BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 497
- 1,202
Mimi ni mkazi wa Arusha, kero yangu ni kuhusu Ofisi ya NSSF Arusha, kuna usumbufu mwingi wanaofanyiwa baadhi ya watu wanaoenda kudai mafao.
Awali, niliambiwa na wenzangu kuhusu usumbufu uliopo kwenye taasisi hiyo na uwepo wa mazingira ya kutengenezwa kutoa ‘kitu kidogo’.
Nilifika hatika ofisi hizo wiki kadhaa zilizopita kufuatilia mafao yangu, ikabainika kuna sehemu jina langu limetofautiana na lililopo katika kitambulisho change cha NIDA, kuna herufi ambayo imeingia nah ivyo kutofautiana na jina lililopo kwenye nyaraka za NSSF.
Nikataka kubadili kitambulisho cha kutumia ili nitumie Leseni ya Udereva kwa kuwa sehemu ya masharti yao yanaeleza kuwa unaweza kutumia kitambulisho cha NIDA au Leseni ya Udereva kufuatilia mafao yako, Watumishi wa hapo wakakataa nisitumie Leseni yangu.
Nikatakiwa kuonana na Mwanasheria wao kwa ajili ya kutengeneza ‘affidavit’, nikatimiza hilo ili nipatiwe kitambulisho na kuendelea na mchakato unaofuata.
Hapo ndipo kazi ilipoanzia, nikaanza kupigwa danadana kila siku, njoo kesho zikawa nyingi, nikiuliza sababu naambiwa hakuna ‘network’, lakini ajabu wapo wengine ambao tena walinikuja mbele yangu wakawa wanapata huduma kama kawaida.
Nilipojaribu kuuliza waliokuwa wanapata huduma wakawa wananiambia “jiongeze”, baada ya muda nikaamua kumfuata kiongozi mmoja wa hapohapo NSSF Arusha na kumueleza shida yangu.
Akaniomba nyaraka nilizokuwa nazo zote, akaenda idara husika kuwauliza nini kimekwamishwa mimi kupata huduma hiyo, wakaanza kutafuta katarasi zangu, zikakutwa chini kabisa kwenye mafaili yao, wakati huohuo nilikuwa nimeambatana na jamaa mwingine ambaye naye alikuwa na shida kama yangu, naye nyaraka zake zikatafutwa na kukutwa chini kabisa.
Yaani ni kama vile walizi ‘dampu’ nyaraka zetu wakisubiri “tujiongeze”, tabia hiyo ni tatizo na Serikali imulike kinachoendelea hapo, si rafiki kwa maendeleo ya nchi na ni mazingira ya rushwa ya wazi kabisa.