DOKEZO Nkasi, Rukwa: Watumishi Ajira Mpya hatujalipwa Fedha za Kujikimu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Teacher Himself 255

New Member
Sep 29, 2023
2
1
Habari wana JF,leo napenda niongelee ubabaishaji wa halmashauri zetu kwenye kuwapa stahiki zao waajiriwa.

Tunakumbuka mwezi wa 6 mwaka huu 2023 serikali iliajiri watumishi wapya kada ya afya na elimu na pia ikasisitiza wapewe fedha za kujikimu.

Napenda nipongeze kwa halmashauri zote ambazo washawapa waajiriwa wapya fedha zao..

Lakini kwa halmashauri yetu ya Wilaya ya Nkasi bado hatuelewi mpaka sasa kama watatupa fedha hizo au la.Naomba mamlaka zinazohusika ziingilie kati katika hili na wachunguze kwanini wanachelewesha fedha za kujikimu kwa ajira mpya.

Unaweza kukuta halmashauri zenye ubabaishaji huwa zinafungua fixed account kwa fedha zinazotakiwa kuwafikia watumishi walio chini ya halmashauri husika.

Naomba TAMISEMI na Wizara ya Utumishi wasimamie katika hilo kuzichunguza halmashauri zetu.
 
Kama tunakumbuka tarehe 03 Oktoba 2023 Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI Mchengerwa aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote kulipa fedha za kujikimu kabla ya tarehe 30 Oktoba.

Lakini hali imekuwa tofauti kwa halmashauri ya wilaya Nkasi ambapo mpaka leo hii tarehe 31 Oktoba, waajiriwa wapya kada ya elimu na afya hatujapewa hela ya kujikimu na kila tukiuliza wao wanasema wanashughulikia.

Tunaomba TAMISEMI iingilie kati ili tuweze kupata haki yetu.
 
Back
Top Bottom