Njombe: Afariki ndani ya gari akiota moto kwenye jiko la mkaa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,790
Thadei Mbawala (48) mkazi wa mtaa wa Mji Mwema halmashauri ya mji wa Njombe ambaye ni dereva wa gari ya kampuni ya maji anadaiwa kufariki dunia ndani ya gari aliyokuwa amepaki nyumbani kwake pembeni kukiwa na jiko la mkaa huku milango ya gari ikiwa imefungwa.

Kituo hiki kimefika nyumbani kwa Mbawala na kuzungumza na Bi. Catherine Haule mke wa marehemu ambaye amesema mumewe ana kawaida ya kuchaji radio pamoja na simu yake ndani ya gari kila anaporejea nyumbani kwa kuwa nyumba yake haina umeme lakini siyo kwenda na kigai pamoja na blanketi kwenye gari.

"Aliporudi jana saa tatu akawa anaendelea na shughuli zake na hapa ndani kuna kigai chake, huwa anaota moto akirudi nikajua kipo kumbe mwenzangu alishachukua pamoja na shuka la watoto huko ndani, sina hili wala lile akaniambia mimi nachaji radio na kile cha kunyolea ndevu nikamwambia sawa mimi naenda kulala akasema tangulia ila milango usifunge" Amesema Catherine Haule, mke wa marehemu.

Amesema mara baada ya kushtuka majira saa kumi na mbili asubuhi kutokana na kupitiwa na usingizi alishangaa kuona mume wake hayupo ndani lakini alipokwenda kwenye gari alifika na kuanza kumuita mume wake lakini milango ilikuwa imefungwa jambo lililomfanya aanze kuomba msaada kwa majirani waweze kumsaidia.

Teophil Mwinuka ni Mtendaji wa kata ya Mji Mwema amesema mara baada ya viongozi kupata taarifa walifika eneo la tukio na kuwapigia simu kampuni ya maji ambao walifika na ufunguo mwingine wa gari walioutumia kufungua mlango na kukuta Mbawala akiwa ameshafariki.

Hata hivyo wakati tukio hili likitokea, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Banga alitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Njombe wakati huu wa majira ya baridi kuchukua tahadhari kwenye matumizi ya jiko la mkaa ambapo watu sita wameripotiwa kufariki dunia kuanzia mwaka 2021 kutokana na matumizi ya jiko la mkaa.
 
Carbon monoxide or Carbon Dioxide effects?
Wataalamu wabobevu wa masuala ya Chemistry tusaidieni kwenye hili.
 
Milichomuua kimesababishwa na gesi ya carbonmonoxide! Ni gesi yenye sumu ambayo haina harufu. Si vyema kuwasha jiko la mkaa ndani ya nyumba kwani inaweza kusababisha vifo.
 
Mimi nipo Primary najua Kukaa jirani na Jiko la Mkaa huku kukiwa hakuna Hewa ya kutosha = Na Kifo....!

Na hata Sasa nimekua Mtu mzima, kila wakati ningemkumbusha kuhusu Hilo na Watoto pia ningewapa Elimu..!

Kinachonishangaza kuona Watu wazima Bado wanapoteza Maisha kisa Jiko la Mkaa...!
 
Mikoa ya baridi kama Njombe inabidi serikali ihakikishe inaweza umeme na heater za umeme kwa Kila familia. La sivyo baridi ya kule Makete, ipelele ward itaendelea kuua watu sana. Pole Kwa familia
 
Niliendaga tanga huko juu milima ya usambara,kuna baridi kali
Usiku tulipokuwa tuko ndani alikuja mama mmoja akatuambia
Nimewaleteeni kuni zenye moto atuweke ndani ili kuwe na joto!
Nkamwambia mama asanteee...Acha tu tutalala hivi hivi
πŸ˜„

Ova
 
Mikoa ya baridi kama Njombe inabidi serikali ihakikishe inaweza umeme na heater za umeme kwa Kila familia. La sivyo baridi ya kule Makete, ipelele ward itaendelea kuua watu sana. Pole Kwa familia
Heater wakiwekea wataiweza mziki wake kwenye bill ya umeme

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…