Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,932
- 39,766
Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza baada ya Tanganyika kupata Uhuru na Tanganyika ilipoungana na Zanzibar kuunda Tanzania.
Mwalimu yeye ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati wa vita ya Kagera na kwenye harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika.
Ukiachilia mbali Mwalimu, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete yeye alikuwa ni mwanajeshi kabla hajawa Rais.
Lakini sina kumbukumbu kama hao maris wanne wa Tanzania enzi wakiwa ni Marais wa Tanzania, waliwahi kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao.
Kama Kuna kumbukumbu za Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao, naomba niwekewe ili nibadili mafaili kwenye kumbukumbu za mbongo yangu.