Njia zipi unatumia kudhibiti upotevu wa Data

morees

JF-Expert Member
Apr 21, 2019
288
614
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na ungezeko la gharama za vifurushi vya internet DATA.

Ebu tushauriane hapa njia zipi hasa zitasaidia kupunguza matumizi ya DATA.

Mimi huwa najiuunga Gb9.5 kifurushi cha mwezi ila mara zote huisha ndani ya wiki mbili tu.

Nimejaribu kupata apps ambazo zinasaidia kupunguza matumizi ya DATA kama Stayfree na my Data manager.
Weka zingine tupate ufumbuzi.
 

Attachments

  • 20230811_114600.jpg
    20230811_114600.jpg
    10.2 KB · Views: 1
Unatumia simu gani?

Mi pixel (Android), my tips:

Muda wote data saver ipo ON.
Nina tabia ya kufreeze App.
Muda mwingi Battery Saver ipo ON.
Hakuna App inayo run Background.
Synchronization ipo OF.
Kazini natumia sana WiFi.
Kwenye WhatsApp autodownload za media ipo OFF.
App ambazo sijazitumia zaidi ya week 2 nazitoa. Nitazidownload nikihitaji.
Sijawahi update App kwa kutumia data.

Another Tips:
Kama upo jirani na nyaya za TTCL fanya mchakato.
Kama una majirani watatu mnaishi nyumba ipo karibu karibu mnaweza kuchanga mkajiunga na internet service providers wale wa kulipia kwa mwezi elfu 70-80 mkashare.
 
Back
Top Bottom