Ombeni Sefue (OS), ombea haya yasikukute na wewe

Nachokiona ni wivu wa kike. Sasa kama Mbowe kasema bila kuleta ushahidi si tunarudi kule kule kwa maneno ya mzee white hair, kama ana ushahidi apeleke mahakamani else anatakiwa ku SHUT UP.
Naona wivu wa kike umeshika hatamu...kwa kutumia wivu wa kike ndugu yetu nae kutumbuliwa
 
kwa umri alio nao 62 ashastaafu utumishi wa umma siku nyingi,aombe rais asimpe kazi. Nyengine apumzike utumishi wa umma.yaishe. Asije
pewa ukatibu tawala Mkoa simiyu.
 
Bwana Sefue unavyoongea na waandishi huku ukichekelea kusema hayo uliyoagizwa (huwa nakuona ukitabasamu),angalia yasikukute kama haya ya OS huyo - labda kama unastaafu kazi kwa umri kesho kutwa![/QUOTE]

yametimia kwani zile mbwembwe zake zote zimeisha leo kwani mkuu kafanya yake na taarifa imetolewa kwa vyombo vya habari
 
Mtoto wa rafiki yangu ni Mwandishi wa habari wa chombo kimoja maarufu hapa Nchini. Baba yake ni kiongozi katika moja ya Taasisi kubwa za umma ambazo hivi sasa zipo katika kipindi kigumu cha kuchunguzwa na hatimaye kufanyiwa marekebishio al maarufu "kutumbuliwa majipu'.

Rafiki yangu ananiambia kila akipigiwa simu na mtoto wake huyo (Mwandishi) huishiwa nguvu maanake anahofu ya kuambiwa "Baba leo tulikuwa Ikulu kumsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi akitueleza maamuzi ya Rais"! Ingawa mtoto hajui, lakini baba mtu hubaki akikosa pumzi mpaka mtoto amalize salaam na kuaga ndipo apumue. Hili linanikumbusha hali ilivyokuwa Miaka ya huko nyuma.

Miaka ya 1990 nikiwa mwajiriwa wa serikali kama Karani katika wizara mojawapo yenye nguvu na kongwe, Serikali hii iliamua kuendesha
zoezi la kupunguza watumishi, maarufu kama 'Redundancy'. Viongozi wakuu walikuwa wakijifungia kwenye vikao vya siri kujadili mwenendo wenyewe na wakitoka huko Mkuu wa Utawala anakuwa amebeba kabrasha lenye maamuzi yote.

Siku zilizofutata Mwangalizi wa Ofisi (au OS yaani - Office Supervisor) alikuwa akiitwa kwa Mkuu wa Ytawala na kupewa kazi ya kusambaza barua kwa watu waliokuwemo katika orodha ya hao walengwa kwa kuwafuata maofisini na kuwakabidhi barua zao. Ama kweli kilikuwa kipindi kigumu, na huyo Bwana OS ilipokuwa akiingia ofisi fulani hali hubadilika kabisa na furaha na vicheko vinavyoendelea hutoweka kama chumvi kwenye maji.

Na huyo OS (ni Marehemu sasa - Mungu amlaze pema huko aliko - sijui?) alikuwa akisha ona utulivu na woga umeshawapata watu, husema kwa sauti ya mamlaka: "E,Ndugu fulani yupo hapa?" Mtume! Macho yote hukodolewa kuelekea kwa mwenzetu mtajwa masikini na kushuhudia anavyosainishwa barua huku akititetemeka kwa simanzi.

Acheni bana, siku hizo ajira serikalini ilikuwa na "security" ya nguvu, uhakika wa maisha. Basi huyo Bw. OS akiondoka huku nyuma huacha watu wakimfariji mwenzao huku wakijiuliza sijui kesho zamu ya nani tena?

Bwana OS aliifanya kazi hii kwa bidii, kwa kujituma na kwa kujiamini kwa vile aliona "mteule mahsusi' hadi akajenga tabia ya kuona ufahari fulani akiingia mahali na kuona watu wanapomwona tu wanatamani kujificha chini ya meza!

Siku ya siku naambiwa Bw.OS alienda kukabidhi Despatch Book kwa Mkuu, na kutoa taarifa kwamba amemaliza kazi ya kuwakabidhi barua walengwa wote. Baada ya kufanya hivyo Mkuu akamwambia "OS, umefanya kazi nzuri, sasa na wewe saini hapa uchukue barua yako!'

Bwana Sefue unavyoongea na waandishi huku ukichekelea kusema hayo uliyoagizwa (huwa nakuona ukitabasamu),angalia yasikukute kama haya ya OS huyo - labda kama unastaafu kazi kwa umri kesho kutwa!

mhhh mkuu unamiaka mingapi? salute! ulichonena kimetimia! MBATATA
 
Shikamoo Jf!

Onyo:
Usichukulie poa kila linaloletwa hapa jamvini, kama umeguswa jiandae kusolve issue yako au anza kujiandaa "kupangiwa kazi nyingine"
C.c
February Marope
Je ni Star Mu Ha! gama
Wafanyakazi wa ofisi ya fedha Open University Dar
 
Shikamoo Jf!

Onyo:
Usichukulie poa kila linaloletwa hapa jamvini, kama umeguswa jiandae kusolve issue yako au anza kujiandaa "kupangiwa kazi nyingine"
C.c
February Marope
Je ni Star Mu Ha! gama
Wafanyakazi wa ofisi ya fedha Open University Dar
tatizo la sisi wabongo nyerere alitupandikiza mbegu mbaya sana ya uwoga. Tunanguvu tu mdomoni. Kwani ukiandika JENISTA MHAGAMA na JANUARY MAKAMBA utanyongwa???
 
Yote tisa na mimi natabiri muda si mrefu cha pombe waziri wa mambo ya undani wa nchi atapigwa chini
 
Back
Top Bottom