Ombeni mtapewa, tafuteni mtapata, bisheni hodi mtafunguliwa ni maneno ya Mungu mwenyewe. Kwanini hujibiwi maombi yako?

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
16,040
21,944
Soma vizuri hasa huko chini kuna ujumbe wako.

Mungu husimamia neno lake. Mungu ni mwaminifu, hadanganyi wala hadanganywi.

Ukiomba kwake usipopata basi usikae kimya ukaanza kusema Mungu hajibu, sijui Mungu hufanya polepole au hata kusema kuwa Mungu hayupo. Muulize Mungu kwanini nimeomba kitu flani kwako mwezi wa pili mwaka jana lakini bado hujajibu? Atakujibu kwanini. Yeye anasema; haya njooni tusemezane…

Watu wengi wanafikiri Mungu ni dikteta, hapana. Mungu ni baba.
Jenga mazoea ya kuongea na Mungu na kujadiliana naye kama unavyofanya na yule umpendaye, utaona naye atafanya hivyo hivyo.

Ukiomba usiwe generalistic. Mfano unaomba eti: Mungu naomba unibariki. Hujafanya ombi hapo na usitegemee jibu kutoka kwa Mungu! Akubariki? Kwenye nini? Baraka ni kitu kipana sana na mtu huwajibika kwa baraka alizopewa, fahamu jambo hilo!

Mungu anataka mtu anaye “ji-comit “ kwake. Ndio maana yeye ni Mungu wa Maagano. Mambo mengi katika Maandiko Matakatifu ni maagano ya Mungu na wanadamu! Kama huna commitment na Mungu you are not serious with him! He too will not be serious with you! Hii ni kanuni ya utendaji ya kimungu, usianze kuhoji. 2+2=4 ni kanuni upende usipende ipo hivyo! Fuata kanuni.

Haja zenu na zijulikane kwa Bwana, Maandiko yanasema hivyo. Kuwa specific katika maombi yako, omba exactly unachotaka bila kumumunya maneno la sivyo maombi yako yatakuwa hayana uhalali mbele ya sheria za kiroho. Maombi mengi ya watu hayajibiwi kwasababu hiyo.

Anza kuwa specific kwenye maombi yako. Usiogope hakuna cha kuficha kwa Mungu! Kama ni hela sema Mungu naomba nijalie nipate milioni 10 hadi ifikapo December 2023. Halafu timiza yote yatakayokupa uhalali wa kumiliki hiyo milioni 10. Jua kwamba Mungu siku zote hubariki kazi ya mtu, yaani kile unachofanya. Kama huna cha kufanya sahau kubarikiwa na Mungu!

Watu wengi hawajibiwi pia ni kwasababu ya vizuizi walivyojiwekea. Dhambi ni kizuizi kikubwa, hivyo kuwa safi kila wakati. Mungu humbariki mtu aliyeko katika mpango wake. Dhambi huleta mashtaka kwa mtu na kwa kuwa Mungu ni mwenye haki basi hapuuzii mashtaka hayo. Hakikisha huna mashtaka yoyote yanayoweza kuwa sababu ya wewe kutojibiwa maombi yako.

Nitaendelea.
 
Mungu ni Roho iliyo ndani yako,ukiomba Mungu nje yako hakuna kitu utapata,Huyo unayemzungumzia wewe ni Mungu wa kizungu! Masharti kibao! Mungu ni Baba anayejua shida zetu,Ni jinsi ya kujitambua tu
 
Back
Top Bottom