Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,904
- 31,974
NYERERE DAY: TUWAKUMBUKE MASHUJAA HAWA WAWILI KWA PAMOJA ABDULWAHID KLEIST SYKES NA JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Leo tarehe 13 Oktoba ndiyo siku aliyozikwa Abdul Sykes siku ya Jumapili mwaka wa 1968.
Fumba macho yako na lete picha ya Mtaa wa Lindi, Gerezani mwaka wa 1968 umma mkubwa umefurika nyumbani kwa Bi. Mruguru bint Mussa watu wako kwenye msiba Abdul Sykes amefariki na maziko yake ndiyo yanasubiriwa.
Dar es Salaam ilikuwa haijapata kushuhudia mazishi makubwa kama haya.
Watu wamefurika mtaa mzima na mitaa ya jirani wanasubiri maiti ipelekwe msikiti wa Kitumbini kwa ajili ya sala ya jeneza kisha mwili ukazikwe makaburi ya Kisutu.
Julius Kambarage Nyerere amekaa barazani nyumbani kwa Bi. Mruguru katika jamvi yuko na Ahmed Rashad Ali na watu wengine maarufu katika mji wa Dar es Salaam.
Katika hawa watu maarufu ni Chief Abdallah Said Fundikira.
Yeye ametokea Nairobi Makao Makuu ya East African Airways ambayo yeye alikuwa Mwenyekiti wa shirika hilo.
Chief Fundikira amekuja kumzika rafiki yake.
Katika baraza hiyo yuko Zuberi Mtemvu, Shariff Abdulkadir Juneid, Rashid Mfaume Kawawa, Ali Mwinyi Tambwe kwa kuwataja wachache.
Mwezi Oktoba jua ni kali sana Dar es Salaam na joto lake linakithiri.
Mwalimu Nyerere ametulia tuli jamvini anasubiri maziko.
Mwili uko tayari waliokuwa wanashughulika ndani walikuwa masheikh wawili maarufu mjini Dar es Salaam, Maalim Mohamed Matar na Sheikh Kassim bin Juma siku hizo anafahamika zaidi kwa jina la Darwesh.
Kabla jeneza alijatoka Mwalimu Nyerere ameomba aruhusiwe kumwaga rafiki yake Abdul Sykes.
Nyerere ameomba auone uso wa Abdul Sykes kwa mara ya mwisho.
Mwalimu akafahamishwa kuwa Waislam hawafunui maiti hivyo akasimama kwa dakika chache kisha akatoka nje.
Usifumbue macho yako bakia hivyo hivyo vuta picha jeneza limetoka na likagombewa kupokelewa Mwalimu Nyerere wasaidizi wake wamemweke nyuma ya jeneza katikati analiangalia jeneza.
Siku ile ulinzi ulikuwa umeimarishwa pakubwa kwa sababu kulikuwa na mgogoro mkubwa wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) mgogoro ambao haujapata kutokea.
Taarifa za kijintelijensia zilikuwa zinasema kuwa Waislam wamekasirishwa na msimamo wa serikali na kuna hofu huenda kuwepo kwa Nyerere mazikoni pale kunaweza kuzua vurugu.
Paul London alikuwa rafiki ya baba yangu na watu wakifanyakazi Exchange, moja ya Idara za Posta ikishughuika na mawasiliano ya simu.
Paul London alikuwa rafiki ya Abdul Sykes.
Katika uimarishajiwa ulinzi siku ile kwa bahati mbaya bila kukusudia kwa jinsi watu walivyoshonana, Paul London alikatiza mbele ya Nyerere.
Watu wa usalama wakambana huku na huku wakaendanae pembeni wakamchuua hadi Central Police.
Baada ya maziko walimwachia baada ya Pau London kueleza vyema uhusiano wake na marehemu.
Mwalimu alitembea kwa miguu kutoka nyumbani kwa Bi. Mruguru hadi Msikiti wa Kitumbini akasimama nje kusubiri sala ya jeneza.
Nje ya msikiti kulikuwa na umma mkubwa.
Siku zile maduka ya jirani na msikiti mengi yalikuwa ni maduka ya Wahindi washoni wa nguo.
Muhindi mmoja kuona Mwalimu kasimama akachuua kiti kumpelekea akae.
Mwalimu akakataa kukaa akabakia kasimama.
Maiti ilipotoka Mwalimu akawa bado yuko nyuma ya jeneza Abdul Sykes anamsindikiza rafiki yake hadi Makaburi ya Kisutu alipozikwa.
Mwalimu hakupata baada ya siku hii kushiriki katika maziko yoyote yale kwa nama hii.
Msomaji wangu naamini unajiuliza nini sababu ya Mwalimu Nyerere kufanya hivi?
Imesadifu kuwa vifo vya marafiki hawa wawili wazalendo, Abdul Sykes na Julius Nyerere vimefuatana tarehe zao katika mwezi huu wa Oktoba kama kadi zao za TANU zilivyofatana.
Huwezi kuandika historia ya Nyerere ukamwacha Abdul Sykes nje ya kurasa zako kwani utakuwa umeidhulumu historia ya Tanzania na umejidhulumu mwenyewe katika utafiti wako.
PICHA: Kulia ni Nangwanda Lawi Sijaona, Abdul Sykes, Julius Nyerere na Dossa Aziz kwenye hafla ya kumuaga Nyerere safari ya pili UNO mwaka wa 1957.
Msikiti wa Kitumbini kama ulivyo sasa.
Msikiti unafanyiwa ukarabati mkubwa.