalia Baba yetu, Salaam Maria...sikuwa nikimuelewa kipindi kile, ila kwa sasa naanza kumuelewa alimaanisha nini.
Kwenye kitabu cha Mathayo 5:13 Yesu aliwaambia wanafunzi wake: (Nyinyi ndiyo chumvi ya dunia) Nao Waarabu husema: (Kuna chumvi kati yetu)
Chumvi imekuwa alama ya uthabiti na udumifu. Hiyo ndiyo sababu kwenye Biblia agano muhimu liliitwa ‘Agano la chumvi’. Chini ya sheria ya Musa, chumvi ilitiwa kwenye matoleo madhabahuni, bila shaka ikionyesha hali ya kutokuwa na ufisadi au uharibifu wowote ule.
Unakumbuka jinsi watu walivyomlilia Elia kwa kumwambia mji wao ni mzuri ila maji mabaya na nchi haizai matunda? Elia akawaambia “Nileteeni bakuli jipya na mtie chumvi ndani yake” Wakampelekea, akachukua, akaenda kwenye chemichemi na kutupa chumvi ndani yake akisema: Hilo ndilo asemalo BWANA, nimeyaponya maji haya na hayatasababisha kifo tena wala kufanya nchi isitokee.”
Chumvi ina siri kubwa sana. Wakati mwingine unaota ndoto mbaya tu, wewe ni mandoto ya kuzimu, wala usihangaike, chukua maji yako, weka chumvi kisha nenda kaoge.
Namna ya kutumia ni hivi! Nunua chumvi ya mawe, chemsha maji yako, yawe ya uvuguvugu. Usiyaoge kwanza, chukua maji ya kawaida, oga, jisugue na sabuni, ukiwa msafi, chukua yale maji yenye chumvi ambapo tayari itakuwa imeyeyuka, anza kuoga. Fanya hivyo kwa siku 7, 14 ama 21 mfululizo, mara moja kwa siku. Fanya hata mwezi mzima. Unaweza kuoga leo, na ukapata majibu leoleo.
Utakapoanza kutumia maji hayo, kitu cha kwanza unaweza kuanza kupata usingizi mzito sana, unaweza kuota ndoto za kukuonyesha jinsi wabaya wako wanavyoanza kuondoka mwilini mwako.
Kuna watu wanasumbuliwa na tatizo la kujichua (Punyeto). Hiyo ni roho chafu, wengine wanasumbuliwa na uzinzi, hiyo ni roho chafu, utakapoanza kuogea maji hayo uliyoweka chumvi, nikwambie tu hizo roho zote zitaanza kutoka. Roho chafu huwa hazipatani na chumvi hata kidogo.
Mungu ameweka nguvu kubwa kwenye chumvi. Duniani tunachezeana sana, Mungu aliliona hivyo na ndiyo maana akaweka tiba na vitu vingine kwenye ardhi kwa kujua kuna siku binadamu watahangaika, tiba itakuwa ni hii.
Mtoto wako anaweweseka usiku, hizo ni roho chafu, muogeshe kwa maji ya chumvi na tatizo litakwisha mara moja. Haya mambo yanaendana na imani yako, wakati unatumia, amini kwamba kila kitu kitakuwa kama kinavyotakiwa kuwa.
Kuna watu wametoa ushuhuda wa mambo mengi tu, jinsi walivyokuwa hawakai na pesa ila baada ya kuogea maji ya chumvi bafuni, wakaanza kukaa na pesa, jinsi watu walivyokuwa wakisumbuliwa na ndoto chafu, baada ya kutumia maji yenye chumvi bafuni, kila kitu kikabadilika.
Anza kuoga maji uliyoweka chumvi ya mawe leo, kwa chochote kitakachotokea njoo utushirikishe, wasioamini, waamini ama kama ulikwishawahi kutumia, unaweza kutuambia hapa.
NB: Mkaa husaidia kukukinga na mambo machafu. Ukiwa unatoka nyumbani, chukua kipande cha mkaa, weka mfukoni halafu tembea nacho. Mamikosi yote ya barabarani ambayo ulitakiwa kuyapata hutoweza kuyapata tena.
Ndugu zangu, huu si uchawi, si ushirikina. Ni nguvu ya vitu ambavyo Mungu ameviweka duniani kwa lengo la kutaka na sisi tupambane na wabaya wetu.
Kumbuka chumvi haitumiki kumnenea mtu mabaya, wakati unaweka kwenye maji, sema unataka nini kitokee, kila kitu kitakwenda kama unavyoomba.
TUNASAIDIANA! ILA KAMA WEWE MTU WA IMANI SANAAAAAAA. POTEZEA HILI SUALA.
Manake kuna msichana majuzi aliombewa kazi TRA na mshikaji wangu, akakataa kwenda kufanya kwa sababu amesema ameokoka na hawezi kufanya kazi sehemu zenye rushwa. Hivyo anamuomba mungu ampe kibali sehemu nyingine ya kazi.