Nyani anapoanza kufa huona miti yote huteleza !

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,749
Kwa kweli naiona Tanzania inavyoingia kwenye shida za kujitakia ingawa uoni huo ni kwenye horizon.

Suala la Zanzibar ni la uzito wa haki za binadamu wala sio CUF au Chadema au CCM ,uchaguzi umefanyika wananchi wamechagua na matokeo kuanza kutangazwa.

Nani alimshauri Jecha kufuta uchaguzi ? Ni suala la muda tu lakini litakuja juu na kila mmoja ataelewa.

nani alimshauri vibaya Mh.magufuli nalo ni suala la muda tu ,Tulimsikia Mheshimiwa akiwakoromea CCM wa ILALA ,hapa aliposema tu CCM waliokuwa wakilizingira umeya wakaingia mitini ,sasa iweje aliweza kuingilia CCM waliokuwa wakinyemelea ILALA na kuwaacha na kukaa kimya kwa CCM wa Zanzibar ,ambao aliambiwa kuwa aliingilie kati ,ila alikaa kimya na kuona bora ILALA kuliko Zanzibar.
Kwa kweli hali ya ILALA imemsuta kwani Chama ni hichohicho kilichotokea Zanzibar ndicho kilichotaka kufanyika ILALA.

Shida na dhiki zinazoanza kupaa ,Mheshimiwa hatoweza kuzikabili kwani Tanzania ni nchi kubwa sana yenye wananchi wanaokaribia milioni hamsini ,wengi wao wasio na kazi ila mahitaji yao wanaitegemea serikali.

Tusiparamie gesi,mapato ya kodi madini yote hayo yanaendeshwa kimataifa wala usidhani una gesi,mafuta na madini ukategemea utauza unavyotaka ,msikilize Mwalimu Nyerere anasema vitu vyetu ila bei na wanunuzi wanapanga na kutoka majuu.

nani alimdanganya mh.magufuli ? kuwa suala la kupindwa kwa haki za binadamu Zanzibar litapoa na kumalizwa kikawaida na kirahisi ? Mbona wamemuingiza mkenge na kumuharibia uongozi wake ambao upo kwenye mstari ulioonekana kuitangaza Tanzania.


Magufuli jahazi litakapoanza kuzama wale wote waliomshauri suala la Zanzibar hatawaona tena wakigonga milango ya Ikulu na watakuwepo mbali wakichekelea ,kwani lengo lao la kumuharibia limetimia.

Kama ilikuwa siri kuwa Tanzania inakandamiza haki za binadamu sasa itakuwa dhahiri ,sijui China Japan wote hao lao moja ,ila kila jambo ni timings tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…