Wordsworth
JF-Expert Member
- Jan 14, 2019
- 1,190
- 3,359
Hakuna ofisi maalum ya madereva wa serikali (wakiwemo wa halmashauri na wizara mbalimbali) kutumia wakati wanasubiri mabosi wao watoke ofisini au kwenye mikutano ya kujenga taifa?
Naona kama wanachoka sana, wengine utawakuta wanawasubiri mabosi wakiwa wamejibanza kwenye vibanda vya karibu vya mama ntilie na hata wale ambao hawajapangiwa magari baadhi yao wapo vijiweni, wengine wanajibanza kwenye maduka ya mangi wanapiga Kvant za kutosha. Baadae tunapishana nao barabarani wanaendesha magari ya serikali kama madereva bodaboda.
Sheria za kazi za watumishi wa umma zinawahusu? Hasa hao wa halmashauri ambao hawajapangiwa magari wawe katika ofisi gani muda wa kazi? Ni aibu.
Serikali ina mpango gani wa kuwa na ofisi za hawa madereva kukaa wakati wa muda wa kazi?