Kwa kila mwanasiasa wa Tanzania anaetaka kuungwa mkono na wananchi wengi amekuwa akijitahidi kujionesha kuwa ni mfuasi wa Rais wa kwanza wa Tzania Mwl Nyerere. Anasifiwa kwa kila kitu lakini kwangu mimi simkubali kabisa Mwl Nyerere. Siamini kama alikuwa na kipaji cha uongozi. Alikuwa ni dikteta. Alifinya uhuru wa habari, aliwafunga wapinzani wake, alileta umasikini mkubwa kwa taifa na wananchi wa Tzania. Si kwamba alikuwa anapendwa bali alikuwa anaongoza wananchi wengi wasiojua dunia inakwendaje"wajinga".
Huyo ndio Nyerere. Kwa miwani yangu namuona kuwa ana mabaya mengi kuliko mazuri kama tunavyolazimishwa kuamini. Kutojilimbikizia mali au kutoa huduma za jamii bure si kigezo cha kutokuwa dikteta maana hata Pinnochet, Hitler na Mussolin walikuwa wanatoa huduma za jamii bora na bure kabisa kwa watu wao.
Nimesikitishwa na hoja mfu ambayo mtu aliyeanzisha mada hii ametoa. Kusema Nyerere hakufanya mambo ya maana katika nchi yetu ni matusi kwa wale ambao wanaelewa nchi yetu ilikuwa wapi na nini kilisababisha uchumi wetu kudorora mwaka 1979-hadi miaka ya tisini. Niliona upungufu mkubwa wa uelewa wa historia ya nchi yetu pale tulipokuwa tukijadili uamuzi wa Mwalimu kuitambua Biafra na kwa kweli wale ambao wanapima maendeleo kwa wingi wa vitu ambavyo wachache wanavyo na si jinsi ambavyo wengi wanavyo.
Je, ni nani asiyefahamu kuwa hadi mwaka 1978 nchi yetu ilikuwa na uchumi mzuri sana hadi IMF walidai kuwa Tanzania lazima itumie akiba yake ya nje na ibakie isiyozidi miezi sita hapo mwaka 1977? Najua mbumbumbu wanaotoa hoja mfu humu ndani watakuwa hawajui hilo. Je, ni nani asiyejua kuwa nchi yetu ililazimika kutumia dola milioni moja kila siku katika vita ya Uganda na kuwa vita hiyo ndiyo iliyofilisi nchi yetu? Mbumbumbu wa historia na uchumi watang'aka kama watu waliofumwa ugoni? Je, ni nani asiyejua kuwa mnamo mwaka 1979-80 bei ya mafuta ilipanda sana duniani na nchi yetu ambayo tayari ilikuwa imefilisika kwa vita haikuwa na fedha za kuweza kuendesha uchumi wake? Mazezeta wa historia na uchumi hilo halipo vichwani mwao kwani hawajui na wala hawajawahi kujishughulisha kujua hilo?
Je, ni nani asiyejua mataifa yanayotoka katika vita na ambayo uchumi wake umeyumbishwa navyo yanahitaji msaada/mikopo kutegemeza chumi zao? Watoa majibu ya kijiweni hawajui hilo kwani hawajawahi kujiuliza kuwa historia ya dunia imeonyesha hivyo kwani hata mataifa ya Ulaya yalipata msaada huo kutoka kwa Marekani katika Mpango wa Marshal. Na suala la mgawo na foleni za chakula na bidhaa baada ya vita je wamewahi kujiuliza kuwa Waingereza walikaa katika mgawo kwa miaka saba na siku waliporuhusiwa kula mayai mawili ni siku ambapo Malkia Elizabeth alisimikwa?
Ninaweza kuendelea kuuliza maswali mengi cha muhimu ni kusema kuwa Mwalimu alikuwa na makosa aliyoyafanya lakini huwezi ukaniambia kuwa eti aliporomosha uchumi kwa siasa za Ujamaa bali kukataa kwake masharti ya kijinga ya IMF na Benki ya Dunia yaliyodai eti serikali yake ilikuwa imeshindwa kuendesha uchumi vizuri ni uongo mtupu. Nilikuwepo wakati ule na nilipanga foleni ya sukari, sabuni na vitu vingine na kwa kweli kama kuna wakati serikali iliwahi kutoa sababu za ukweli kuhusiana hali ya uchumi ni wakati ule. Kama mtu aliyepata nafasi ya kusoma si tu sheria bali uchumi na siasa za taasisi za kimataifa za pesa ninathibitisha kuwa hali mbaya ya uchumi ilichangiwa kwa sehemu kubwa na sababu za nje na si za ndani. Kwa bahati mbaya watu wenye kupenda majibu mepesi na kwa kweli ya kijiweni ndio wako mstari wa mbele kupotosha ukweli na kutaka kutufanya kuwa sisi tu mazezeta wasio na uwezo wa kuchambua mambo. Chuki zao kwa Mwalimu kwa kweli huwezi ukazieleza vizuri kwani mtu ambaye alidiriki hata kutaifisha taasisi za kidini na kuzifanya za watu wote hivi sasa anaonekana kuwa alikuwa na ajenda ya kupendelea watu wa madhehebu fulani? Hivi hii kweli inaingia akilini?
Ninamalizia kusema kuwa maamuzi ya Mwalimu mengi yalilenga ustawi wa watu na si wa kutaka kujinufaisha na kama alikuwa mtu aliyependa watu wasisome je si huyu aliyetaifisha shule ili watu wa dini na makabila yote wasome? Je si huyu aliyeanzisha elimu ya watu wazima na kusababisha kiwango cha kujua kusoma na kuandika kupanda na kuwa asilimia 95? Si huyu aliyejenga miundo mbinu kama Tazara na viwanda vingi ambavyo mafisadi wamevigawa bure? Si huyu aliyeweza kushinda mbinu za benki za nje kuua NBC pale ilipotaifishwa? Si huyu ambaye hakutumia madaraka yake ya uraisi kujitarisha na hata watoto wake hali zake ni zinakaribia za Watanzania wengine.
Inanisikitisha sana kuona haya yote lakini watu wenye ajenda ovu ndivyo walivyo na hawatachoka kupotosha historia ili nia zao ovu zifanikiwe. Napenda kusema kuwa watashindwa kwani wale wenye uelewa mzuri wa mambo tutasimama imara kupangua hoja zao mfu.
Acheni kutuchanganya, mema aliyoyafanya Nyerere yanajishuhudia hadi leo ingawa mapungufu pia hayakosekani.Kuna kitu kinaitwa "programmed mind" watu wengi wanakariri kwamba nyerere ni kiongozi mzuri si kweli
Pamoja na hayo uliyoysema pia alikuwa haambiliki japo hana maarifa (mjinga) ameshauriwa sana kuhusu uchumi lakini akawa sideline wapinzani wa mawazo yake.
Alipoondoka nchi ilikuwa taabani kiuchumi, na wananchi walikuwa hohehahe (nguo viraka, sabuni hakuna wala sukari acha bei zake)
Alikuwa mchoy na mnafiki..kila mwenye hela kwake ni mwizi..
Aliwadhulumu watu wengi mashamba na majumba yao ambayo wengi wao wamenunua na kujenga kwa mikopo..
Mtu anayejitambulisha na kumsifia nyerere ana maradhi makubwa.
Kwanza sehemu ya kwanza ya hoja yako haina ukweli; ni wapi Nyerere "anasifiwa kwa kila kitu?"
Pili tuangalia hoja zako ambazo umeziweka kiujumla na bila ya shaka wapo wanaoamini kama unavyoamini: Ili hoja zako ziwe na ukweli ni lazima zipimwe na ukweli wa historia na vile vile kutafuta sehemu nyingine ya kulinganishia. Unasema Nyerere:
Alifinya uhuru wa habari - Kwa vipi? Sheria ya Magazeti ya 1976 (ya wakati wa Nyerere) bado ipo; Sheria ya Usalama wa Taifa ya 1970 bado zipo na zinatumika sasa ni nani aliyefungua uhuru wa vyombo vya habari kuliko aliyehakikisha sheria ipo ya kufungua? Lakini unafikiri ni kweli upo uhuru wa habari kulinganisha na wakati wa Nyerere?
aliwafunga wapinzani wake - Ni mpinzani gani wa Nyerere aliyefungwa kwa kumpinga Nyerere na ili hoja iwe na nguvu ni vizuri kuonesha ni nani aliyefungwa bila ya kutumia sheria zilizokuwepo?
alileta umasikini mkubwa kwa taifa na wananchi wa Tzania. - Kabla ya Nyerere "kuuleta" umaskini, Tanzania ilikuwa na utajiri gani ambao ulipotea? Unataka tuamini kuwa wakati wa Mkoloni Tanzania ilikuwa ni tajiri na Watanzania walikuwa na unafuu zaidi kuliko wakati wa Nyerere? Hapa inabidi ulete figure na hali ya watu wa wakati huo.
Sasa hiyo sehemu moja; sehemu ya pili unalinganisha utawala wa Nyerere na utawala wa nchi gani nyingine iliyofanana na ya kwetu ili tuweze kupima na kusema kuwa "wao" walipiga hatua kubwa ya maendeleo kwa sababu viongozi wao walifanya kinyume kabisa na alichofanya/kilichofanyika wakati wa Mwalimu.
Hivi ni mapungufu gani aliyoyafanya Nyerere kama binadamu?, hebu tupeni basi hayo mapungufu tuyapime, huenda ndio hayo Wanaompinga wanaona kwamba ni mistakes kubwa sana zilizopelekea sisi kuwa hapa tulipo.
Angejenga mfumo bora wa uongoz kwa kuwezesha uundaji wa katiba inayokidhi maslah ya uma hapo ningemkubali, vingine vyote havina uzito kama katiba, sasa sifa za nini.
kushindwa kwa waliomfuatia hakumaanishi kwamba yeye alipatia.tangu alipoondoka miaka zaidi ya ishirini na tano iliyopita hao walioko madarakani wameshindwa nini kuandika Katiba Mpya? Mlitaka hadi awaandae watoto wake kumrithi ndio mngejua amewaandalia vizuri?
Unaonyesha dhahiri umetumwa. Nyerere ndie aliesababisha madudu kama haya ya Dowans? Mmetoa ahadi kede kede zisizotekelezeka, sasa mnamtafuta mchawi. Wacha kutupotezea, tunataka suluhisho la matatizo yaliyopo sasa, umeme, elimu kushuka viwangob uchumi mbovu n.k. Mtaendelea kulia Nyerere kaleta matatizo mpaka lini? Robo karne imekwisha tangu Nyerere aondoke madarakani. Time to deliver, wacha porojo.
Kwa kila mwanasiasa wa Tanzania anaetaka kuungwa mkono na wananchi wengi amekuwa akijitahidi kujionesha kuwa ni mfuasi wa Rais wa kwanza wa Tzania Mwl Nyerere. Anasifiwa kwa kila kitu lakini kwangu mimi simkubali kabisa Mwl Nyerere. Siamini kama alikuwa na kipaji cha uongozi. Alikuwa ni dikteta. Alifinya uhuru wa habari, aliwafunga wapinzani wake, alileta umasikini mkubwa kwa taifa na wananchi wa Tzania. Si kwamba alikuwa anapendwa bali alikuwa anaongoza wananchi wengi wasiojua dunia inakwendaje"wajinga".
Huyo ndio Nyerere. Kwa miwani yangu namuona kuwa ana mabaya mengi kuliko mazuri kama tunavyolazimishwa kuamini. Kutojilimbikizia mali au kutoa huduma za jamii bure si kigezo cha kutokuwa dikteta maana hata Pinnochet, Hitler na Mussolin walikuwa wanatoa huduma za jamii bora na bure kabisa kwa watu wao.
kushindwa kwa waliomfuatia hakumaanishi kwamba yeye alipatia.
ni kwa nini aliabolish vyama vingi vya siasa katika kipindi chake?
MM achana naye! Kuna watu hapa sijui wamesomea choo gani! Usi-argue nayenani alikuambia aliabolish?
Mwalimu alishasema viongozi na serikali si malaika, yapo mapungufu yaachwe na mazuri yachukuliwe na serikali zinazofuata.
Kabla ya kumpongeza au kumlaumu Mwalimu kuna mambo ya msingi kuangalia. Mwalimu alichukua nchi ikiwa katika hali gani hasa upande wa viongozi na elimu zao? Mwalimu alifanya nini baada ya hapo, na alituachia nini alipoondoka.
Winston Churchill ni PM wa Uk anayekumbukwa sana na mwenye heshima sana UK na duniani kote. Hata baada ya kuiongoza Uingereza kuepeuka aibu kubwa mbele ya Mjerumani, bado alishindwa uchaguzi uliofuata. Lakini mapungufu yake ya kiutawala hayajaondoa heshima yake ndani ya Taifa lake.
Mwl alichukua nchi kukiwa hakuna wasomi na wananchi wakiwa mbumbu kabisa kama alivyosema mmoja wetu humu. Ni kwa kutumia uadilifu na uzoefu nchi ikaanza kutambaa na hatimaye kusimama. Ushahidi kwa sisi tulioona kwa macho yetu, form vi walikuwa wanapangiwa kazi (sio kutafuta) kuziba pengo la wasomi. Ni wakati huo Mwl alikuwa anaomba Scholarship kwa nchi marafiki na zilitolewa kwa mtu mwenye sifa na si kwa kabila au dini. Haya yote yakiendelea Mwl alikuwa anajenga Chuo kikuu ambacho leo asilimia 90 ya wasomi wamepitia hapo.
Elimu wakati wa Mwl ilihakikisha kuwa hata mtoto wa masikini alipata Warrant ya kwenda shule. Leo tuna maprofesa waliotoka kwenye kuokota maembe na kuchunga ng'ombe na sasa wanalisaidia taifa.
Upande wa Afya, Mwl alijenga vituo vya Afya, Hospitali za mikoa na Wilaya. Leo tembelea vituo vya Afya kama Magomeni, Mnazi mmoja au Temeke uone nani aliweka jiwe la msingi au kufungua. Kote nchini utaona majina kama Mustafa Songambele, Kawawa, Nyerere, Karume, Mwakawago, n.k
Mwl alikuta umeme wa Pangani, akajenga Nyumba ya mungu, Mtera, Kidatu, na hata kuvusha kwenda Zanzibar. Ni mabwawa hayo ambayo leo tumeshindwa kujenga mengine kama si kulinda maji na vyanzo vyake.
Mwl akaona njia ya kuinua uchumi wa nchi si kwenda kuomba misaada ya kuletewa mitumba, akajenga viwanda kama Mwatex, Mutex, Urafiki, Tanganyika Packers, Bora, UFI, Kilitex n.k. Kwa wale tuliokuwapo enzi hizo kulikuwa na Shift za kazi, Asubuhi, mchana na usiku. Tulitumia bidhaa zetu wenyewe na malighafi zetu. Leo tunauza ng'ombe Uarabuni ili tuagize nyama za makopo Brazil na South. Tunanunua nguo hafifiu za kichina na hatusafirishi tena vitenge vya urafiki.
Wakati tulipokuwa na janga la njaa nchi nzima, Mwl alihakikisha kuwa huo unga wa yanga au bulga unamfikia mtu wa mwisho kijijini. Si kweli kuwa alizuia watu wasihifadhi chakula.
Vyuo vyote vya ufundi, uganga na kilimo vilijengwa wakati wa mwalimu, leo tumeviua vyote kwasababu hatuna pesa za kuvihudumia na kule vijini wana lima kama wajuavyo, wanajitibu kwa Tetracyline kwa maana hakuna wataalamu, bado tunawadangaya na kilimo kwanza
Mwl akatuachia TAZARA, moja ya infrastructure kubwa barani , leo mahindi yanaoza Sumbawanga kwasababu reli haifanyi kazi.
Akajenga reli ya Segera Ruvu, na kuiendeleza ya kati hata baada ya kufa kwa EAC. Pamoja na yote hayo tumeshindwa kuweka mafuta kwenye mabehewa na leo tunaomba ''visa'' kwenda Mwanza au Bukoba.
Hayo ni machache tu mazuri ya Mwl ambayo huwezi kuyafananisha na awamu yoyote kwasababu mwalimu alianza na msingi, sasa hawa wa sasa hata kurepea paa hawawezi.
Mapungufu ya Mwl ni pamoja na kutaifisha mashamba ya mkonge na kuyaacha mapori. Ni pamoja na kutofanya marekebisho ya uchumi mapema kabisa, kuua vyama vya ushirika na kuingiza siasa hata katika utaalamu kwa uchache tu.
Kama tutaangalia uwepo wa TV kama kigezo cha maendeleo basi hatutamtendea Mwl haki.Kipaumbele cha Mwl hakikuwa TV, na sijui TV inmsaidiaje mtoto kwenda shule kama hana karo. Mimi nimeishi zama za Mwl nakuhakikishia kuwa tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Lakini sifa moja ambayo watu hawaisemi ni kujenga taifa lenye watu waadilifu,kama mwl angekuwa kama hawa wa leo, angeweza kuuza hata mkoa mmoja na tusingejua. Madini aliyoacha si ndiyo yanasaniwa mikataba mahotelini uingereza!!
Kimataifa mwl alikubalika sana, soma Declassified information ya CIA kuhusu Mwl. Wao wanasema kama kuna kiongozi waliyemuogopa alikuwa ni Mwl, na walisema endapo ujamaa ungefanikiwa basi Afrika ingekuwa sio wanayoitaka, na walihakikisha hilo halitokei. Haya si maneno yangu tafadhali!!
Namalizia kwa kusema, Mwl kama mwanadamu ana mapungufu yake, lakini kwa ugumu na changamoto zilizomkabili, matokeo ya kazi yake hatutayafananisha na mwingine aliyefuata. Maendeleo ya miaka 24 ni makubwa kuliko yale ya Mwinyi/Mkapa/ JK. Tuliokuwepo zama hizo hatuhitaji kusimuliwa.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Hapo kwenye red hebu tupe ushahidi, sio porojoNyerere ana mazuri yake aliyofanya lakini tunakosea sana tunapokuwa tunasema nyerere hakuwa na kosa na kila alichofanya tunasema kidumu...hata kama kina mapungufu makubwa. Nyerere alikuwa msomi na akaja na mfumo wa Ujamaa na kujitegemea lakini cha kushangaza leo hii hakuna hata kijiji kimoja cha ujamaa ambacho kimebaki kama mfano ili tuseme hili lilikuwa wazo zuri la msomi nyerere.
Watu walitupa chumvi na sukari baharini,wakafukia ela zao chini . Ushindani haukuendekezwa na kama mtu/sehemu flani itaonekana inaendelea itawekewa mikakati ya kusimamishwa ili isubiri kwingine .Haikuwa sahihi.Kimsingi mikakati yote ndio imeleta taifa la watu waoga hata kudai maslai yao ya msingi ni tatizo kubwa.
Chaguzi za kipindi kile zilikuwa kati ya Nyerere na kivuli.Tujiulize kweli hadi mwaka 80 Tanzania mtu agressive alikuwa nyerere pekee?
Alikuwa mwanasiasa mzuri lakini alikuwa anakosea sana kukataa mawazo ya wataalamu.Wachumi walimshauri vizuri jinsi ya kuhundle mashirika ya umma lakini akakataa kabisa ,wataalamu wakaishia kukimbia nchi.