Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete waliwahi kuvaa Magwanda ya JWTZ walipokuwa Marais?

Jiwe alikuwa ni Jiwe haswa alipaswa kuvaa combat. Amiri Jeshi Mkuu anatakiwa kuvaa combat. Ambao hawakuvaa ndio "malimbukeni"

Namkumbuka sana Jiwe. Rais anatakiwa kuwa kichaa kichaa tu asiyetabirika leo ataongea nini. Sio Rais mnajua kabisa kila siku speech zake ni kulia lia tu kama wananchi wake

Jiwe ilibaki kidogo tu angeendelea kuwa hai kuna siku angemwambia mtu Kmmk mbele ya camera
Basi Nenda
 
Usitake kusema "watu wote" kama vile ushafanya sensa ya kujua ni wangapi wanaona ni Sawa au wangapi wanaona si sawa raia kuvaa nguo za jeshi.

Rais ni raia tu kama Mimi na wewe na si mwanajeshi. Inakuwaje avae sare za jeshi?

Ni Raia Namba Moja basi tufanye kuwa Raia namba moja kumempa privilege ya kuvaa uniform za Jeshi kwenye tukio la kijeshi

Wewe ni Raia wa milion 43 Ni marufuku kuvaa uniform za Jeshi hata ukiwa ndani kwako
 
Nyerere aliwahi kuvaa magwanda ya mgambo wakati wa Vita vya Kagera.

Ila Nyerere ni "War President" . Ali mobikize majeshi wakati wa vita hivyo huyo kidogo ana rationale ya kuvaa nguo za kijeshi kwa muktadha huo.

Wengine wote ni kick.

Wanatakiwa kujua kanuni ya "Civilian Control of the Military".
Jibu nzuri sana mkuu 👏
 
Elimu ya uraia uliyodai sinayo,ni ya nchi gani?..maana huku kwetu Marais wanne walivaa sare za jeshi,rais wa china,France na urusi walivaa,hiyo elimu ya uraia inapatikana darasa la ngapi ambalo wengine hatukufanikiwa kufika?
We akili ndogo kawekeze tu kwenye Mapuya ukishavaa migombamigomba basi unajiona uko juu ya Nchi
 
We akili ndogo kawekeze tu kwenye Mapuya ukishavaa migombamigomba basi unajiona uko juu ya Nchi
Wenyewe badala ya.kujadili hoja wamekaza shingo wakidhani wanatetea "chama chao" kumbe wanaonekana hawana walijualo.

hp4510 anadai kwa kuwa Rais in "raia namba moja" basi hiyo tu inampa haki ya kuvaa mavazi ya JWTZ.
Sidhani kama hata kama anajua kwa nini Rais anaitwa raia namba moja. Nadhani kwake yeye Rais kuitwa raia namba moja anaona Rais kawa juu ya watanzania wote.
 
Mwl. Nyerere sio tu alivaa bakabaka bali alivaa hadi mavazi ya mgambo.
 
Hebu weka picha Mwalimu Nyerere akiwa amevaa nguo za JWTZ tena zikiwa na vyeo visivyokuwepo kwenye Jeshi.

Mwalimu hakuvaa nguo za Mgambo Bali alivaa Khaki nguo zinazojulikana Dunia nzima kuwa ni nguo za "field".
Uwe unafuatilia mambo. Mwl. Nyerer alivaa sare za JWTZ na mgambo sio khaki kama unavyosema yaani awe katikati ya jeshi la akiba alafu avae nguo za khaki


20250111_070648.jpg
20250111_070710.jpg
20250111_070710.jpg
20250111_070657.jpg
20250111_070701.jpg
20250111_070705.jpg
 
Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza baada ya Tanganyika kupata Uhuru na Tanganyika ilipoungana na Zanzibar kuunda Tanzania.

Mwalimu yeye ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati wa vita ya Kagera na kwenye harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika.

Ukiachilia mbali Mwalimu, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete yeye alikuwa ni mwanajeshi kabla hajawa Rais.

Lakini sina kumbukumbu kama hao maris wanne wa Tanzania enzi wakiwa ni Marais wa Tanzania, waliwahi kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao.

Kama Kuna kumbukumbu za Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao, naomba niwekewe ili nibadili mafaili kwenye kumbukumbu za mbongo yangu.
Washamba waliopata Urais kwa fluku ndiyo wanavaa hayo makombati
 
Back
Top Bottom