simplemind
JF-Expert Member
- Apr 10, 2009
- 16,418
- 9,207
Pamoja na Dr Shein kuendelea kuwa Rais kwa kutumia kifungu tata cha katiba, Novemba 12 Zanzibar itazidi kutumbukia kwenye mgogoro wa kikatiba kutokana na kotokuwepo wawakilishi.
Kifungu cha 90(1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 kinaeleza kwamba:
"90.(1) Wakati Baraza litakapovunjwa, Uchaguzi Mkuu wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi utafanywa na mkutano wa mwanzo wa Baraza jipya utafanywa si zaidi ya siku tisini toka kuvunjwa kwa Baraza."
Baraza la Wawakilishi lililopita lilivunjwa tarehe 13 Agosti, 2015. Kwa maana hiyo, kwa mujibu wa kifungu cha 90(1) cha Katiba ya Zanzibar, Baraza jipya linapaswa kuitishwa si zaidi ya tarehe 12 Novemba, 2015.
Kwa mujibu wa kifungu cha 29 na 92(2) cha Katiba hiyo, Baraza la Wawakilishi linaweza tu kuongezewa muda iwapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakapokuwa kwenye vita.
Kwa msingi huo, sasa hivi hakuna Baraza la Wawakilishi ambalo ndiyo chombo cha wananchi wa Zanzibar kinachoisimamia Serikali yao, na Baraza jipya linapaswa kuitishwa si zaidi ya siku tisini tokea Baraza lililopita lilipovunjwa.
Kwa maana hiyo, ifikapo tarehe 12 Novemba, 2015 ni lazima Baraza jipya lililochaguliwa tarehe 25 Oktoba, 2015 liitishwe na lisipoitishwa, nchi yetu itaendelea kutumbukia kwenye mgogoro mkubwa zaidi wa kikatiba na kiutawala.