Under-cover
JF-Expert Member
- Nov 13, 2023
- 1,557
- 2,582
nawaambiaga watu kila day hapo mwishoni mistari 3, wakishua au waliotoka kwenye stable economic atleast.Pole sana kaka, ila pia niseme tu kwamba ulikosea tangu mwanzo, ulivyomfungulia hiyo ofisi ulimuachia majukumu yote ya kiofisi yawe juu yake kwahiyo hii imefanya ajisahau na ahisi ni biashara yake peke yake. So hiyo mistake sijui unawezaje kuirekebisha tena coz ulitakiwa kila siku mpige hesabu wote na uwe unatembelea ofisi mara kwa mara na uoneshe kuijali hiyo sehemu na hii ingemfanya ajue kwamba hiyo biashara ni ya familia sio yake peke yake.
Kingine inaonekana mkeo hajawahi kushika pesa nyingi kwenye maisha yake so kutokana na hiyo hali ilifanya asiwe na uhuru wa kifedha kupelekea kutokuyaishi yale maisha ya ndoto yake. Kwahiyo hivyo vyote unavyoviona anafanya sasa hivi ujue ndio vitu ambavyo anavipenda na ndio vipo kwenye damu yake so ni vile tu wewe umechelewa kumjua mapema kwasababu hakuwa na pesa na wewe uliyokua unamuachia ilikua nje ya budget zake.
Kwahiyo sio kwamba ndoa yako iko matatani ila ni kwamba mkeo anaishi uhalisia wa maisha yake na amekua huru zaidi kwa namna ile ambayo wewe haukuizoea kwenye miaka 12 or 13 iliyopita.
Mkeo yuko na financial freedom now so kama ulizoea kumpangia majukumu na kufuata hizo orders zako now hafanyi coz ako na uhuru wa kifedha na anauwezo wa kujiamulia kwasababu haumbabaishi tena.
Ushauri wangu kwako ni unaweza kufanya jambo moja kati ya haya mawili, moja ni ufanye namna umfilisi ili arudi tena kuwa mama wa nyumbani na ale msoto miezi kadhaa then ndio umfungulie tena ofisi na mara hii make sure wewe ndio unakua the main player kwenye hiyo ofisi utakayo ifungua.
Mbili, ishi kwa namna anavyotaka yeye yaani uyakubali hayo mabadiliko ya mkeo na uyazoee but uendelee kuplay part yako as a man na baba wa familia huku ukijitahidi kumfanya mkeo awe rafiki yako, kama ni out umtoe coz skuizi anapendeza na kunukia usipomtoa wewe watamtoa wenzio na nguo nzuri mnunulie pamoja na hizo manukato anazopenda, najua itakua ngumu ila ndani ya miezi mitatu utaona furaha ya ndoa yako tena.
NB: Vijana ambao hamjaoa make sure mnaoa wanawake ambao wamezoea kushika pesa na wako stable financial or their mindset kwenye pesa imetulia.