Ok Pinda... here is the deal..

Nachukulia haya kama amri kutoka JF, kama mtumishi wenu nitasema! Nitahoji! Nitatoa ushahidi kuwa PM hajasema ukweli wote kuhusu Meremeta! Jumatatu

Huyu Mkuu ndio kwanza katoka Bungeni kakimbia kuja hapa JF kuchangia kwamba ataleta ushahidi Pinda katupeleka peleka tu.

Ni kama anajua kwamba huku JF watu hawataikubali hii stori ya Pinda, na watakuwa wanajiuliza wakina Slaa na Zitto mbona wanamwacha apete?

Kwa hiyo anawahi kuja kutuambia kwamba alikuwepo Bungeni, na aliwasikia wanavyo jaribu kutupeleka peleka, na kwamba hawaaichi. Anaenda kujiandaa.

Anajua tunafikiri nini wanachi, hayuko out of touch. Quite ironic, Mtoto wa Mjini yuko in touch kuliko Mtoto wa Mkulima. Anakumbuka tunamtegemea yeye atutetee mbele ya kina Pilato huko.

Zitto chukua muda wako, kafanye mavitu yako weekend hii, halafu nenda kawaharibie Jumatatu mwanangu.

Kazi njema.
 
Kanuni zitatumika ipasavyo.......... niachie!

Tena inabidi PM afafanue hoja yake aeleweke na kabisa tujue kisheria jeshi linaweza kufanya biashara ya madini nje ya utaratibu wa kisheria....

Tunakuombea Zitto, Mungu awe nawe.
 
hivi pinda hana kweli akili au? maana alipo chaguliwa watu walimsamehe madhambi ya alipokuwa waziri wa serekali za mitaa, na familia ya mwl ikamuunga mkono, na kanisani alikwenda kuombewa na mwisho wana wa ufipa wakamfanyia matambiko yao ya jadi. leo hii anafanya vitu hivi ina maanisha nini kwa hao watu walio muunga mkono?
 
Sierraleone, Liberia, Congo na Angola: Nchi zote hizi zina utajiri wa madini ambao umetajirisha mifuko binafsi ya majenerali wa kijeshi ambao ama walipindua serikali, ama walijitwalia maeneo yenye utajiri wa madini ambao uliwafanya wawe matajiri wa kupindukia (savimbi, foday sankoh, jean pierre bemba, museveni, salim saleh, samuel doe).Inawezekana kabisa jeshi letu limeamua kuiga mtindo huo....

Issue ya Jeshi kumiliki meremeta na kuifanya issue ya usalama wa taifa hiyo ni danganya toto tu ya kuficha wizi na ujambazi unaofanywa na baadhi ya askari kwa kushirikiana na majambazi fulani yaliyokubuhu ndani ya serikali na ccm! Lazima taifa lijulishwe nani ni mmiliki wa meremeta, wanazalisha dhahabu kiasi gani, mapato yanakwenda kwa nani etc etc.

Hatusemi kwamba jeshi letu lisiwe na miradi....i mean kama jeshi wanaweza kufuga kuku na kulima nyanya basi jeshi hilo hilo linaweza kumiliki mgodi wa dhahabu. tofauti hapa ni transparency....uwazi na ukweli wa mapato na matumizi!! we want to know. we deserve to know.
 
SISIEMU wameshaona 2010 kuna harufu mbaya ya kubwagwa vibaya. Sasa wameanza kuingiza sababu za ajabu ajabu, na anayetoa hizo sababu ni Waziri Mkuu. Yaani haiwezi kuingia kichwani kwa watanzania. Wanafikiri wakitaja jeshi basi wananchi watafunga vinywa vyao. Watafanya ujanja wao but these guys need to talk with our VOTES. Kura zetu 2010 lazima tuwasafishe.
Nafikiri JF kwa kushirikiana na taasisi zingine tujaribu kushirikiana na kuhamasisha watanzania kuiondoa hii serikali kwa kutumia KURA zetu.
 
Kanuni zitatumika ipasavyo.......... niachie!
watakusililiza kaka.mi huwa naumia roho sana pale unaposimamia halafu naibu spika anakublust kama mtoto mara zitto kaa chini.na juzi nilisikia sijui ulikuwa unaongelea nini coz niliona kwenye tv .taarifa ya habari chanel 10 ukiwanyamazisha wabunge wa chama cha ccm mana walikuwa wanapiga kelele kama watoto wa chekechea na kuna mmoja aliropo kaa chini wewe mwingine hana ababu huyo.[alkimaanisha huna adabu ]sasa sijui naomba mungu anipe punzi hiyo j3.Laiti wangeonyesha wakati DR Slaa akisoma hotuba ya kambi ya upinzani tungejua kila kitu
 
Kama mtakumbuka niwahi kuhoji swala hili hapa kijiweni JF - kuhusiana na Jeshi kumiliki madini!...
Lakini lilipita kama upepo hadi Pinda kapindisha kweli!...
 
Kama mtakumbuka niwahi kuhoji swala hili hapa kijiweni JF - kuhusiana na Jeshi kumiliki madini!...
Lakini lilipita kama upepo hadi Pinda kapindisha kweli!...

Mzee unajua kuna mambo yamesemwa hapa ambayo kama tungezingatia wala tusingefika mbali namna hii. Kudos kwako kwa kuwa trailblazer!!
 
Kama tuaminivyo waafrika kama ukila kiapo kwa wazee wako wa nyumbani halafu ukakiuka...huwa kutatokea madhara....mie namwonea huruma Pinda....kwa sababu alipokwenda Mpanda aliapa....

04.03.2008
Nikichukua rushwa Mungu anichukue - Pinda

Na Reuben Kagaruki, Mpanda

WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda ameapa kwa wananchi kuwa kamwe hatajihusisha na vitendo vya rushwa kwani kufanya hivyo ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu na viongozi wa aina hiyo wanapaswa kulaaniwa.

Bw. Pinda alitoa kauli hiyo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Usumvye wilayani Mpanda.

Alisema anataka kufanana na kiongozi wa kimila wa Kimasai aitwaye 'Laigwanan' ambaye kwenye kiapo chake wakati wa kupewa wadhifa huo huapa kuwa "Nikikiuka niliyoapa kuyatenda Mungu nilaani, niadhibu na ikibidi nichukue mapema," Bw. Pinda alisema.

Bw. Pinda alisema atakuwa kiongozi wa aina ya Laigwanan na kuwataka wasaidizi wake nao kuiga mfano wa 'Laigwanan.'

Alisema hapendi kuwa Waziri Mkuu kwa kuiangalia nafasi hiyo kwa utamu bali anahitaji kuitekeleza kwa kiapo.......

Huruma jamani....uwiiiiiiiiiiiiii
 
Pamoja na mapungufu yote ya Hayati Mwalimu Julius K Nyerere, chini ya utawala wake tulikuwa angalau na kaheshima. Nakumbuka 1971 tukienda Uingereza tulikuwa watanzania watatu, wakenya wawili na Mganda mmoja na tulipofika uwanja wa ndege Heathrow, kuonyesha tu pasi za Tanzania tuliambiwa piteni wakati wenzetu wa Kenya na Uganda ilibidi wakahojiwe kwa kirefu.

Kwa sasa siyo kuwa tu hatuheshimiwi bali pasi zetu zinaangaliwa mara mbili mbili. Kwa kifupi tunadharauliwa, kushukiwa na kutiliwa shaka hata na majirani zetu. Watu wanashindwa kuelewa kwa nini nchi iliyojaaliwa kila aina ya neema imo kwenye lindi la umasikini kiasi hiki. Ukweli ni kuwa kitendo cha kukubali kundi la hawa mafisadi likishirikiana na wageni kuitafuna nchi na sisi tukiwa tu watazamaji, ni haki mtu yeyote atudharau na hili linaumiza kweli kweli.

Mwalimu alitoa usemi moja ambao lazima sasa tuufanyie kazi kisawasawa. Maneno yalifanana hivi, “kama mtu mwenye akili anakupa wazo(jibu) la kijinga na wewe unatambua kabisa kwamba ni la kijinga halafu unalikubali hilo la kijinga, basi hakuna shaka na wewe ni juha la kutupwa“. (not exact words). Siafiki mimi kuonekana juha, la hasha, no no no. Hawa watu wanatudharau na kwa nini tuendelee kawaachia wazidi kutuzuga ?
 
Mwalimu alitoa usemi moja ambao lazima sasa tuufanyie kazi kisawasawa. Maneno yalifanana hivi, “kama mtu mwenye akili anakupa wazo(jibu) la kijinga na wewe unatambua kabisa kwamba ni la kijinga halafu unalikubali hilo la kijinga, basi hakuna shaka na wewe ni juha la kutupwa“. (not exact words). Siafiki mimi kuonekana juha, la hasha, no no no. Hawa watu wanatudharau na kwa nini tuendelee kawaachia wazidi kutuzuga ?

"kama mtu mwenye akili akikupa wazo la kijinga akijua na wewe una akili nawe ukalikubali (wazo hilo) atakudharau" - Nyerere (Mei Mosi 1995, Mbeya)
 
"kama mtu mwenye akili akikupa wazo la kijinga akijua na wewe una akili nawe ukalikubali (wazo hilo) atakudharau" - Nyerere (Mei Mosi 1995, Mbeya)

samahani nimekukuta hapa sasa nnakuuliza hapa hapa kulikoni kule kwenye radio yetu mbona sikupati samahani kwa kuuliza hapa


naomba unijuilishe leo jumamosi nnata nianze kustarehe
 
Asante kwa kunishtua.. nimeirudisha kwenye automated system.. kutwa nzima ilikuwa inacheza kutoka hapa Studio.. lakini sasa hivi tunafanya upgrade ya mwisho kabla ya kesho.. ila baadaye usiku huu nitakuwa "live" pia...
 
The Meremeta Gold Company
The Governor is the custodian of this ill conceived mining project. He guaranteed this project from the Government for USD 100 million in 1999.

Anna Muganda was a major shareholder and partner who brought in Time Mining to manage and operate the Meremeta Mines on behalf of the Government of Tanzania. She went on to become the wife of Balali in 2004.

The Meremeta Mines was a classic example of Daudi Balali giving Guarantees to companies in which he had an interest, the company thereafter filed bankruptcy and the Bank of Tanzania paid the funds against the Guarantee. Noting the strategic importance of having its own Gold Mine, Bank of Tanzania invested heavily into this mine while the South African partners raised the money andsoldtheir shares after utilizing the funds in the first year of operation.

The Governor, after supporting the loss making operation for 7 years, sold the mining rights to Rand Gold, making the Government mine
unsustainable.

The loss to Government of Tanzania is USD 132 million paid to the lenders against the Guarantee from BOT with interest and penalties.
The Governor made payments in October 2005 before the end of Third Phase Government.

He sold the mining rights to RAND Gold for below market prices causing a further loss of USD 100 million. Total loss to Government of USD 232 million
__________________
We Study More About Less and Less Until we learn something about NOTHING.
 
Mzee Mwanakijiji nitakuwa na wewe katika sala hii ya kuwapa laana,
Mungu naomba uwe upande wetu ili hawa mafisadi wahukumiwe hapa hapa duniani
Eeh Mungu,angalia Pinda anvyopindisha mambo na kutufanya siye wapuuzi na wajinga
Eeh baba sikia maombi yetu na naomba uyajibu kwa siku hizi mbili tu.

Na kwa kuwa wameamua kutufanya wapuuzi na mazezeta tusiyo na msikio na akili
Na kwa kuwa wanatamani watukamate ili watuue kabisa na kutoa macho
Na kwa kuwa Nasimamia katika haki na sina namba 666 kwenye paji la suo wangu
Nina Imani ya kuwa Pesa za Meremeta Zitarudishwa na tutashinda.

Enyi vingozi mlio na roho ya udanganyifu na waongo wa kutupwa msio na aibu,
Nawaandikieni nikiwaomba tutumie siku hizi mbili kwa ajili ya haya tu yafuatyo
Kwanza Muachie Ngazi kwa kosa la kupitisha Bajeti ya kutuning'iniza siye makini
Pili Naomba mjiunge nasi na kuanza kudai haki yetu kama Wanajamii makini

Najua wanaona Tunawakera,ila Naamini nyie mtakekerekaa zaidi wakati si mwingi
Ninajua wiki inaio kuja itakuwa ni wiki mbaya sana kwenu na familia zenu zakifisadi
Nimepata Ujumbe wenu na niko tayari tena na nasisitiza niko tayari kwa lolote
Ila La msingi mjue Siko tayari kukubali kumezeshwa matapishi kwa kuogopa kufa.

Najua Mnasifika kwa uchawi na mambo mabaya,ila Mungu ninaye muamini hawapendi
Mmejipalia makaa,Mmelewa Mvinyo wa madaraka,Mmekuwa wahuni,mmekuwa wa ovyo
siwapendi kamwe,na sitawapenda milele kwa kuwa nyie si wana wa Mungu
Hatma ya Tanzania kwa uongozi huu,nawaonea huruma wajukuu zangu huko mbeleni

kwi kwi kwi kwi

Do we really Need Pinda?



Ngoja niongezee kidogo,
Nakumbuka Mkesha wa mwaka mpya (2008) kulikuwa na kongamano la kidini kubwa sana pale uwanja wa taifa na ajenda kubwa ilikuwa kuiombea Tanzania, na mimi nilikuwepo pale na nilifarijika sana, naamini maombi yale sasa yanafanya kazi, kwa kuwa kadri mafisadi wanavyojichanganya ndio wananchi wanazidi kupata hasira dhidi yao

Na sasa nitamke yafuatayo,

Kuanzia leo nimeamini Pinda nae ni fisadi na ni kiongozi dhaifu
Sasa hivi unakuja mvurugano wa hali ya juu nchini kwetu na baada ya hapo neema itafuatia na tutakuwa na serikali mpya na CCM itazikwa kabisa (hata mmea ili uote ni lazima mbegu ioze kwanza kisha inatoa mmea mpya)

Nimalizie kwa sara,

Ewe MUNGU muumba mbingu na nchi, tunaomba utusaidie sisi masikini wa Tanzania,
Sisi ambao Mafisadi wakishiba tunaambulia makombo
Sisi ambao tumewapa dhamana ya kutuongoza ila tumegeuzwa mazezeta

Tunakuomba uwafahamishe kwamba na sisi ni viumbe watu kama wao na wala sisi sio mbwa
Tunakuomba uwashushie nguvu yako na uwabadilishe kiburi chao kwa nguvu yako kisha uyaweke wazi mambo yao ya kisirisiri na kiwiziwizi ambao unasababisha watanzania wengi wanakufa kila siku kwa magojwa ambayo yanatibika ili hali wao wamefisadi pesa zetu za madawa

Ee Mungu baba ibadili Tanzania,
 
Ngoja niongezee kidogo,
Nakumbuka Mkesha wa mwaka mpya (2008) kulikuwa na kongamano la kidini kubwa sana pale uwanja wa taifa na ajenda kubwa ilikuwa kuiombea Tanzania, na mimi nilikuwepo pale na nilifarijika sana, naamini maombi yale sasa yanafanya kazi, kwa kuwa kadri mafisadi wanavyojichanganya ndio wananchi wanazidi kupata hasira dhidi yao

Na sasa nitamke yafuatayo,

Kuanzia leo nimeamini Pinda nae ni fisadi na ni kiongozi dhaifu
Sasa hivi unakuja mvurugano wa hali ya juu nchini kwetu na baada ya hapo neema itafuatia na tutakuwa na serikali mpya na CCM itazikwa kabisa (hata mmea ili uote ni lazima mbegu ioze kwanza kisha inatoa mmea mpya)

Nimalizie kwa sara,

Ewe MUNGU muumba mbingu na nchi, tunaomba utusaidie sisi masikini wa Tanzania,
Sisi ambao Mafisadi wakishiba tunaambulia makombo
Sisi ambao tumewapa dhamana ya kutuongoza ila tumegeuzwa mazezeta

Tunakuomba uwafahamishe kwamba na sisi ni viumbe watu kama wao na wala sisi sio mbwa
Tunakuomba uwashushie nguvu yako na uwabadilishe kiburi chao kwa nguvu yako kisha uyaweke wazi mambo yao wa kisirisiri na kiwiziwizi ambao unasababisha watanzania wengi wanakufa kila siku kwa magojwa ambayo yanatibika ili hali wao wamefisadi pesa zetu za madawa

Ee Mungu baba ibadili Tanzania,

Amina! Amina! Mungu tubariki Watanzania na utupatie nguvu ya kulikomboa Taifa letu kutoka mikononi mwa Mafisadi.
 
Amina! Amina! Mungu tubariki Watanzania na utupatie nguvu ya kulikomboa Taifa letu kutoka mikononi mwa Mafisadi.

Ama kweli FREEDOM IS AROUND THE CORNER!
Unajua niliwashtua viongozi wetu kuwa...Ni kweli viongozi wa dini zote walivyosema kuwa KIKWETE NI MPANGO WA MUNGU!

Mfano wa AYUBU..Ambao niliutoa hapa JAMVINI na Samuel SITTA kuurudia...Umenipa matumaini na UHAKIKA KUWA...AFRICA IS NOT CURSED BUT BLESSED!
ITS GODS TIME AND NOBODY CAN CHANGE THAT!
GOD WILLING...WE WILL BE VICTORIOUS!
 
Back
Top Bottom