Nyumba za National Housing (NHC) Dar zinapatikanaje?

Wanajukwaa Habari,

Naomba kuwekwa wazi hivi hizi nyumba za NHC kwa Hapa Dar zinapatikanaje? au wanaoishi hiz nyumba wameshazinunua au hawahami?,? Mwenye experience kidogo please
Kupata nyumba hizo unanunua haki ya upangaji kwa million 10 mpaka na zaidi inategemea iko wapi.

Hakuna mtu anarudishaga hizo nyumba, kuna watu wanalipa kodi na hawakai mtu yupo nje ya nchi friji iko on inawekwa luku tu na kufanyiwa usafi lakini hakai mtu.
 
Wanajukwaa Habari,

Naomba kuwekwa wazi hivi hizi nyumba za NHC kwa Hapa Dar zinapatikanaje? au wanaoishi hiz nyumba wameshazinunua au hawahami?,? Mwenye experience kidogo please
Hizo nyumba nenda Samora tower ulizia makao makuu ya NHC utaoneshwa pale. Kuna kikengo kiko karibu na Samora avenue ndio wapo humo kuna form utapewa. Utalipa elfu kama 4 hivi kupitia control number. Then utapewa form ukaijaze, hani personal details, tin number, family status na unapendekeza nyumba ikipatikana iwe maeneo gani na bajeti yako ikoje.

Hizi nyumba kupata sio ishu sana ila uwe na mkono mrefu kidogo. Wahindi mbona wanazilipia kila siku na hawang'oki mule.
 
Kupata nyumba hizo unanunuwa haki ya upangaji kwa million 10 mpaka na zaidi inategemea iko wapi.

Hakuna mtu anarudishaga hizo nyumba, kuna watu wanalipa kodi na hawakai mtu yupo njenya nchi friji iko on inawekwa luku tu na kufanyiwa usafi lakini hakai mtum
Kwa Tafsiri hio Hizi za zamani zote zipo covered, miradi mipya ndio ambayo inawezekana kupatikana.
 
Hizo nyumba nenda samora tower ulizia makao makuu ya NHC utaoneshwa pale. Kuja kikengo kiko karibu na samora avenue ndo wapo humo kuja form utapewa. Utalipa elfu kama 4 hiv kupitia control number . Then utapewa form ukaijaze, hani personal details, tin number, family status na unapendekeza nyumba ikipatikana iwe maeneo gan na bajeti yako ikoje

Hizi nyumba kupata sio ishu sana ila uwe na mkono mrefu kidogo. Wahindi mbona wanazilipia kila siku na hawang'oki mule
Samora Tower posta, Siku nitasogea hapo,
Huo mkono mrefu ndio shida hapo
 
Nina Miaka 5 nafatilia niweke Jamaa zangu, nimetumia Hadi njia ya Hela ila siyo Rahisi kiivyo
Hela pale apewi mtu yoyote. Kuna jamaa mmoja mwaka jana hizo form mimi nilizifata pale akajaza kaweka picha na unazipeleka kwa wakili. Mwaka jana huohuo kapata Posta pale nyuma ya JNICC ndo anaishi. Yeye aliomba Posta au Masaki na bajet aliweka 800k monthly.
 
Kwa Tafsir hio Hizi za zamani zote zipo covered, miradi mipya ndio ambayo inawezekana kupatikana.
Miradi mipya aliharibu Msechu kwa kujifanya msomi kumbe mpumbavu tu.
Kajenga appartment Morroco eti kununua bei yake million 400, kama siyo chizi huyu umuitaje?

Mtu mwenye million 400 huwezi kumuuzia appartment wakati ana uwezo wa kumiliki nyumba.
 
Hizo nyumba nenda samora tower ulizia makao makuu ya NHC utaoneshwa pale. Kuja kikengo kiko karibu na samora avenue ndo wapo humo kuja form utapewa. Utalipa elfu kama 4 hiv kupitia control number . Then utapewa form ukaijaze, hani personal details, tin number, family status na unapendekeza nyumba ikipatikana iwe maeneo gan na bajeti yako ikoje

Hizi nyumba kupata sio ishu sana ila uwe na mkono mrefu kidogo. Wahindi mbona wanazilipia kila siku na hawang'oki mu

Hela pale apewi mtu yoyote. Kuna jamaa mmoja mwaka jana hizo form mm nilizifata pale akajaza kaweka picha na unazipeleka kwq wakili. Mwaka jana huohuo kapata posta pale nyuma ya jnicc ndo anaishi. Yeye aliomba posta au masaki na bajet aliweka 800k monthly
Yeye pia alitunua mkono wa Mtu ?, au kwamba bajeti yake ndio ilishawishi?
 
Hela pale apewi mtu yoyote. Kuna jamaa mmoja mwaka jana hizo form mm nilizifata pale akajaza kaweka picha na unazipeleka kwq wakili. Mwaka jana huohuo kapata posta pale nyuma ya jnicc ndo anaishi. Yeye aliomba posta au masaki na bajet aliweka 800k monthly
Ndo uelewe tu kuna Namna alirefusha Mkono
 
Wanajukwaa Habari,

Naomba kuwekwa wazi hivi hizi nyumba za NHC kwa Hapa Dar zinapatikanaje? au wanaoishi hiz nyumba wameshazinunua au hawahami?,? Mwenye experience kidogo please
Unanikumbusha kuna Aunt mmoja alikaa nje miaka mingi, akawa anarudi Tanzania anataka nyumba za NHC.

Akauliza kwa sauti "Pale NHC namjua nani pale?" Akajijibu "Aaah, namjua Mkurugenzi Mkuu".

Kwa Tanzania hiyo ndiyo process ya kupata nyumba.

Watu wanauliza unamjua nani, hawaulizi mchakato.
 
Hivyo wewe Tayar unamjua mtu uwe mkono wangu.?😀
 
Soko la "real estate" Tanzania bado sana, kupata nyumba NHC kama ni mtanzania wa kawaida ni ngumu sana kwasababu wenye pesa wanakabia kwa pesa. Na wanaojenga ni wa aina hiyo hiyo.

Kila anaejenga Tanzania analenga matajiri ila mapinduzi ya real estate yanahitajika Tanzania. kila anaejenga anawaza mamilioni.
 
Back
Top Bottom